Bernard Membe yupo kweli?

Bernard Membe yupo kweli?

Anayevuma kwa sasa ni Tundu Lissu tu.

Na si kwamba anavuma kwa sababu ana sera bora na anazinadi kwa ustadi!

La hasha.

Anavuma tu kwa kelele kelele anazozipiga akiwa huko kwenye mizunguko yake ya kutafuta wadhamini.

Sasa ikija kwa Bernard Membe, si ajabu ukimwuliza Mtanzania wa kawaida barabarani kuwa jana au leo Membe alikuwa wapi, sidhani kama kuna mtu ataweza kukuambia.

Kwa Lissu hali ni tofauti kabisa. Majuzi ile alikuwa Ikungulyabashashi. Juzi alikuwa sijui Arusha au Kilimanjaro. Jana alikuwa Iringa au Morogoro....

Sasa huyo ‘jasusi mbobezi’ yeye yuko wapi?

Hata vile vijembe vyake dhaifu kule Twitter naona hatoi tena.

Isije akawa keshaguswa na sasa ananuka!

Jamaa ni dhaifu sana. Siasa naona haimkubali. Haiba yake haiendani na mikikimikiki na mashamsham ya kisiasa.
Subiri ana kuja. Usiwe na haraka maana kuna watu mtapelekwa hosipitali
 
Sasa kama unajua mahali Lisu alipo mbona 'sijui, au' zipo nyingi sn? Wewe siunafahamu exactly mahali alipo?
Nimetumia neno ‘sijui’ mara moja tu kwenye bandiko zima!

Hizo ‘sijui’ nyingi sana wewe umeziona wapi?

Nionyeshe tafadhali:
 
Tundu Lissu : Tunataka Uhuru na Kazi, Uhuru na Maendeleo ,Uhuru na Umoja. Utu wa mtanzania lazima urudishwe kutoka kwa hawa CCM Mpya hatuwezi kubezwa na kunyanyaswa katika nchi yetu Tanzania.

Mkuu, nikiyataja si nitakuwa nimetukana tena? Kwa kweli staji mkuu

Kimsingi hakuna matusi kwa maana ya matusi, ila ni ukweli mchungu unaowakilishwa kwa lugha kali. Kama Shetani angeweza kushitaki, usishangae angeenda kuwashitaki watumishi wote wa Mungu kwa jinsi wanavyomkemea kwa lugha kali kwa kuingiza watu kwenye dhambi. Nikuambie tatizo lilipo boss, ni kwamba Magu hawezi siasa za ushindani, na kwa bahati mbaya anapenda kusifiwa jambo ambalo sio baya. Ila anaamini kusifiwa ni haki yake ya msingi, hivyo anapokutana na mtu asiyemsifia kabisa, huku akitaja madhaifu yake waziwazi, tafsiri yake hayo ni matusi. Na kwa bahati mbaya hata wafuasi wake amewaambukiza udhaifu wake, kiasi hata nyie mnaona hayo ni matusi na mkikwepa ukweli anaopewa.

Kama kuna siku angekuwa ametukanwa kile kiungo uzazi cha mzazi wake wa kike, hapo ningesema kuwa kweli alitukanwa, lakini kuambiwa kuwa amepora uhuru wa bunge, mahakama, wa vyombo vya habari. Ama kuambiwa kuwa anamiliki makundi ya kihalifu, na hataki kukosolewa, hapo kuna matusi gani zaidi ya ukweli?
 
Anayevuma kwa sasa ni Tundu Lissu tu.

Na si kwamba anavuma kwa sababu ana sera bora na anazinadi kwa ustadi!

La hasha.

Anavuma tu kwa kelele kelele anazozipiga akiwa huko kwenye mizunguko yake ya kutafuta wadhamini.

Sasa ikija kwa Bernard Membe, si ajabu ukimwuliza Mtanzania wa kawaida barabarani kuwa jana au leo Membe alikuwa wapi, sidhani kama kuna mtu ataweza kukuambia.

Kwa Lissu hali ni tofauti kabisa. Majuzi ile alikuwa Ikungulyabashashi. Juzi alikuwa sijui Arusha au Kilimanjaro. Jana alikuwa Iringa au Morogoro....

Sasa huyo ‘jasusi mbobezi’ yeye yuko wapi?

Hata vile vijembe vyake dhaifu kule Twitter naona hatoi tena.

Isije akawa keshaguswa na sasa ananuka!

Jamaa ni dhaifu sana. Siasa naona haimkubali. Haiba yake haiendani na mikikimikiki na mashamsham ya kisiasa.

Jiwe naye yuko wapi? Jana alikuwa wapi na kesho je? Nani anajua?

Lissu tunafahamu kwa sababu yeye ni mfu aliyefufuka.

Hata pamoja na makatazo yenye ahadi za vipigo vya mbwa koko waungwana hawakuvumilia kwenda kumwona mfufuka tangia JKNIA.

Membe, Jiwe, Rungwe, Lipumba, yule wa TLP, NCCR nk hawa ni kina Harry na Tom tu. Binadamu wa kawaida wanaotafuta wadhamini.

Halipo jipya hapo.
 
Kama Shetani angeweza kushitaki, usishangae angeenda kuwashitaki watumishi wote wa Mungu kwa jinsi wanavyomkemea kwa lugha kali
😄😄😄😄😄

Daah, umefikilia nini mkuu, si unajua tena shetani yeye ni king'ang'anizi
 
Kwa nchi kama yetu, watu wengi ni wa hovyo Sana, ingawa ni Jambo la muhimu na lazima, Ila wengi badala ya kuongea ki staha, wanatukana tu Kwa kila Aina ya matusi

Na hata Mimi nigekuwa tu kama Magufuli,
Orodhesha hayo matusi hata matatu tu wanayotukana hao watu unaosema. Orodhesha tu labda hatuyasikii
 
Membe si jasusi tena kama wengi walivomezeshwa. Alitoka katika kitengo cha usalama muda mrefu sana kipindi cha Nyerere huko nyuma. Watu wengi wamepita na mifumo mingi imebadilika hana tena mizizi huko usalama wa taifa. Imebaki ni CV tu hata haiwezi fanya chochote.
Siku zote mahali pengi sana kachero mzoefu huwa hana kustaafu kazi bali upumzika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom