Better late than never, CHADEMA anzisheni YouTube Online TV haraka iwezekanavyo

Better late than never, CHADEMA anzisheni YouTube Online TV haraka iwezekanavyo

Kusema ukweli tokea Lissu arudi,anzia mkutano wa kamati kuu na mkutano mkuu. Nilifuatilia matangazo Mwananchi digital Kila Lissu akiongea wakiona anaelekea kumsema Magufuli wanaanza kupungunza sauti na mwisho wanafinyia sauti ndani kabisa.

Leo sasa kituko nilikuwa naangalia Millard Ayo yaani habari ya Lissu sauti haisikiki kabisa na mwisho wakastop kabisa kuonyesha.

Ila Millard Ayo hiyo hiyo walionyesha Uchaguzi UVCCM sauti ilikuwa fresh tu.

Jamani eeeeh mwenye macho haambiwi tazama.

Chadema anzisheni YouTube channels nunueni vifaa kama hamna hela semeni tuwachangie. Na muajiri watu kwa kazi hiyo.

Kitengo cha mawasiliano CHADEMA amkeni huu muda wa mapambano acheni kulalamika wale kina Milard Ayo wanaogopa .

Hata mkianzisha You tube channel lazima mfate sheria na taratibu na pia lazima mpewe leseni na lazima mzingatie miiko ya uandishi wa habari ...mkiruhusu matusi na uchochezi sheria ziko wazi mtapigwa pin kama kawa !

Anzisheni lakini lazima mjue kuwa sheria ziko wazi hakuna mtu wa kirisk chombo chake kisa mropokaji
 
..well, ulisikia Jpm na wapiga debe wake walivyokuwa wakitaja majina wakati wa kampeni?

..Jpm alifikia mpaka kudai ndugu yake Lowassa amepeleka kesi mahakamani na kuzuia bomba la maji kutoka ruvu lisipite.

..pia upo mkutano wa kampeni wa Jpm ambapo Lowassa alitukanwa kwamba amejisadia haja kubwa jukwaani.

..na huko tunakoelekea sina uhakika kama Jpm atafanya kampeni bila kuwatukana au kuwakashifu wapinzani, ila tujue kwamba ni mtu ambaye ana rekodi ya kufanya kampeni chafu na matusi.

..lingine tunalopaswa kujiuliza ni kama Jpm ataweza kuhimili na kuvumilia kashfa na matusi yatakayoelezwa kwake.
Na ndiyo maana sikumtaja mtu mkuu najua hili linafanyika kwa vyama vyote.

Mwisho wa siku hakuna hoja zinazojengwa kwenye kampeni zaidi ya kuzigeuza kuwa viwanja vya mipasho.

Ni vigumu kutomsema mpinzani wako ila inapokuwa hotuba nzima umeitumia kwa personal attacks matatizo yetu wananchi hayatajadiliwa kamwe.
 
..I totally agree with you.

..idara ya habari na PR ya CDM imedumaa sana.

..hata matukio wanayorusha wanafanya hovyo-hovyo tu.

..Inawezekana hii kazi inafanywa na watu ambao wana majukumu mengine, na hili la kupasha habari wananchi ni ziada.
Plus hizo media zinaweza kuiniza pesa kwenye matangazo ya biashara baada ya kampeni, zinakuwa chanzo cha mapato kwa ajili ya kampeni zijazo na kukuza chama.
Gari zile hazizalishi kihivyo baada ya kampeni ila zitakuwa zinakula pesa za ukarabati tu huku zikiendelea kuchakaa.
Walitakiwa wanunue gari kiasi na pesa nyingine iende kwenye bajeti ya media huko kwenye PR.
 
Na ndiyo maana sikumtaja mtu mkuu najua hili linafanyika kwa vyama vyote.

Mwisho wa siku hakuna hoja zinazojengwa kwenye kampeni zaidi ya kuzigeuza kuwa viwanja vya mipasho.

Ni vigumu kutomsema mpinzani wako ila inapokuwa hotuba nzima umeitumia kwa personal attacks matatizo yetu wananchi hayatajadiliwa kamwe.
.....
Chama chake ni CCM. Yeye mwenyewe kasema CCM ni nyumbani. Atakisemaje CCM vibaya? Mimi nimesma nchi. Nitajie nchi (km Afrika Kusini - Malema, Uingereza - Labour Party, USA - Biden, Uganda - Boby Wine nk) ambako wanafanya kampeni bila kutaja Rais ama chama kilichoko madarakani. Tumia akili - huwezi kufanya kampeni bila kumtaja mpinzani wako na chama chake. Usipendekeze mambo yasiwezekana.
 
Wanatakiwa na nani au na nini kuwa neutral?

CNN ya Marekani, kwa mfano, ipo neutral?
Demokrasia huambatana na fair access to the media kwa vyama vyote vya siasa.

Nchi kama Tanzania ina media ya taifa ambayo inaendeshwa kwa kodi za wananchi. Je, haitakiwi kuwa neutral ama kutoa fair coverage kwa vyama vyote?!
 
Lissu Ana ilani yake binafsi kwenye kichwa. Na anaamini yeye ni bora na anajua kuliko chadema wote, hakuna anayeweza kumshauri, anatakiwa aeleze sera na aache personal attack. Usitegemee TV ya taifa irushe maneno ya jazba na uchochezi.
Wala lisu hayuko hivyo. Na kama ulimskoa alisema yeye anatama kumuondoa magufuli madarakan sijamsiki akisema wewe fulan mpumbavu, au wewe fulan nitakuchakaza aama wewe mama fulan panua panua panua hadi wapi.

