Biashara Gani Ina faida Nzuri?

Biashara Gani Ina faida Nzuri?

Kuhusu biashara gani inayoingiziza hiyo faida au zaidi kwa siku ni swali pana sana (too general). Inategemea una mtaji kiasi gani, na moyoni mwako unapenda biashara za aina gani. Baadhi ya biashara kwa upana wake na faida kwa siku ni kama ifuatavyo

  1. Nunua dala dala ndogo (Hiace au Nissan Carravan) kwa milioni 20. Kila siku itakuwa inalaza 35,000/=
  2. Nunua Yutong bus kwa around 100 milion peleka Arusha. Kila siku italaza around 500,000/
  3. Nunua Scania Semi trailer kwa 90 milioni, Peleka mizigo Zambia, Congo, Malawi, au kubeba containers bandarini. Utalaza wastani wa 200,000/ kwa siku
  4. Nunua mayai kitunda kwa tsh 5500 trei jitume kutafuta wauza chipsi walau kumi watakaonunua trei tatu kila mmoja kwa siku wauzie kwa tsh 6500, utalaza walau 25,000/ kwa siku kama faida
  5. Jiunge kukatisha tiketi Ubungo terminal, ukipata wateja 10 kwa siku utapata 20,000
  6. Nunua Suzuki Carry kwa 7 milion kabebe miziko masokoni, utapata 40,000 kwa siku
  7. Anzisha M pesa sehemu yenye mzunguko wa watu wa wastani, utapata 30,000/ kwa siku
  8. n.k.

Duuuu ndio maana naipenda sana JF sio mchezo kabisaaa,maana mkuu umetoa njia zote kabisaaaa na nini cha kufanya,hongera sanaaa

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kuhusu biashara gani inayoingiziza hiyo faida au zaidi kwa siku ni swali pana sana (too general). Inategemea una mtaji kiasi gani, na moyoni mwako unapenda biashara za aina gani. Baadhi ya biashara kwa upana wake na faida kwa siku ni kama ifuatavyo

  1. Nunua dala dala ndogo (Hiace au Nissan Carravan) kwa milioni 20. Kila siku itakuwa inalaza 35,000/=
  2. Nunua Yutong bus kwa around 100 milion peleka Arusha. Kila siku italaza around 500,000/
  3. Nunua Scania Semi trailer kwa 90 milioni, Peleka mizigo Zambia, Congo, Malawi, au kubeba containers bandarini. Utalaza wastani wa 200,000/ kwa siku
  4. Nunua mayai kitunda kwa tsh 5500 trei jitume kutafuta wauza chipsi walau kumi watakaonunua trei tatu kila mmoja kwa siku wauzie kwa tsh 6500, utalaza walau 25,000/ kwa siku kama faida
  5. Jiunge kukatisha tiketi Ubungo terminal, ukipata wateja 10 kwa siku utapata 20,000
  6. Nunua Suzuki Carry kwa 7 milion kabebe miziko masokoni, utapata 40,000 kwa siku
  7. Anzisha M pesa sehemu yenye mzunguko wa watu wa wastani, utapata 30,000/ kwa siku
  8. n.k.

Mawazo chanya haya..asante sn ila hapa mi naona kununua magari ni hela ndefu..deal hapa ni mayai au kufungua M pesa sehem.. i repeat THANKS SO MUCH MKUU
 
yes! I think this is a great thinker ndo maana naipenda jamii forum. Thnx mkuu

kwa uelewa wa haraka juu ya biashara jibu lake la namba tano i dont think so wateja kumi kwa ubungo ambao wanalipa miambili thats uongo couse wao wanaingiza elfu mbili how came upewe 20000 au nimesoma vibaya hizo amount
 
gari ikisharudisha nusu ya pesa uliyonunulia + gari lenyewe ni kama umeshaanza kutengeneza faida kwa kuwa bado gari unayo !
 
