TANZIA Bi. Saada Ali Hassan amefariki Dunia katika hospitali ya Mnazi Mmoja

TANZIA Bi. Saada Ali Hassan amefariki Dunia katika hospitali ya Mnazi Mmoja

Wakati tunawaonya kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi, wengi mlikaza shingo.
R.i.P Bibi, yamkini ungelijua kwamba leo ulie mpigania ndio kwanza anakula meza moja na mtesi wako...😪
Sidhani kama bibi alitoka nje kwenda kupambana zaidi ya kufuatwa alipokuwa amejipumzisha.
 
KESHO YETU ANAIJUA MUNGU TU LEO TUNAAPA WENGINE TUNAZIKA RIP
MLIOBAKIA MUWE NA FUNDISHO MSHIKAMANE MJENGE ZNZ YENU ACHANENI NA WAHUNI
 
Oho God. Mzee wa watu , Mtanzania huyu. Kipigo kimemfanya atoke duniani. Hiki kilio hakitawaaacha salama wanasiasa na vyombo vilivyoshiriki kuwatesa Watanzania .

Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Bi Saada Ali Hassan ambaye amefariki majira ya saa saba za usiku katika hospital ya Mnazi Mmoja. Idadi waliopoteza maisha yao kama sehemu ya uchaguzi inaongezeka

Poleni wafiwa na HAKI itapatikana tu Insha’Allah Pumzika kwa amani

View attachment 1644429
Inasemekana bibi aliposikia Maalim anaenda kuunga mkono juhudi, aliona bora ajifie tu.
Apumzike ka Amani.
 
Usimtetee kabisa maana alikuwa akiongea anaweka msisitizo wa ushari na kuhamasisha vurugu, viko wapi sasa leo anaapishwa wengine wanauguza majeraha, Visiwani igeni tabia ya Bara wenzenu tunawasikiliza tu na kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii lakini kwenye vurugu huwa tunawaambia watangulie wao na familia zao na Sisi tuwafuate,

Ila huyu mama yangu sijui yamemsibu yepi maana siamini kama alishiriki ktk vurugu
Alipigwa na polisi baada kukutwa eneo ambalo polisi waliliona kama la vurugu, huamini nini sasa ?, watu wengi wamedhuriwa na polisi kwa ujinga wa polisi, polisi makini anatumia akili yake kabla ya kuchukua hatua yoyote ambayo inaweza kudhuru, wangapi wamejeruhiwa na polisi wakiwa hawana makosa ?, hawa policcm ni wa kulaani kwa nguvu zote na pia serikali haiwezi kukwepa laana ya damu iliyomwagika hapo
 
Hivi nyinyi wengine mbona huwa wapumbavu saana!! sasa hapa unashabikia ujinga wa police wa ccm ?, stupid kabisa, hivi mnadhanai tukiendelea kuwachekea hawa polisi kuna siku watakuja kuheshimu haki za binadamu ?

Ujue, hakuna mahala popote ambapo polisi anaruhusiwa na sheria kumpiga mtu, sheria inataka mtu anapokosa apelekwe mbele ya mahakama, Hakimu ndie anaeweza kutoa hukumu, sasa hapa polisi wanapiga na kujeruhi watu kabla ya kuwapeleka mahakamani, ni kosa kubwa polisi kumpga mtu anapokuwa kwenye maandamano kwa sababu maandamano yapo kwa mujibu wa sheria za nchi, sio za ccm
Maandamano yanaweza kuwepo kisheria,je kibali cha kuandamana wanacho pia? Mbaya zaidi ndio hao viongozi wao wanaungana kuendelea kula bata. Inaumiza sana, ila na sisi raia tuwe makini na ushawishi wa wanasiasa njaa,wanatutumia kisha wanatuacha tufe.
 
Sijawahi sikia tza uchaguzi umewahi pita salama bila kumwaga damu za watu
 
Back
Top Bottom