Betty Mkwasa: Fani ya Uandishi wa Habari ipo ICU kwa sasa na Nasikitika Wahusika tumenyamaza tu, huku ikienda Kufa kabisa

Betty Mkwasa: Fani ya Uandishi wa Habari ipo ICU kwa sasa na Nasikitika Wahusika tumenyamaza tu, huku ikienda Kufa kabisa

Mtalaumu waandishi mtalaumu madaktari na Kila aina ya kada shida ni uwekezaji mdogo katika mfumo wa elimu
Je Betty na nguli wenzake waliongea chochote kuhusu mfumo wa elimu pale ambapo mwl mmoja mwenye njaa alifundisha watoto 1000 wenye njaa!?(Akiwa mkuu wa wilaya)
Je alihimiza upatikanaji wa walimu wa kutosha!?
Maabara za lugha na science
Viwanja vizuri vya michezo kukuza haiba za watoto n.k
Kifupi ni kuwa ukitaka kuharibu jamii haribu mfumo wa elimu na kwa hapa tulipo italaumiwa Kila kada huku wakitakiwa watoe kitu hawana
 
Wee Genta, huyu mama si alikua mkuu wa mkoa juzi juzi hapa? Au nimechanganyaa files? Dooooh
Umeniangusha sana kwani nilikuwa nakukubali mno kama Mtu ambaye upo very up to date kwa Information. Nimesikitika.
 
Betty yuko sahihi kabisa,fani ya waandishi wa habari wakati huu inawatu wasiojua taaluma yao......FM RADIO'S ziko choka mbaya,hata mtu akionekana ni comedian tu,basi anapewa Mic, maneno yasiyo na staha yanasikika hewani bila shida,makelelee studio hata night club kuna nafuu.Television mambo ya hovyo yanaonyeshwa bila shida wala uoga,aaah yaani tasnia imekufa kabisa.Printing media huko nako magazeti huwezi kununua,ukakuta critical analysis ya jambo likiwa limenyooka,siku hizi ni praise team tu.

Kiufupi Media inachangia serikali legelege,mmomonyoko wa maadili,siyo 4th pillar of the government tena...... INASIKITISHA
 
Tatizo waandishi wenyewe wa habari wajinga

Fani zote mtu.kutambuliwa mfano mwanasheria, Engineering, mfamasia ,Daktari nk lazima mtu awe na digrii ya fani husika na husajiliwa na bodi inayosimamia weledi nk

Mswada uliandaliwa kuwa kuwe na bodi ya waandishi wa habari na wasajiliwe na kiwango cha kusajiliwa lazima awe na digrii kwenye fani ya uandishi wa habari wakapinga ohh hiyo ni kinyume cha katiba kuminya uhuru wa habari.Serikali ikazira kuwa basi nendeni mtakavyo

Sasa matokeo ndio hayo akina Mwijqku form four failures wanaoponda elimu iwe commerce nk ndio watangazaji nguli

Wachekeshaji wafanya vituko nk

Ndio maana uandishi wa habari sasa hivi ni kituko
 
Mkuu chakula kinatolewa kulingana na aina ya walaji , watangazaji hawa inatoa picha ya aina ya wasikilizaji iliyopo kwa wingi.
kuna classmates zangu wawili ni watangazaji wakubwa tu ila kwa nilivyowajua nimeshangaa wamepataje nafasi hiyo na kuwa maarufu kiasi hicho.
You have got a point....
WaTz hatupo serious, kama vile akili ya kuwa serious haipo kwq vichwa vyetu. Hatuwezi kuachanisha entertainment, crap, serious issues.
Tupo kama Jokers tu..clowns of some sort.

