Best Quote: "Hata ingekuwa JM ningemtosa"

Best Quote: "Hata ingekuwa JM ningemtosa"

Huyo mama nimemfuatilia kwa muda kidogo na mpaka sasa i can count on her lakini isije ikawa big talk and do nothing,time will tell!

You are very right Koba na wala hujakosea. Ninamfahamu vizuri sana huyu mama ni big talk kweli na ni 'opportunist'.
Kwa wanaomfahamu kabla ya kuwa na Charles Nyange hadi JM wanaelewa vizuri.
 
Tuelezeni basi huyu mama opportunism yake inakujaje, mimi mmama nimemmind siku mkadhaa hasa baada ya kutoka bungeni in protest wakati Zitto alivyosimamishwa ubunge, I liked that.

Halafu baada ya kutoa that Malecela comment Spika Sitta (Mzee Muhuni huyu) akamchombeza "angalia mama usije kukosa pa kulala usiku"
 
Mimi nadiriki kumtetea huyu Mama kwa kweli .Maneno aliyo yasema hatakaa atoke Mbunge yeyote wa kuchaguliwa wa CCM wa kuyasema haya .Amesema kwa hisia na amesema akiwa alianza siku nyingi kuutafuta ukweli .Hana chuki wala kitafuta cheo huyu naamini hili .
 
Tuelezeni basi huyu mama opportunism yake inakujaje, mimi mmama nimemmind siku mkadhaa hasa baada ya kutoka bungeni in protest wakati Zitto alivyosimamishwa ubunge, I liked that.

Halafu baada ya kutoa that Malecela comment Spika Sitta (Mzee Muhuni huyu) akamchombeza "angalia mama usije kukosa pa kulala usiku"

Six ni wivu tu unamsumbua babu huyu na speed na standard zake ambazo zinathibitisha kuwa yeye ndiye "mkurupukaji" katika mambo mengi. Hata leo alikuwa anafanya mambo kwa kuharakisha tu as if ametishwa na Mt Kenya mafia!

Mama Kilango so far alianza kujijenga zaidi kwenye issue ya zitto na kweli anajitahidi kiasi chake..... Hongera Mama Kilango!
 
1
. Ninamfahamu vizuri sana huyu mama ni big talk kweli na ni 'opportunist'.

Mkuu Pundamilia,

Nilikuwa nimeanza kukuheshimu sana hapa JF, mpaka nilipoiona hii post yako, what a shame! Wewe Mtanzania umeibiwa weee na kina Lowassa, mpaka umeme hakuna, jiji zima la Dar linanuka moshi kwa vi-generator ambavyo havijapimwa na chombo maalum cha serikali kuona kama polution yake ni hatari kwa wananchi au la, taifa limeibiwa mapesa kibao na hawa kina Lowassa, leo badala ya kudai kina Lowassa wapelekwe Jela, wewe unamtukana Mbunge aliyemshindilia Lowasssa misumari ya mwisho kwenye jeneza lake?

Nilifikiri utakuwa hapa kuongelea kwamba Lowassa, baada ya kuwakamatisha wabunge kule Manyara, just because alikuwa anamtaka mtu wake apite, angepaswa anyamaze kuhusu haki, maana yeye binafsi haijui haki, leo wewe unamtukana Mbunge ambaye taifa zima limekubali kuwa ni shujaaaa!

Pundamilia, maneno yako ni udaku na uzandiki, kwa sababu ukweli ni kwamba humjui huyo mama, amekuwa mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni, amekuwa senior accountant kuanzia Gulf Air mpaka Air Tanzania, Mbunge wa kuteuliwa na Rais baada ya kuonewa na Sumaye na Mmme mwenziwe Keeenja, kwenye ubunge wa Ubungo ambako ni clear kuwa mama alishinda, tena akiwa single maana then hakuwa mke wa Malecela, na ni mfanya Biashara mkubwa sana mwenye maduka kuanzia Dodoma, Dar, na Kihurio, wabunge wote hununua vitu vyao muhimu kwenye maduka yake huko Dodoma, ana nyumba zake binafsi toka Dodoma mpaka Dar, kutokana na biashara zake za nguo toka USA, na amekuwa hivi kabla hajaolewa na Malecela, leo unamwita opportunists exactly kwa misingi ipi mkuu?

