Bernard Membe yupo kweli?

Bernard Membe yupo kweli?

Kapotea hata kampen hazijafika muda wake.
Wewe ni Ngabu kweli, Sisi kwetu Jina Ngabu linamaanisha, ni mtu ambaye Kwa Wakati Fulani, njaa imemshika,bahati Nzuri pengine akakutana na mtu akampatia karanga za kutafuna, Wakati wakiachana tu na huyo mtu aliyemgea karanga, Mbele yake akamwona mtu ambaye naye ananjaa, huyo mtu akataka kuomba karanga Ili ale, matokeo yake aliyeombwa, akaztupia zote mdomoni mwake akimwambia Yule jamaa aliyeomba kuwa, nimemaliza karanga na mdomo umejaa karanga asiweze hata kuongea vizuri, hiyo ndio inaitwa amezi Ngabu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]duh
 
Anayevuma kwa sasa ni Tundu Lissu tu.

Na si kwamba anavuma kwa sababu ana sera bora na anazinadi kwa ustadi!

La hasha.

Anavuma tu kwa kelele kelele anazozipiga akiwa huko kwenye mizunguko yake ya kutafuta wadhamini.

Sasa ikija kwa Bernard Membe, si ajabu ukimwuliza Mtanzania wa kawaida barabarani kuwa jana au leo Membe alikuwa wapi, sidhani kama kuna mtu ataweza kukuambia.

Kwa Lissu hali ni tofauti kabisa. Majuzi ile alikuwa Ikungulyabashashi. Juzi alikuwa sijui Arusha au Kilimanjaro. Jana alikuwa Iringa au Morogoro....

Sasa huyo ‘jasusi mbobezi’ yeye yuko wapi?

Hata vile vijembe vyake dhaifu kule Twitter naona hatoi tena.

Isije akawa keshaguswa na sasa ananuka!

Jamaa ni dhaifu sana. Siasa naona haimkubali. Haiba yake haiendani na mikikimikiki na mashamsham ya kisiasa.
Kwani campaign tayari shosti au
 
Bado anasubiri "Tsunami ya vigogo" na wanachama wapya toka mikoa ya Lindi, Mtwara, wanaokuja kunogesha kampeni pamoje naye. The question is: Kachero gani mbobezi asiyeweza ku-assess situation on the ground?!!
 
Dogo tuseme hili mara ngapi ili uelewe? Tume bado haijapitisha wagombea, kwahiyo hakuna kitu kama hicho. Ni propaganda za WAHUNI WACHACHE huko CCM, umeelewa sasa?

ITOSHE TU KUSEMA, MITANO YA UTAWALA HUU WA MKONO WA CHUMA SASA BASI..
Unachokisema na anachofanya muuzaji Lissu ni vitu viwili tofauti. Itoshe tu kusema Magufuli mitano mingine. Najua unaumia lakini haina namna vumilia tu Ikulu si mahali pa wauza nchi kama akina Lissu. Bahati nzuri hata yeye mwenyewe Lissu hatajipigia kura, atampigia JPM, the best of the best presidents in Africa.
 
Bernard Membe ana hali gani huko kwenye campaign trail?🤣
 
Membe yupo japo mambo sio mambo
 

Attachments

  • kumbushodawson_20200905_154128_0.jpg
    kumbushodawson_20200905_154128_0.jpg
    58.8 KB · Views: 3
CCM waliona mbali maana jamaa angeishia njiani kama hivi na kumuunga mkono mgombea wa upinzani.
 
Back
Top Bottom