Alisema wazi anataka akishinda atangazwe kuwa kashinda na hata kubali kuonewa je hilo nalo.ni.neno baya?
 
Kazi kupost ela zetu za ruzuku zimenunua Magari [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yan chadema mnafuraisha sana
Pesa za ruzuku wangewapa Wananchi maana magari si ni vitu, na wao hawataki maendeleo ya vitu.
 
Ipo chadema media TV

Sasa mbona haiko active kurusha matokeo? Hii kutegemea TV za wengine ndio nini wakati wanajua hali iliyopo sio? Kipindi hiki wahakikishe kuwa wanapata coverage kubwa mitandaoni, ndio silaha kubwa kwao.
 
Hata mkianzisha You tube channel lazima mfate sheria na taratibu na pia lazima mpewe leseni na lazima mzingatie miiko ya uandishi wa habari ...mkiruhusu matusi na uchochezi sheria ziko wazi mtapigwa pin kama kawa !

Anzisheni lakini lazima mjue kuwa sheria ziko wazi hakuna mtu wa kirisk chombo chake kisa mropokaji
Wanaweza kumuomba mtu anayeishi nje ya nchi kufungua youtube channel. Kisha watu wakawa wanashare link na video. Eg labda iite kampeni 2020. Wakitaka kuruka live huyo mtu aliye nje anaweza kuwapa credentials, au rtmp key, au stream key au restream account wakatumia kiulainiiiiii tu maana sheria haijazungumzia jinsi ya kuzuia youtube channel toka nje ya nchi. Pia sheria haijazungumza lolote juu ya rtmp.
 
Demokrasia huambatana na fair access to the media kwa vyama vyote vya siasa.

Nchi kama Tanzania ina media ya taifa ambayo inaendeshwa kwa kodi za wananchi. Je, haitakiwi kuwa neutral ama kutoa fair coverage kwa vyama vyote?!
Ni kweli.

Sizijui vizuri sheria zetu za vyombo vya habari hususan kuhusu coverage za vyama vya kisiasa.

Kama hakuna, basi kunapaswa kuwepo na ‘equal time rule’ kwa wagombea wote wa vyama.
 
Ushauri mzuri sana, hili ni jambo la msingi sana kuelekea kwenye mapambano ya kudai uhuru.
Kusema ukweli tokea Lissu arudi, anzia Mkutano wa Kamati Kuu na Mkutano Mkuu. Nilifuatilia matangazo Mwananchi digital Kila Lissu akiongea wakiona anaelekea kumsema Magufuli wanaanza kupungunza sauti na mwisho wanafinyia sauti ndani kabisa.

Leo sasa kituko nilikuwa naangalia Millard Ayo yaani habari ya Lissu sauti haisikiki kabisa na mwisho wakastop kabisa kuonyesha.

Ila Millard Ayo hiyo hiyo walionyesha Uchaguzi UVCCM sauti ilikuwa fresh tu.

Jamani eeeeh mwenye macho haambiwi tazama.

CHADEMA anzisheni YouTube Channels nunueni vifaa kama hamna hela semeni tuwachangie. Na muajiri watu kwa kazi hiyo.

Kitengo cha mawasiliano CHADEMA amkeni huu muda wa mapambano acheni kulalamika wale kina Milard Ayo wanaogopa .
 
Naam!

Wanachomfanyia Lissu si sawa kabisa.

Sheria ya vyombo vya habari iko wazi mtu akitukana au akavunja sheria wewe ndio utawajibika! Shida ya Lissu atabiriki ndio maana vyombo vya habari vina jikinga ! Mbowe akiongea wanajua fika hakuna shida na hakuna tatizo lolote anaweza wasababishia
 
Huyu millard ayo atafute nchi ya kwenda kuanzia November mwaka huu maana huyu mtoto kazidi. Havumiliki tena
Mnalia kuna udikteta, ona nyie ambao mko ndotoni kama watawala tayari mmeshaanza kutimua watu huko huko ndotoni. Bora usingizi uishe maisha yaendelee.
 
Huo ni ushauri wako
Pia CHAUMA, ACT , DEMOKRASIA MAKINI na CUF wasisahau ushauri huu.

Ila siasa za kuanza kutaja mtu au watu mwanzo mwisho sio nzuri. Uza sera unaenda kutufanyia nini. Au wewe shida yako kujifanya unajua kuyafanya vizuri anayoyafanya unaemtaja?

Yapo mengi ya kusema kwenye kampeni zaidi ya kuanza kutukana na kuwataja watu.
 
Demokrasia huambatana na fair access to the media kwa vyama vyote vya siasa.

Nchi kama Tanzania ina media ya taifa ambayo inaendeshwa kwa kodi za wananchi. Je, haitakiwi kuwa neutral ama kutoa fair coverage kwa vyama vyote?!
Hata chombo cha umma kina taratibu na sheria zinazokiendesha,
Mfano bunge si la chama chochote ukiongea maneno yasiyokubaliana na sheria za huko unaambiwa toa hilo neno.

Kwa sababu lissu hatabiriki ataongea nini, ukiweka live utarrusha mambo mengine sio, so wanaona bora kumrecord kisha wataedit.
 
Back
Top Bottom