Hivi wewe Pundamilia, shughuli aliyoifanya huyu mama jana bungeni wewe unaweza kuifanya? au tuambie umewahi kuifanya wapi huko duniani licha ya bongo? Hivi vijana haya maneno mnayarusha rusha mnaelewa maana yake au ndio ngumbaru? Unamwita opportunist kiongozi ambaye amekuwa akilala macho kuutafuta ukweli kuhusu Richmonduli, na amekuwa mwenyeji wa hapa JF kila siku kutafuta data, ambazo 1/3 alizozimwaga jana bungeni amezitoa hapa JF, maana tumekuwa tukim-forwardia kwa muda mrefu sasa, amezimwaga mbele ya Lowasssa, mwenyewe uso kwa uso, wewe unasema ni opportunist? Wallahi sisi weusi ni ngozi ya matako, yaaani mkuu huna hata haya umekalia keyboard kuchapa haya maneno ya choooni?

Kuacha Mwakyembe na huyu mama, nitajie kiongozi mwingine wa CCM, unayemjua asiyekuwa opportunist anayeweza kumtwanga Lowasssa, mbele ya uso wake? Spika mwenyewe alikuwa ameamua kukimbia huyo ungesema ni opportunist ningekuelewa mpuuuzi mkubwa wewe. Hivi unaelewa kuwa kuwekwa kwake wa kwanza huyu mama kwenye kuzungumza bungeni jana haikuwa bahati mbaya, ila Spika alishinikizwa na wabunge karibu wote kuwa mama apewe wa kwanza ili amalizie misumari ya jeneza la Lowasssa, unafikiri kati ya hao wabunge hakukuwa na wanaume?

2.
Kwa wanaomfahamu kabla ya kuwa na Charles Nyange hadi JM wanaelewa vizuri.

Mkuu unahitaji kushika adabu yako, maana inaonekana hukufunzwa na wazazi wako kuheshimu watu, mimi ninamfahamu huyu mama kabla hajaolewa na Malecela, na akiwa mke wa Nyange, ambaye alikuwa mmoja wa wakurugenzi kule kiwanda cha bia kwa sababu walikuwa ofisi moja na mshikaji wangu wa karibu sana Marehemu Guntram Itatiro, ambaye mkewe ni dada wa mmoja wa wafanyakazi wa ndani wa familia yangu ambaye amekuwa nasi for the last 20 years, nimewaona mara kwa mara kwenye sherehe mbali mbali, walifkia mahali yeye na Nyange, hawakuelewana wakapeana talaka, Nyange ameoa na mama ameolewa sasa naomba useme exactly ni sababu ipi inayomfanya yule Nyange awe safi na huyu mama awe mbaya?
Ninaomba useme ni bina-adam wangapi unaowajua, ambao kabla ya kuoa na kuolewa walikuwa malaika?

Mkuu Pundamilia, ninakuomba next time kabla hujamtukana kiongozi yoyote hakikihs akuwa una ukweli, uliyoyasema hapa ni uongo tena wa mchana kweupeee, Mama Anna Kilango, ni mfanya biashara mkubwa sana mkuu hata kabla hajaolewa na Malecela, na hajawahi kuwa opportunist maana angekuwa basi angeshakuwa waziri, kama walivyo kina Buriani, huyu kwa aliyoyafanya jana ni shujaaa wa taifa mkuu, kabla ya kikao cha bunge kuanza jana niliongea na wabunge wengi na yeye akiwa mmoja wapo, nikamkumbusha ile hard work ya kutafuta dataz hapa JF na akanihakikishia kuwa anaenda kumkoma nyani and she did, na leo asubuhi pia niliongea nae tena, mkuu Pundamilia, ukweli ni kwamba Lowassa alienda bungeni kutoa mallamiko ya kuonewa bila hata ya kuisoma ile ripoti nzima ya Mwakyembe, kwa hiyo wananchi wenye uchungu na taifa walimbonyeza mama mapema kuwa Lowassa hajaisoma, ndio mama alikuwa akimtwanga kwa kutumia barua zake Lowasssa, mwenyewe kwa sababu hakujua kuwa kwenye ile ripoti kuna barua zake mwenyewe kwa mawaziri akiwaagiza kuhusu mlo, na pia kumbuka kuwa ripoti iliyotolewa kwetu kuna yaliyobakizwa mkuu, maana viongozi wa kumainika kama huyu mama walipewa kakitabu toka last weeek,

Msiyoyajua ulizeni, badala ya kuja kurusha matusi hapa kama vile tuko kilabuni, mkuu hikli sio kilabu cha pombe, hii ni forum inayosomwa na wananchi dunia nzima, na kuna mashirika ya habari maarufu duniani yanachukua habari hapa, sasa kuwa muangalifu na unachosema kwanza mkuu.

