Bernard Membe yupo kweli?

Bernard Membe yupo kweli?

Anayevuma kwa sasa ni Tundu Lissu tu.

Na si kwamba anavuma kwa sababu ana sera bora na anazinadi kwa ustadi!

La hasha.

Anavuma tu kwa kelele kelele anazozipiga akiwa huko kwenye mizunguko yake ya kutafuta wadhamini.

Sasa ikija kwa Bernard Membe, si ajabu ukimwuliza Mtanzania wa kawaida barabarani kuwa jana au leo Membe alikuwa wapi, sidhani kama kuna mtu ataweza kukuambia.

Kwa Lissu hali ni tofauti kabisa. Majuzi ile alikuwa Ikungulyabashashi. Juzi alikuwa sijui Arusha au Kilimanjaro. Jana alikuwa Iringa au Morogoro....

Sasa huyo ‘jasusi mbobezi’ yeye yuko wapi?

Hata vile vijembe vyake dhaifu kule Twitter naona hatoi tena.

Isije akawa keshaguswa na sasa ananuka!

Jamaa ni dhaifu sana. Siasa naona haimkubali. Haiba yake haiendani na mikikimikiki na mashamsham ya kisiasa.
ni vyema pia kuuliza mbona bosi wa MATAGA naye tambo zake ambazo amekuwa akiziimba for the past 5 years zimepotea baada ya Lissu kuzi neutralise ndani ya wiki 1 tu?

tangu Lissu katinga mjini yaonekana kila mtu pichu imeminya nidaroko!
 
Siku zinayoyoma simsikii Membe kabisa huku bara nilimwona visiwani gafla amepotea Nini kimemtokea mliopo karipi naye?
Au ndio muungano wa ACT na chadema umekubaliwa?
 
Daaaa mkuu nilikuwa nadhani ni mlala hoi tu kama sisi
Nchi hii ione hivihivi, Lisu ataisaidia sana Chadema kuwa chama imara lakini Magufuli anapiga tano tena, ndio mfumo ulivyo huwezi kubadili kitu, wapo everywhere.

Ukiona mpaka masheikh na maaskofu wapo kwenye network ya watawala usipoteze muda wako.

Mbowe ajiandae mapema kukabidhi uenyekiti wa chama kwa Lisu ambaye ataindaa vyema Chadema kuchukuwa dola 2025.

Mnachopaswa kukuelewa ingawa wengi hamtokubali kuelewa, huwezi kumuondoa madarakani sitting President kwa mfumo wa Tanzania labda anapoondoka madarakani na kugombea urais wote mkiwa fresh candidate ambao mko powerless.
 
Sudan walikuwa na mfumo sawa na wakwetu na Zimbabwe ambao ni matunda ya Nyerere, lkn wananchi walipo amua kuwa basi ilikuwa basi.
 
Ameona kazi aliyotumwa na ccm kuifanya upinzani inazidi kuwa ngumu na inashusha hadhi yake. Anafikiria kumwambia aliyemtuma atafute mtu mwingine maana yeye hafahamiki zaidi ya kamati kuu ya ccm na kijijini kwao tu.

Anaona Tundu Lissu anazidi kupeta tu
 
Kabisa!

Ila hao watawala nao ni wapumbavu tu.

Katika zama hizi ni kazi bure kupiga marufuku vyombo vya habari kutangaza habari.

Washamba wanajua hilo? Wao ni nguvu tu kwa kwenda mbele. Wanajua wakibana vyombo vya habari ndio watapata mvuto.
 
Kwa nchi kama yetu, watu wengi ni wa hovyo Sana, ingawa ni Jambo la mhimu na lazima, Ila wengi badala ya kuongea ki staha, wanatukana tu Kwa kila Aina ya matusi

Na hata Mimi nigekuwa tu kama Magufuli,

Huwa ninacheka sana nikisikia watu wanasema eti wapinzani kazi yao ni kutukana. Fuatillia vizuri hayo yanayoitwa matusi, utakuta ni ule ukweli ambao wapambe wanaowazunguka watawala hawawezi kuwaambia, na kwa vile ukweli huo hawaambiwi kwa lugha ya kuremba, ndio inabidi waseme ni matusi ili kupoteza ukweli usifahamike. Kwasababu ww ni muelewa wa kiwango cha kuridhisha, hebu weka hayo matusi wangalau mawili tuyaone.
 
Sudan walikuwa na mfumo sawa na wakwetu na Zimbabwe ambao ni matunda ya Nyerere, lkn wananchi walipo amua kuwa basi ilikuwa basi.
Jiandae kisaikolojia, matokeo ya Urais Tanzania yakishatangazwa hayahojiwi popote.

Tanganyika kamwe haiwezi kufanya mabadiriko kabla ya Zanzibar kutokea mabadiriko na ccm ikubali kumkabidhi ushindi wake Maalim Seif.

Lakini tatizo ile salaam yao ya Mapinduziiiii Daimaaaaaa ndio penye shida.
 
Back
Top Bottom