1
Mkuu Pundamilia,
Nilikuwa nimeanza kukuheshimu sana hapa JF, mpaka nilipoiona hii post yako, what a shame! Wewe Mtanzania umeibiwa weee na kina Lowassa, mpaka umeme hakuna, jiji zima la Dar linanuka moshi kwa vi-generator ambavyo havijapimwa na chombo maalum cha serikali kuona kama polution yake ni hatari kwa wananchi au la, taifa limeibiwa mapesa kibao na hawa kina Lowassa, leo badala ya kudai kina Lowassa wapelekwe Jela, wewe unamtukana Mbunge aliyemshindilia Lowasssa misumari ya mwisho kwenye jeneza lake?
Nilifikiri utakuwa hapa kuongelea kwamba Lowassa, baada ya kuwakamatisha wabunge kule Manyara, just because alikuwa anamtaka mtu wake apite, angepaswa anyamaze kuhusu haki, maana yeye binafsi haijui haki, leo wewe unamtukana Mbunge ambaye taifa zima limekubali kuwa ni shujaaaa!
Pundamilia, maneno yako ni udaku na uzandiki, kwa sababu ukweli ni kwamba humjui huyo mama, amekuwa mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni, amekuwa senior accountant kuanzia Gulf Air mpaka Air Tanzania, Mbunge wa kuteuliwa na Rais baada ya kuonewa na Sumaye na Mmme mwenziwe Keeenja, kwenye ubunge wa Ubungo ambako ni clear kuwa mama alishinda, tena akiwa single maana then hakuwa mke wa Malecela, na ni mfanya Biashara mkubwa sana mwenye maduka kuanzia Dodoma, Dar, na Kihurio, wabunge wote hununua vitu vyao muhimu kwenye maduka yake huko Dodoma, ana nyumba zake binafsi toka Dodoma mpaka Dar, kutokana na biashara zake za nguo toka USA, na amekuwa hivi kabla hajaolewa na Malecela, leo unamwita opportunists exactly kwa misingi ipi mkuu?
Hivi wewe Pundamilia, shughuli aliyoifanya huyu mama jana bungeni wewe unaweza kuifanya? au tuambie umewahi kuifanya wapi huko duniani licha ya bongo? Hivi vijana haya maneno mnayarusha rusha mnaelewa maana yake au ndio ngumbaru? Unamwita opportunist kiongozi ambaye amekuwa akilala macho kuutafuta ukweli kuhusu Richmonduli, na amekuwa mwenyeji wa hapa JF kila siku kutafuta data, ambazo 1/3 alizozimwaga jana bungeni amezitoa hapa JF, maana tumekuwa tukim-forwardia kwa muda mrefu sasa, amezimwaga mbele ya Lowasssa, mwenyewe uso kwa uso, wewe unasema ni opportunist? Wallahi sisi weusi ni ngozi ya matako, yaaani mkuu huna hata haya umekalia keyboard kuchapa haya maneno ya choooni?
Kuacha Mwakyembe na huyu mama, nitajie kiongozi mwingine wa CCM, unayemjua asiyekuwa opportunist anayeweza kumtwanga Lowasssa, mbele ya uso wake? Spika mwenyewe alikuwa ameamua kukimbia huyo ungesema ni opportunist ningekuelewa mpuuuzi mkubwa wewe. Hivi unaelewa kuwa kuwekwa kwake wa kwanza huyu mama kwenye kuzungumza bungeni jana haikuwa bahati mbaya, ila Spika alishinikizwa na wabunge karibu wote kuwa mama apewe wa kwanza ili amalizie misumari ya jeneza la Lowasssa, unafikiri kati ya hao wabunge hakukuwa na wanaume?
2.
Mkuu unahitaji kushika adabu yako, maana inaonekana hukufunzwa na wazazi wako kuheshimu watu, mimi ninamfahamu huyu mama kabla hajaolewa na Malecela, na akiwa mke wa Nyange, ambaye alikuwa mmoja wa wakurugenzi kule kiwanda cha bia kwa sababu walikuwa ofisi moja na mshikaji wangu wa karibu sana Marehemu Guntram Itatiro, ambaye mkewe ni dada wa mmoja wa wafanyakazi wa ndani wa familia yangu ambaye amekuwa nasi for the last 20 years, nimewaona mara kwa mara kwenye sherehe mbali mbali, walifkia mahali yeye na Nyange, hawakuelewana wakapeana talaka, Nyange ameoa na mama ameolewa sasa naomba useme exactly ni sababu ipi inayomfanya yule Nyange awe safi na huyu mama awe mbaya?
Ninaomba useme ni bina-adam wangapi unaowajua, ambao kabla ya kuoa na kuolewa walikuwa malaika?
Mkuu Pundamilia, ninakuomba next time kabla hujamtukana kiongozi yoyote hakikihs akuwa una ukweli, uliyoyasema hapa ni uongo tena wa mchana kweupeee, Mama Anna Kilango, ni mfanya biashara mkubwa sana mkuu hata kabla hajaolewa na Malecela, na hajawahi kuwa opportunist maana angekuwa basi angeshakuwa waziri, kama walivyo kina Buriani, huyu kwa aliyoyafanya jana ni shujaaa wa taifa mkuu, kabla ya kikao cha bunge kuanza jana niliongea na wabunge wengi na yeye akiwa mmoja wapo, nikamkumbusha ile hard work ya kutafuta dataz hapa JF na akanihakikishia kuwa anaenda kumkoma nyani and she did, na leo asubuhi pia niliongea nae tena, mkuu Pundamilia, ukweli ni kwamba Lowassa alienda bungeni kutoa mallamiko ya kuonewa bila hata ya kuisoma ile ripoti nzima ya Mwakyembe, kwa hiyo wananchi wenye uchungu na taifa walimbonyeza mama mapema kuwa Lowassa hajaisoma, ndio mama alikuwa akimtwanga kwa kutumia barua zake Lowasssa, mwenyewe kwa sababu hakujua kuwa kwenye ile ripoti kuna barua zake mwenyewe kwa mawaziri akiwaagiza kuhusu mlo, na pia kumbuka kuwa ripoti iliyotolewa kwetu kuna yaliyobakizwa mkuu, maana viongozi wa kumainika kama huyu mama walipewa kakitabu toka last weeek,
Msiyoyajua ulizeni, badala ya kuja kurusha matusi hapa kama vile tuko kilabuni, mkuu hikli sio kilabu cha pombe, hii ni forum inayosomwa na wananchi dunia nzima, na kuna mashirika ya habari maarufu duniani yanachukua habari hapa, sasa kuwa muangalifu na unachosema kwanza mkuu.
Ahsante, na anytime nipo mkuu kwa maelezo zaidi.