Ahsante, na anytime nipo mkuu kwa maelezo zaidi.
 
ES Nakuamini una nyeti za mama, kama nilivyosema juu mama nimemmind tangu alivyoshupalia issue ya Zitto, ila nilishtushwa na hizi tuhuma za "opportunism". I am glad you set the record straight.
 
Teh heh ehee,
Lakini Mzee ES, hivi lakini ukijua mtu lazima umvue nguo zote?? Maana sometimes unaelezea info nyingi kuzidi hadi inaharibu counter argument yako.
 
Mkuu simvui mtu nguo, hizi ni zama za uwazi, hakuna siri kama hapo niliousema ni ukweli ambao unatakliwa uwekwe wazi, ninasema JF played a big role kwenye kutoa dataz za Richmonduli, the matter of fact hata picha ya kwanza kwa serikali ya ofisi ya Richmond kule Texas, ilianzia hapa JF, mkuu Mwakyembe ameshatufumbua sasa hakuna siri za kijinga ukweli usemwe wazi, kitendo cha kumtukana huyu mama yaaani siwezi nikaelewa wakati leo Tanzania nzima mama anasherehekewa na wananchi walio wengi.

Kama huu ukweli kuhusu huyu mama ninaoujua umekuuudhi I am not sorry mkuu, kwa sababu ninajua time na wakati wa kila kitu, lakini ni lazima niweke record straight kwamba kwanza ninamfahamu huyu mbunge kama ninavyowafahamu wabunge wengi kwa karibu, na kwamba hayo maneno ya kumtukana matusi ya nguoni ni pathetic!

Samahani kama nimekukwaza na huu ukweli wa kumjua huyu mama mbunge, against matusi aliyotukanwa, maana sioni kuwa yamekusumbua, lakini umesumbuliwa na ukweli wa kumjua mama! Ukweli ni kwamba ninafanya hivyo kumfahamisha mtukanaji kuwa ninamfahamu anayemtukana, na kwamba matusi yake sio kweli!

Ahsante Mkuu!
 
Anne Kilango kwa sasa,arguarbly,ndiye THE most likable na most POPULAR female politician in Tanzania.Sahau Migiro,Ana Makinda,Mongela,fisadi Zakia na bimkubwa Salma.Ukichanganya na ILE TIMU YA WAZALENDO WALIOAMUA LIWALO NA LIWE LAKINI MAMVI LAZIMA AONDOKE,basi hata ripoti ya EPA inaweza kabisa kuondoka na watu kadhaa.BRAVO Anne Kilango
 
Hapana mkuu,
Sidhani 'opportunist' ni tusi as such. Kuna quotations nyingi nimesoma siku chache zilizopita, nimekuna kichwa. Wewe umejibu na data vizuri, ku-counter fact kwamba sio 'opportunist'. Ila tu vitu vingine nimeona hukuhitaji kutaja. Ninachojaribu kusema ni kwamba, kama jamaa kachemsha, basi kwa jinsi ulivyojibu, na wewe kama umekwenda level sawa na yeye kwa jinsi ulivyomchambua huyo mama. Sijasema who is right or wrong. Ila nina uhakika unaweza kutoa pointi zako vizuri tu bila kum-over expose huyo mtu.
Nadhani ni rahisi zaidi, kumwacha anayesema huyo mtu ni 'opportunist', amwage data zake, halafu wewe ndo unajibu kwa kuvunja pointi by pointi. Sasa yeye kaongea sentensi mbili, wewe umetoa essay. You get my drift?
Anyways, kwa wengine tunaojifunza pointi zako nzuri sometime, kwenye hili huwa naona unachomoza kidogo. Just a well meant opinion, nothing personal.
Heshima.
 
