Better late than never, CHADEMA anzisheni YouTube Online TV haraka iwezekanavyo


Milioni 300 na zaidi wameshindwa hata kununua vikamera vya kujirekodi basi ujuwe wana matatizo, kwa hiyo wanazidiwa na Milad ayo pesa au ni upuuzi wao?
Milad ayo anafanya biashara hahitaji migogoro isiyokuwa na tija sababu mtaji katafuta mwenyewe, hivyo chadema lazima wajiongeze.
Unaenda kuchukua taarifa kwa mtu yeye kila kitu anazungumzia mtu mmoja tu, kila siku, lazima aachwe aongee mwenyewe.
 
Nimeona hayo hata mimi na naunga hoja kabisa.
 

Wacha1 mbona ulikuwa unaipondaga sana CCM nini kilitokea?!
 
Sijui kwanini huu ushauri CHADEMA huwa hawaufanyii kazi.Ni miaka nenda rudi wanashauriwa Hii kitu hawafanyi sijui kwanini.Inabidi pia wawe na wandishi wao wapiga picha wao ambao watachukua matukio yote.
 

Wewe una mapungufu ktk ufahamu tu. Huwezi kutafsiri kitu ktk mantiki yake kusuduwa.....

Mfano; mgombea yeyote anayewania kumtoa mgombea anayetetea kiti chake hawezi kufanya kampeni zake bila kutaja madhaifu, makosa ya KISERA, MIPANGO na MAUMUZI ya utawala unaotakiwa kufurushwa....

Katika mazingira ya uchaguzi huu, hata kutaja na kuusema udhaifu binafsi wa mgombea wa CCM Bwana Magufuli kwa kweli ni ruksa kabisa. Na katika eneo hili Magufuli ataipata fresha maana ana nadhaifu lukuki yanayom disqualify kuwa kiongozi bora...

Katika video hii, Tundu yuko very clear kabda kwa wasitaka kuelewa kwa sababu zao binafsi....

Kaongelea UONGO na ULAGHAI aki connect na manunuzi ya Ndege, Mabwawa ya umeme na taabu za wakulima...

Ameongelea mahusiano ya kimataifa nini atafanya na nini kinafanywa na utawala wa sasa wa CCM ya Magufuli..

Mwisho kamalizia na nichagueni Mimi tuondoe tabia ya kudanganyana na kulaghaiana na kudhalilishana....

Wewe unataka atoe ahadi siyo? Kuwa mkinichagua nitatoa milioni 50 kila kijiji mkagawane? Nichagueni nijenge barabara? Niwajengee shule, hospitali nk no, au siyo?
 
Swadaktaaaa! Ushauri kuntu huu.
 
Kumbe na wewe unamkubali Lissu?? Tangu lini?
 
Nafuatilia mkuu...

Yupo kwenye orodha ya watakaopata kura yangu mwaka huu.

Udiwani CCM
Ubunge Chadema
Urais CCM.
Mimi naona kabisa kura zangu mwaka huu inaenda kwa mkuu wa nchi tu. Sababu kubwa ni kuwa mkiwa na kiongozi wa upinzani hata maendeleo mnacheleweshewa. Jimbo nililopo Mnyika alibanwa mbavu balaa, actually hata kupitapita alishindwa. Kibamba mostly watu wanaona bora kuirudisha CCM tu ili maisha yaende, tuna changamoto kubwa ya miundombinu as hii bado ni wilaya mpya.
 
Huyu millard ayo atafute nchi ya kwenda kuanzia November mwaka huu maana huyu mtoto kazidi. Havumiliki tena
Haaaaaaa mwacheni jamani... fikiria azam,TV na ITV's wameshindwa kutangaza sembuse kaayo
 
Kweli kabisa.. tabia ya jiwe kusema watu vibaya hadharani siyo nzuri, ni ya kupuuzwa
 
Waoongee na Maria Sarungi maana tayari ana online TV japo imefungiwa kwa sasa. Wakodi vifaa wabadili jina, wajisajili chap.
Mkuu, wataruhusiwa KUSAJILIWA? Kumbuka walikuwa na gazetj TANZANIA DAIMA, kuelekea uchaguzi huu, Serikali ikalifuta, bila sababu ya msingi. Sasa, sidhani kama wanaweza kuruhusu kupatikana mdomo mwingine wa washindani wao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…