Mpaka pale tutakapoacha kuwa ndezi ndipo mambobyataanza kuwa serious.
Hata viongozi tunapata vichekesho tu chini mpaka juu. Wale wenyenupeo kidogo wanatuangalia wanatuona kama puppets
 
"Siku hizi Mtu akiwa tu ni Maarufu, Mchekeshaji, Msanii au Mbwabwaji Mitandaoni basi haraka sana anakuwa Mtangazi wa Redio na Tv. Naumia sana kuona hii Fani yenye Heshima kubwa duniani kote sasa hapa Tanzania ikiwa ipo ICU na Siku si nyingi inaenda Kufa kabisa. Sikatai ujio wa Teknolojia kwani hilo ni Jambo jema ila pamoja na Teknolojia lakini ile Misingi Mama ya Utangazaji / Uandishi wa Habari haijabadilika na wala haitokuja Kubadilika. Na kinachonisikitisha zaidi Sisi ambao ndiyo Wahusika tumenyamaza na wala hatuhoji hivyo kuendelea tu kuruhusu Upuuzi na Ukiukwaji mkubwa wa Kimaadili kuendelea kuwepo", amesema Mtangazaji Mkongwe, Mshindi wa Kike wa Afrika wa Tuzo ya Uandishi wa Habari za Ukimwi na Mweledi wa Tasnia Elizabeth ( Betty ) Mkwasa alipokuwa akizungumza na TBC1 katika Miaka 73 ya Utangazaji Tanzania.

GENTAMYCINE kila mara nimekuwa nikiisema hapa JamiiForums hii Tasnia ya Habari na Utangazaji halafu naonekana kama vile nina Nongwa nayo au nina Agenda nayo / nao Binafsi na wapo hadi Wanaonishutumu haya sasa leo kasema Mhusika mwenyewe hebu mbishieni basi na Yeye au Mshutumuni kama mfanyavyo Kwangu.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE a.k.a Akili Kubwa na Tajiri wa Maono hakuna ambacho nakisema JF huwa hakiji Kutokea Ok?
Wanaoua tasnia ni Wana habari wenyewe
 
Wanachojua ku ripoti tu habari za wanasiasa, kutoa taarifa za raisi au waziri kasema hivi au vile kaamka kalala.Yaani hawana mpango wa kwenda kutafuta habari na kuibua kero za watu
 
"Siku hizi Mtu akiwa tu ni Maarufu, Mchekeshaji, Msanii au Mbwabwaji Mitandaoni basi haraka sana anakuwa Mtangazi wa Redio na Tv. Naumia sana kuona hii Fani yenye Heshima kubwa duniani kote sasa hapa Tanzania ikiwa ipo ICU na Siku si nyingi inaenda Kufa kabisa. Sikatai ujio wa Teknolojia kwani hilo ni Jambo jema ila pamoja na Teknolojia lakini ile Misingi Mama ya Utangazaji / Uandishi wa Habari haijabadilika na wala haitokuja Kubadilika. Na kinachonisikitisha zaidi Sisi ambao ndiyo Wahusika tumenyamaza na wala hatuhoji hivyo kuendelea tu kuruhusu Upuuzi na Ukiukwaji mkubwa wa Kimaadili kuendelea kuwepo", amesema Mtangazaji Mkongwe, Mshindi wa Kike wa Afrika wa Tuzo ya Uandishi wa Habari za Ukimwi na Mweledi wa Tasnia Elizabeth ( Betty ) Mkwasa alipokuwa akizungumza na TBC1 katika Miaka 73 ya Utangazaji Tanzania.

GENTAMYCINE kila mara nimekuwa nikiisema hapa JamiiForums hii Tasnia ya Habari na Utangazaji halafu naonekana kama vile nina Nongwa nayo au nina Agenda nayo / nao Binafsi na wapo hadi Wanaonishutumu haya sasa leo kasema Mhusika mwenyewe hebu mbishieni basi na Yeye au Mshutumuni kama mfanyavyo Kwangu.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE a.k.a Akili Kubwa na Tajiri wa Maono hakuna ambacho nakisema JF huwa hakiji Kutokea Ok?
Zembwela nae mtangazaji?
 
Back
Top Bottom