Mkuu Nzoka,

Kwanza ninataka kuamini kuwa wewe sio Koba, Pundamilia, ameraise two important ishus ambazo zinagusa kwanza personal life ya kiongozi wa siasa, na amejaribu kuuua character ya a popular kiongozi of the time, inaonekana kuwa wewe na mimi tumesoma shule tofauti, wewe inaonekana umesoma English, na mimi nimesoma political sciense ikiwa ni pamoja na a lot of experience kwenye siasa za kweli,

Sikatai point yako ambayo kama mwenyewe unavyosema umeitoa kwa "nia njema", lakini tatizo ni kwamba kwenye siasa kuuua character ya kiongozi kama Pundamilia alivyofanya, sio lazima useme maneno mengi, hayo tu aliyoyasema Pundamilia yanatosha kuharibu jina la kiongozi wa siasa, Pundamilia amegusa sehemu mbili muhimu,

(1). Kwamba kiongozi ni opportunist, (2). Yeye anamjua binafsi Kiongozi kuwa ana tabia mbaya, kabla na hata baaada ya kuolewa ikiwa ni pamoja kumtaja mume wa zamani wa kiongozi.


Kwa mtizamo wako wa angle ya English school, mkuu anatakiwa kujibiwa kwa sentesi mbili au moja, ila kwa angle yangu ya siasa mkuu Pundamilia anatakiwa kueleweshwa (1). little history ya kiongozi, (2). kwamba hamjui, na tatu (3). kiongozi huyu hana hizo tabia alizozisema, (4). Kumsafisha mbele ya macho ya wananchi ambao wanaweza kumtizama kwa wasi wasi kutokana na maneno hayo ya Pundamilia, ambayo ni very damaging kwa mwananchi asiyemfahamu huyu mama vizuri.

Mkuu kwenye siasa, adui akikutupia mawe, ni lazima kwenye kumjibu umpelekeee mpaka nyumbani kwake, that is what I always do, kwa sababu ni lazima uelewe kuwa aliyeandika ana sababu, na hasa pale alipomtaja mume wa zamani wa mama, sasa kum-shut down lazima counter argument iwe strong with serious information kumuonyesha mtukanaji kuwa I know the person, ili kama kweli anazo damaging info zaidi lazima ziwe serious na strong, au aache kabisa ambayo ndio nia hasa ya kumjibu kwangu with details. huyu mkuu asingetaja mambo ya mume wa zamani nisingekwenda that deep,

again sina mpango wowote wa kuacha hiyo tabia pale atakapotukanwa kiongozi au mwananchi yoyote ninayemfahamu, mimi nilitegemea uwe outraged na matusi aliyotukanwa mama, lakini nashangaa kuwa umekuwa offended na majibu yangu ya kumtetea mama kiongozi kuliko matusi aliyotukanwa, anyways mkuu unajua hapa nia na madumuni ni kuelimishana, kuna ishu zinahitaji sentensi moja, kuna ishu mbili, na kuna ishus zinazohiatji essay, cha muhimu ni hoja, sio urefu wala ufupi wa maelezo au elimu, ila ni muhimu tunapoandika kuwa na ukweli, ushahidi, au dataz.

nia na madhumuni yangu ilikuwa kumuonyehsa mkuu Pundamilia, kuwa hamfahamu huyu mama Kiongozi, na kwamba huyu mama sio opportunist, na wala hana tabia mbaya kabla na baada ya kuolewa katika ndoa zake mbili, if I have to nitarudia tena kwa the same details, samahani sana mkuu kama unakwazika na style yangu ya uandishi, ila sina mpanfgo wowote wa kuibadili, especially at this time and age.

Ahsante Mkuu!
 
Waama hoja ni nzito na Mkuu FMES nashukuru kwa kuweka rekodi sawa. Hata mimi huchukia pale maneno ya uongo yanapowekwa kwa mtu (awe kiongozi au sio kiongozi). Kitu ambacho huyu mkuu pundamilia anahitaji kuelimishwa, ni kutofautisha kati ya opportunist na patriotic.

Kwa maoni yangu, Mama Kilango amefanya kitu ambacho viongozi wengi hawana ujasiri wa kukifanya. Kukemea uozo ndani ya chama chake kwa faida ya Taifa, kwangu mimi hiyo ni patriotism. Hakuwa na hulka ambayo mara nyingi hujitokeza katika nyakati kama hizi, hulka ya ku-politicize issues muhimu kama hizi.

Kudos to Mama K.
 
