Hiyo biere sitokuja kuisahau,2000+ years niliwahi kuishobokea kwa fujo Kama chupa nne hivi za baridi, nilijamba cheche siku hiyo.
Pale soko jipya kawe enzi hizo nilikuwa naishi mbezi chini.
Aseee ilikuwa saa 10 jioni hivi ilipofika saa 12 nikawasha pira mpaka home sikumbuki nilifikaje hapo naamini malaika wapo.
Mbaya zaidi nilikuwa peke yangu home, wameanza kurudi alikuwa mshua. Asee mshua aligonga kengele hola, alipiga simu yangu hola,
ilibidi abonye security alarm maana alikuwa anatembea nayo kwenye Gari. Ndiyo wakaja hao knights support wakaruka ukuta kuingia ndani wakakuta nimekata moto, Ilibidi niwekewe drip.
Baada ya hapo mshua akasema Sasa bongo hii uhame utakufa kabla Mungu kupenda hicho ndiyo chanzo Cha kwenda State.
Sikuiyona Tena hiyo bia hivyo kama bado ipo nitaitafuta pambano lirudiwe maana ilinipiga kwa TKO first round.