TANZIA Bi. Saada Ali Hassan amefariki Dunia katika hospitali ya Mnazi Mmoja

Wakati tunawaonya kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi, wengi mlikaza shingo.
R.i.P Bibi, yamkini ungelijua kwamba leo ulie mpigania ndio kwanza anakula meza moja na mtesi wako...😪
Sidhani kama bibi alitoka nje kwenda kupambana zaidi ya kufuatwa alipokuwa amejipumzisha.
 
KESHO YETU ANAIJUA MUNGU TU LEO TUNAAPA WENGINE TUNAZIKA RIP
MLIOBAKIA MUWE NA FUNDISHO MSHIKAMANE MJENGE ZNZ YENU ACHANENI NA WAHUNI
 
Inasemekana bibi aliposikia Maalim anaenda kuunga mkono juhudi, aliona bora ajifie tu.
Apumzike ka Amani.
 
Alipigwa na polisi baada kukutwa eneo ambalo polisi waliliona kama la vurugu, huamini nini sasa ?, watu wengi wamedhuriwa na polisi kwa ujinga wa polisi, polisi makini anatumia akili yake kabla ya kuchukua hatua yoyote ambayo inaweza kudhuru, wangapi wamejeruhiwa na polisi wakiwa hawana makosa ?, hawa policcm ni wa kulaani kwa nguvu zote na pia serikali haiwezi kukwepa laana ya damu iliyomwagika hapo
 
Maandamano yanaweza kuwepo kisheria,je kibali cha kuandamana wanacho pia? Mbaya zaidi ndio hao viongozi wao wanaungana kuendelea kula bata. Inaumiza sana, ila na sisi raia tuwe makini na ushawishi wa wanasiasa njaa,wanatutumia kisha wanatuacha tufe.
 
Sijawahi sikia tza uchaguzi umewahi pita salama bila kumwaga damu za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…