Biashara gani halali inaweza tengeneza faida ya kuanzia laki tatu kwa Siku?

Umeweka notation ya kilimo na share kwamba huitaji Ila ningependa kukupa njia kupitia kilimo na mifugo waweza toka, kwa kufanya haya
1. Nunua na kuuza pembe jeo kwa wa kulima
2.pia waweza fungua duka la uuzaji wa vyakula vya mifugo
Kama vile Kuku, bata na pia waweza weka machine ya kutotoresha vifaranga... Ni hayo pia nakupa hangalizo, usije ukafanya share na mtu yoyote ata akiwa ndugu yako.. Itakugharimu
 
Hiyo pesa usije ukaichezea huko unakosema kwenye forex au btc, sikushauri. Biashara za kufanya ziko nyingi. Kama una muda hebu chukua milioni 2 tu, nenda kabebe viazi Njombe peleka hapo Masasi tu wala usihangaike kwenda Mtwara wala Lindi, shusha mzigo wako hapo ndani ya siku mbili umemaliza, na kama ni mjanja utakuwa umeshatengeneza network tayari. Na kama una mtu wa kukusaidia unamwacha Njombe wewe unakaa Masasi mnacheza huo mchezo, ni mchezo huku ukiangalia na mahitaji ya mazao mengine kama Maharage. Ni mchezo mzuri, ila uwe na muda tu.
 
kuna order kila mwezi trip 2 nje kutengeneza milioni 15 kwa mtaji huo.mwenye order milioni 5,wewe milioni 5,na mm milioni 5 tugawane kila mwezi.ukiona inalipa na una 12 million cash nitafute tupige kazi.0625648094
Tatizo hujatililika kama wenzako ili kumshawishi kama itamlipa au vip?
Biashara gani hiyo mnayopeleka order nje na mnapiga faida
Usikimbilie kuweka namba tu
Fanunua then mtu akubali namba atakuomba mwenyewe baada ya kuridhia
 
Hiyo 50000 bila shaka ni mauzo! Hapo faida (baada ya kuondoa gharama) ni sh ngapi? Kumbuka chakula chako, na gharama ya muuzaji hata kama ni mwenyewe ni sehemu ya gharama!
 
Hata mm na uzoefu huo ila kwa kiasi hicho bado hajanunua mzani, jiko la kuyeyushia, leseni, akarabati nyumba ya kununulia nk aajiri vijana
2 millions tu unaweza kuanza kununua DHAHABU!

Inategemea unataka uwekeze kwa kiwango gani!
Wewe unazungumzia Jiko la kuyeyushia n.k....mwenzio anazungumzia labda kununua Mercury na kwenda Site!
 
Kasome kifungu kifungu cha VI cha hiyo sheria 1-4 wameandika na adhabu zake kwanza huruhusiwi kujishughulisha na shughuli za madini kama huna leseni ukikamatwa madini yanachukuliwa na unashtakiwa we jipe moyo na ujuha wako huo
Hahaha kaka ukianza kuwaza vifungu vya sheria nchi hii utoboi mkuu
 
How is he going to get experience without practice it?
 
Wooote naona munaongelea dhahabu mara leseni mara achimbe mara anunue auze lakini munasahau kabisa kuwa anaweza kufanya biashara ya kusuport mining process kama KUKODISHA COMPRESSORS NA MACHINE ZA KUDRILL. ANAWEZA KUJENGA BAA NA HATA MGAHAWA HUKO.MOGODINI NA ZIKAMLIPA HIYO PESA KWA SIKU KIULAINI KABISAAA
 
Ukipata mashine ya uchapaji bahasha au vifungashio kwa Ujumla,bahasha za ukubwa wote
Kuna hela hpo si kitoto
 
Waweza ifanyia ht nyumbani ukishapata leseni.,Materials pia si ngumu kuzipata,Usambazaji waweza ufanya mwenyewe pia na watumiaji ni wengi kuanzia stationaries,Restaurants n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…