M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,027
ni vyema pia kuuliza mbona bosi wa MATAGA naye tambo zake ambazo amekuwa akiziimba for the past 5 years zimepotea baada ya Lissu kuzi neutralise ndani ya wiki 1 tu?Anayevuma kwa sasa ni Tundu Lissu tu.
Na si kwamba anavuma kwa sababu ana sera bora na anazinadi kwa ustadi!
La hasha.
Anavuma tu kwa kelele kelele anazozipiga akiwa huko kwenye mizunguko yake ya kutafuta wadhamini.
Sasa ikija kwa Bernard Membe, si ajabu ukimwuliza Mtanzania wa kawaida barabarani kuwa jana au leo Membe alikuwa wapi, sidhani kama kuna mtu ataweza kukuambia.
Kwa Lissu hali ni tofauti kabisa. Majuzi ile alikuwa Ikungulyabashashi. Juzi alikuwa sijui Arusha au Kilimanjaro. Jana alikuwa Iringa au Morogoro....
Sasa huyo ‘jasusi mbobezi’ yeye yuko wapi?
Hata vile vijembe vyake dhaifu kule Twitter naona hatoi tena.
Isije akawa keshaguswa na sasa ananuka!
Jamaa ni dhaifu sana. Siasa naona haimkubali. Haiba yake haiendani na mikikimikiki na mashamsham ya kisiasa.
tangu Lissu katinga mjini yaonekana kila mtu pichu imeminya nidaroko!