Biashara gani halali inaweza tengeneza faida ya kuanzia laki tatu kwa Siku?

Mkuu msimuingize huyo jamaa kwenye kununua dhahabu,atauziwa unga wa makufuli yaliyosagwa
 
hahaha umenikumbusha kipindi fulani nilienda kwenye machimbo ya dhahabu Karenge Kigoma nikalala kwenye gest ya mifuko ya cement......sahani moja wali maharage elfu tatu....dah
 
Ww utakuwa mhaya ww maana si kwa mijisifa hiyo
 
Mbona kama unatumia nguvu nyingi kuelezea point zako hizo...msikatishe watu tamaa ...kuna watu tena wanfanya biashara halali na wanapata hio faida ..kila mtu ana mipangokazi yake ailyojiwekea ..sasa wewe nani unayejua location zote za kibiashara hapa tanzania yote hadi usemee hamna mtu anayeingiza hio faida...acha hizo
 
Asante kiongozi nimekuelewa vizuri,vipi biashara ya chakula?.
 
Kuna jamaaa niliwahi mtembelea mkoani Tabora(Nzega) anauza nafaka,aliniambia kwa siku faida anayopata akipata ndogo ni 250K,na nilijaribu kukaa pale kuangalia mzunguko wa biashara yake kiukweli anauza sana.Sema ndio hivo kaanza kuuza nafaka tangu 2007,kwahiyo ana miaka kumi sokoni.
 
Kama biashara ni hasara tu bila faida, inakuwaje iwe bado inafanyika? Wewe unaweza fanya biashara yenye hasara tupu bila faida?
Kwa mfanya biashara akifanya biashara yakula inamuingizia pesa yakula bila kuleta faida ya juu baada yakutoa matumizi hio nisawa na hasara.
 
Mkuu naona umeingia JF kwa gia ya mamba! Ukiwakosa kwenye madini badi unawadaka kwenye udalali wa viwanja!
Mimi sio dalali, madini ni biashara yangu, Kiwanja ni changu nimenunua 2013, saivi nimepata shida ndio nakiuza
 
mzee inawezekana kabisa akiwekeza kwenye uvuvi.
kuna mda wanapta mpka lki tano
 
Tafuta sehemu yenye watu wengi (kipato cha kati) fungua duka muhimu la dawa (ADO) utapiga mzigo ila simamia kikamilifu kama huna hiyo taaluma mtafute mwenye cheti cha ADO
 
Kama uko dar ingia kwenye biashara ya vitafunwa especially chapati na maandazi ila fanya chai ya rangi bure.Fanya iwe mobile kitchen kwenye gari kama kirikuu au hiace kukuu ambayo unaweza pata hata kwa m3 .Gari yako asubuhi inaenda kutega kwenye centre zenye watu wengi kama kariakoo,mbagala,posta,ilala etc.

Target yako inakua ni kuuza chapati 400 kwa sh 500 na maandazi 200 kwa sh 200 kila siku asubuhi.Target ya hiyo faida utaifikia tu.
 
Biashara ya chakula ndiyo sahihi kwa hapa Tanzania. Kuna wanadamu mil 55+ Tanzania ambao midomo yao mil 55+ ina njaa kali. Tumia hiyo fursa kuilisha. AZAM ANAPIGA GAP HAPO TU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…