Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Amani iwe nanyi wadau!
Kwa wapenda mabadiliko wenzangu napenda kuwasalimu kwa furaha sana. Furaha Hii ni kwa sababu Kuu kuwa ile siku yetu muhimu i karibu sana. Tumebakiza siku Saba watanzania tuandike historia kuu, itakayosomwa na kuheshimiwa na vizazi na vizazi.
Naomba nirudi kwenye mada. Leo Kiongozi wa ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif ametoa maneno mazuri na mazito sana akimzungumzia Mgombea wao wa kiti ya Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Ndugu Bernad Kamilius Membe kuwa kama Chama kimeshaamua kumuunga mkono Tundu Antiphas Lissu hivyo pamoja na yeye kuwa mgombea hivyo aheshimu maamuzi ya Chama.
Baada ya maneno haya ya Maalim Seif, CCM wameamua kuuvalia njuga huu mjadala kujaribu kuleta picha kuwa hili suala linaweza kuharibu kura za upinzani.
Napenda kuwapa pole sana wana CCM kwa hoja zao hizi mfu wanazojaribu kuzileta kwa sababu kamwe haziwezi fanikiwa na hii ni kwa sababu zifuatazo.
1. Wapenda Mabadiliko waliojitoa kweli kufanya mabadiliko mwaka huu walishajua kuwa Membe si mwana mageuzi. Walijua kuwa yeye ni Lumumba project na walikuwa wanasubiri tu muda ufike aoneshe rangi zake halisi. Mungu anatupenda sana Watanzania rangi halisi za Membe zimeshaonekana. Hivyo suala la Membe kukataa kumuunga mkono Lissu kamwe haliwezi kuwastaajabisha Watanzania. Huyu anajulikana na alishaonekana tangu awali.
2. Membe kumuunga mkono au kutomuunga mkono Tundu Antiphas Lissu haiwezi kupunguza vyovyote kura za kimbunga atakazopata Tundu Antiphas Lissu mwaka huu. Watanzania wengi wameshaamua kwenda na Lissu na kuachana na Magufuli na CCM yake baada ya miaka zaidi ya 50 ya mateso chini ya CCM. Anachofanya Membe ni michezo ya kitoto ya Miaka ya 70 ambapo propaganda ndo zilikuwa na nguvu kuliko ukweli.
Napenda kumaliza kwa kusema vyovyote vile kwa kuungwa mkono na Membe au kutoungwa mkono na Membe, Watanzania tumeshaamua mwaka huu kuwa tunaenda na Tundu Antiphas Lissu. Mpakwa mafuta wa Mungu aliyeponywa risasi 16.
Viva Lissu, Viva Chadema.
#LissuforPresident