Kinachoniumiza ni kuwa kwa vyovyote vile ukiwa masikini utaendelea kuwa masikini tu kwasababu kelele ni nyingi masikioni mwa masikini .
Mara panda miti itakutoa , walipojaribu maliasili wakasema tutaona [emoji3]
Mara nenda kachimbe madini huko wakaishia kuliwa hela kwa waganga na kuangukiwa na kifusi [emoji3] wakapungua idadi.
Mara chipsi zinalipa tafuta kijiwe huko wakaishia kufukuzwa na mgambo wa jiji ati sio eneo maalumu la biashara [emoji3]
Mwingine akamwambia kuwa bodaboda maana utapata hela zaidi ya maticha wote nchini [emoji3] huko masikini wa watu wakaishia kupata ajali na kuvunjika miguu wako nyumbani wanawategemea masikini wenzao
Cc
mpwayungu village
ROBERT HERIEL akawaambia masikini jutahidi kuwa bahili ili uwe tajiri masikini wa watu wakafa na utapiamlo na kwashakoo wao na watoto wao.
Wakaambiwa nenda kalime maana mali utaipata shambani [emoji3] huko Mungu akawaambia sijawaita huku nyie akagoma kuwapa mvua .
Basi wanaharakati wakasema maendeleo ya mtu yataletwa na serikali yao ndiyo kwanza madaktari wa heshima za tozo , umeme na rushwa wakaongezeka nchini .
Mwisho ewe masikini popote ulipo unasoma hiki kipande wasikudanganye chochote hawa walioshiba nenda kafanye chochote ukipata mkate kwaajili ya familia ikutoshe kusema wewe ni tajiri maana hapa kwenye hii dunia tunapita masikini wewe .
Acha kuwaza makuu wakati vizazi vyako havikuwa nayo pambana upate chakula cha kutosha hayo mengine ni anasa bwana masikini[emoji3]
Ukiendelea kuwasikiliza hawa utakufa kwa mawazo rafiki yangu masikini.
Sent using
Jamii Forums mobile app