Besigye ashindwa Kesi ya kumrejeshea Martha Karua na Lukwago katika timu yake ya Mawakili

Besigye ashindwa Kesi ya kumrejeshea Martha Karua na Lukwago katika timu yake ya Mawakili

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
Mahakama Kuu ya Kampala nchini Uganda imekataa ombi la Dkt. Kizza Besigye na Obeid Lutale la kurejesha mawakili Martha Karua na Erias Lukwago katika timu yao ya utetezi.

Jaji Simon Peter Kinobe, katika uamuzi wa kurasa 42 uliotolewa Jumanne, amesema kuondolewa kwa Karua nchini Uganda na kuzuiliwa kwa Lukwago hakukuvunja haki ya Besigye na Lutale kupata uwakilishi wa kisheria au kusikilizwa kwa haki.

Karua alizuiwa kuingia Uganda kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe mnamo Juni 22, 2026, na baadaye kutangazwa kuwa prohibited immigrant na kuondolewa nchini humo. Besigye na Lutale walipinga hatua hiyo wakisema iliathiri haki yao ya kuchagua mawakili wanaowataka.

Kwa upande mwingine, Lukwago alikamatwa na kuwekwa katika Gereza la Luzira kwa tuhuma zinazohusiana na kosa la misprision of treason, hali iliyomzuia kushiriki katika utetezi wa Besigye na Lutale.

Hata hivyo, Jaji Kinobe amesema Besigye na Lutale bado walikuwa na timu kubwa ya mawakili. Kwa mujibu wa mahakama, walikuwa wakiwakilishwa na takribani kampuni 13 za sheria zenye zaidi ya mawakili 50 waliowachagua wenyewe.

Mahakama pia ilizingatia kwamba kesi hiyo ilikuwa imeahirishwa mara kadhaa ili kuwapa muda wa kupanga upya timu yao ya utetezi pale changamoto za uwakilishi zilipojitokeza.

Kuhusu Karua, mahakama haikuamua ikiwa uamuzi wa mamlaka za uhamiaji wa kumzuia kuingia Uganda ulikuwa halali. Jaji alisema suala hilo linapaswa kupingwa kupitia judicial review, badala ya kutumia kesi ya kikatiba iliyowasilishwa na Besigye na Lutale.

Jaji pia alisema Karua angeweza kushiriki katika baadhi ya shughuli za kesi kwa njia ya mtandao iwapo mahakama ya kesi ingetoa ruhusa hiyo.

Kuhusu Lukwago, mahakama ilisema kukamatwa kwa wakili hakumaanishi moja kwa moja kwamba haki ya mteja wake ya kupata uwakilishi wa kisheria imekiukwa. Kinachopaswa kuthibitishwa ni ikiwa kutokuwepo kwake kuliathiri kwa kiasi kikubwa uwezo wa Besigye na Lutale kupata utetezi madhubuti.

Mahakama ilihitimisha kuwa hawakuweza kuthibitisha hilo na hivyo ombi lao likatupiliwa mbali bila kuamriwa kulipa gharama za kesi.

Besigye, Lutale na Kapteni Denis Oola wanatarajiwa kurejea mahakamani Agosti 18, 2026, mbele ya Jaji Emmanuel Baguma. Mahakama inatarajia pia kupokea ripoti ya kitabibu itakayoonyesha iwapo Besigye yuko katika hali inayomwezesha kusimama kesi.
 
Back
Top Bottom