Hongera sana Mama Anne Kilango Malecela, yaani tunataka Majasiri wengine kutoka CCM pale Bungeni kama wewe. Wewe fikiria mle Bungeni kuna mijitu ni mi-Professor, mingine mi-Doctor(PhDs na MDs) lakini bado iko imezubaa tu kama mapimbi na kukalisha mipumbu yao kama Mabwabwa wa Lamu(excuse my french), yaani Mijitu na Elimu zao inapelekeshwa kama Watoto wadogo kisa eti kukilinda Chama, nyaambaaaaaf kabisa. Yaani nilikuwa na hasira sana kuhusiana na Sakata la huyu Jambazi Lowassa lakini baada ya kusoma alichosema huyu Mama nimepata furaha kidogo kujua kwamba kuna baadhi ya viongozi pale Bongo nao wamechoshwa na huu ushenzi unaofanywa na Mijambazi iliyo ndani ya CCM.
 
nia na madhumuni yangu ilikuwa kumuonyehsa mkuu Pundamilia, kuwa hamfahamu huyu mama Kiongozi, na kwamba huyu mama sio opportunist, na wala hana tabia mbaya kabla na baada ya kuolewa katika ndoa zake mbili, if I have to nitarudia tena kwa the same details, samahani sana mkuu kama unakwazika na style yangu ya uandishi, ila sina mpanfgo wowote wa kuibadili, especially at this time and age.

Ahsante Mkuu!

Mheshimiwa naona kweli umesimama upande wa haki, i can see that you have tried to use your political experience to counter the attempt of assasination of this character. Kweli hata kwa maoni yangu sioni kama ni jambo zuri.
Lakini kwa kifupi ni kuwa, in politics which is a dirty game, mtu kuwa opportunist kwa malengo ya kisiasa sio mbaya, mbona kuna vyama opportunist, na hata watu wengi ni maopportunist tu kwenye mambo ya kisiasa, this is how people play the game.
Lakini ni vizuri sana kuwa you have come on defence of innoncent character!
 
Field Marshall ES,
humfahamu mama kilango. ungekuwa unamfahamu usingemtetea hapa. wazee wa kipare tayari wameapa huyu mama ubunge ni miaka 5 tu. mama kilango amewatukana matusi makubwa wazee wa kihurio-jitengeni kutokana na kisasi chake kisichokwisha kwa mzazi mwenzake.

serekali iliamua kutoa fedha kujenga sekondari 2 kihurio-uzambara na kihurio-jitengeni. lakini kwa ubinafsi alionao mama kilango akaamua sekondari ijengwe kihurio-uzambara alikozaliwa yeye.

katika mkutano wa hadhara mama kilango akawaambia wananchi wa kihurio-jitengeni wakiwemo wazee kwamba hataki kusikia habari ya ujenzi wa sekondari jitengeni. mama kilango akasema anayetaka kuongelea suala hilo akazungumzie chumbani na mkewe!!!

wazee na wananchi wa kihurio-jitengeni wakaamua kujenga sekondari kwa nguvu zao wenyewe bila msaada wa serikali na mbunge wao. sekondari ya jitengeni imejengwa wakati sekondari ya mama kilango inasuasua.

wazee wameamua wembe ulomnyoa ndhira 'daniel yona' ndiyo huohuo utakaomnyoa anna kione kilango. hawataki tena kumsikia huyu mama. kama kuna anayempigia debe basi ampe ubunge wa taifa, lakini same mashariki hapati tena.

tayari mabalozi wawili na katibu mkuu mstaafu wameombwa kuchukua fomu za ubunge mwaka 2010.
 
Mzee ES Kudos sana mkuu
bungusile wewe ndiye hasa humjui huyu mama na kama una underground propaganda pole.

Unasema ana kisasi na mtalaka wake thats human, kwa matendo aliyokuwa akifanyiwa wakati yuko na nyange (watu wa block 41 wanajua) lazima hata kama ni wewe ungekuwa na hasira.
Mama ni jasiri kwani hata baada ya kuachana na nyange na nyange kuoa tena but she stod on her own two feet na kuanza biasha ra taratibu pale pale kwake block 41 akishona nguo za maharusi na kupamba na baadae kuimport fro US. Slowly as single akaingia UWT na later own kugombea na keenja jimbo la ubungo (which we all know she won lakini walimchezea faulo kubwa sana )
But still she never gave up akaendelea na leo ni mbunge wa jimbo. Huyu hata kigodo huwezi kumfananisha na wale mama zetu ambao ila siki wanataka viti maalumu, kwenda jimboni nah.
Bangu, sipendi kuchangia sana siasa ila kwa hili my fingers just cant stop, kwa sababu huyu mama aliwahi kuwa very close neighbor na sote tunamjua alivyo strugle.
Unasema amepeleka sekondari moja kijijini kwake? sasa hapo tatizo ni nini? kama serikali imetenga pesa kwa sekondari mbili na moja kajenga kijijini kwake, mbona safi tu? mi nilidhani utasema zote kajenga kijijini kwake? au alikula hela?
My brother some times jipange uje na full data.
nani kati ya wale rubberstapms(wabuge wengine waoga wa CCM) wangekuwa na uthubutu wa kuongea kama yule mama? just tell me lod and clear nani?
The fact remains the same she made a huge move na comments zake zenye ukweli, ambazo zinamlenga mnyonge, lets wait and see the next election she wont loose as you vow cause we wana wa wanyonge know what she is.
 
in politics which is a dirty game, mtu kuwa opportunist kwa malengo ya kisiasa sio mbaya, mbona kuna vyama opportunist,

Mkuu ninakuelewa, kama point ya Pundamilia, ilikuwa ni hiyo yaaani oppportunist wa kisasa, basi asngetaja ndoa na waume wa mama, alipowataja hao ilikuwa ni personal sio siasa, tena.

Mkuu Bangusule,

Kama sio huyu mama soko lililotakiwa kujengwa kule Magharibi, lisingejengwa Mashariki, na ku-cost Mathayo uwaziri wa mlo, Barabara iliyofungulkiwa majuzi na rais isingejengwa kule Kihurio, contena zima la vitabu limepelekwa huko toka UK, hayo maneno ni yako wewe na mchango wako wa kwanza hapa JF, mama sio tu atashinda tena bali ataendelea tu huko maana kwa aliyoyafanya juzi bungeni yanatosha kumpa ubunge kuanzia wa CCM mpaka upinanzi na popote pale bongo, ni wananchi kama wewe tu ndio anaweza kumnyima kura, lakini sio jimbo zima na rekodi za huko zinafahamika mkuu acha blah1 blah tutaziweka hapa, toka awe mbunge rais ameshaenda karibu mara kumi huko mkuuu unafikiri ni kwa nini? Majuzi umesikia huyu mama anataka maelezo kuhusu deal ya Bandari Kati ya Mkapa na Karamagi, next itakuwa Kiwira na Mkapa, mkuu wewe fasten your belt mama anakuja kama kifaru, na JF tuko nyuma yake mkuu!

Ahsante Mkuu
 
wazee wameamua wembe ulomnyoa ndhira 'daniel yona' ndiyo huohuo utakaomnyoa anna kione kilango. hawataki tena kumsikia huyu mama. kama kuna anayempigia debe basi ampe ubunge wa taifa, lakini same mashariki hapati tena.

tayari mabalozi wawili na katibu mkuu mstaafu wameombwa kuchukua fomu za ubunge mwaka 2010.

Mkuu Bangusile, ha samahani "bangusule"

Baadhi tuko tayari kwenda huko milimani kuhakikisha mama huyu anarudi bungeni. Hiyo kazi tunaweza kuifanya bure hata bila kulipwa senti tano.

Hao makatibu na mabalozi unaowataka wagombee siyo vibaya wakagombea udiwani ili waweze kusaidiana na mama huyo. Sioni yeyote mwenye uwezo wa kukaa bungeni akaongelea masilahi ya nchi kama mama huyu alichofanya bungeni.

Tunahitaji watu wengi wakusaidia na akina Dr. Slaa, Zitto na wengineo siyo wa kwenda kulala na kutaka sifa nyingi eti nilikuwa Katibu/sijui balozi na kuwasifia MAFISADI ili wapate mgao kutoka kwao.

Hila kama wamekwambia wewe au kama wewe ulikuwa katibu/Balozi na unataka kugombea gombea tu(haki yako ya kikatiba) ila utashindwa kwa kishindo tu.

Lazima mwaka huuu huyu mama MAFISADI watamkoma tu wakae mkao wa kupigwa makombola.
 
Back
Top Bottom