Kama watu wote wangekuwa wanachangia positively kama HP 1 jamii ya kitanzania ingeathirika na aura ya prosperity. Sisi sote ni ndugu hapa tunaojivunia values za uafrika wetu so kwanini wadau wengine mnatoa ushauri potofu? Respect due people. Au sio?
 
kwa uelewa wa haraka juu ya biashara jibu lake la namba tano i dont think so wateja kumi kwa ubungo ambao wanalipa miambili thats uongo couse wao wanaingiza elfu mbili how came upewe 20000 au nimesoma vibaya hizo amount

Mkuu bila shaka alimaanisha wale mawakala wa mabasi makubwa ambao kila akipeleka mteja mmoja anapata buku mbili.
 
biashara yoyote ambayo inahusu utoaji wa huduma inaweza kukupatia 20,000 au zaidi ya hapo,,,,, fungua hair cutting saloon, au kupaka rangi na kuchonga kucha wakinadada, au kasomee ku deal na nywele za watoto wa kike utapiga zaidi ata ya mia kwa siku,,,
The profit issue and capital budgeting and repaying the amount of capital invested are two independent issue, we deal with the operating cost and other related costs like depreciation and revenue to find that profit combining the cost of financing but not cost of machine or asset used to generate profit.
acheni lugha mbaya.....
 
Habari wana JF,ningependa ku share ideas na watu wenye uzoefu na biashara, katika biashara kikubwa kinachoangaliwa ni faida , kwa watu wenye uzoefu na biashara mbali mbali nilikua naomba kuuliza biashara gani ya mtaji wa chini inayoingiza faida ya tsh 20,000 na kuendelea kwa siku??????

Tafuta mtaji wako kama wa laki nne au tano hivi:

Amka saa nane usiku, nenda pale soko la Buguruni, magari ya matunda na mboga mboga kutoka mikoani yanapoanza kuingia we ongea na mtu ukamate kama magunia yako kadhaa, halafu unaanza kuwauzia madalali waliochelewa, kwenye kila gunia, tuseme gunia la kabichi unaongeza sh elf moja mia tano mpaka elfu mbili, wakija madalali unawaambia bei yako wao wanaweka kingine kwa juu na kutafta mteja angalia hapo chini:

Bei ulionunua kwa gunia tuseme ni elf 50,000+1500(faida unayoitaka) Dalali analeta mteja 55,000 au 60,000

20,000/1500=13 (point desh desh) kama utakuwa na uwezo wa kununua magunia 15 at least kwa siku unaweza ukandoka na sh 20,000/= halau ni kitu utafanya kuanzia saa nane, tisa kumi unaondoka saa mbili au tatu asubuhi.
Ila kufahamiana na watu wa sokoni ni muhimu, ljua namna ya kuwa handle. kwa hii biashara pia ni muhimu kuwa na namba za madereva wa magari waletao mizigo sokoni na kujua walaji wanapenda kitu gani kwa wakati upi, ni biashara nzuri sana ukiwa siyo mvivu wa kuwahi kuamka asubuhi na inakuruhusu uendelee na shughuli zako nyingine.
 
mkuu biashara ya phamacy ukipata sehemu kama ilipo nakiete yaani faida ni 100% sema leseni zake ni ngumu kupatikana pia mtaji kwa sehemu kubwa ni ngumu kupata

pia kuna vitu vingi ikiwemo kumuajiri nesi mwenye ujuzi(wako wengi mtaani),frame iwe kubwa kiasi,pia A.c si unajia joto na dawa hazipatani

lakini pia mtaji inategemea na kiasi unachotaka kuanza nacho cha dawa

faida ni 100%

enhance njoo huku
 
Nunua vinguo vya watoto vya mitumba utembeze mitaan, ila jaman kama una wazo la biashara kwa mtaj wa elfu20 naona kama unatania vile!
Bwana jitahidi kuelewa swali uckurupuke.........Eeeebo
 
kwa uelewa wa haraka juu ya biashara jibu lake la namba tano i dont think so wateja kumi kwa ubungo ambao wanalipa miambili thats uongo couse wao wanaingiza elfu mbili how came upewe 20000 au nimesoma vibaya hizo amount

mkuu jamaa yupo sawa kabisa hapo anamaanisha kwa wale wanakatisha tiketi za kwenda mikoani na kitu cha ukwl kabisa maana hata mm nimeshuhudia kabisa kwa macho yangu na nilishawahi kupeleka wateja wawili nikapata zangu buku nne!! Na hapo nilikua mwanza pale nyegezi stand yan hawa majamaa wanapesa mbaya maana kama ww ukipata tu mteja anayekwenda mkoani ni mkampeleka ofisini buku 2 yako unapewa
 
Habari.

Biashara zote ngumu na inataka kujitolea kwl kwl km upo vitani. Cha msingi ni location na aina ya bidhaa utakayouza au service utakayoitoa. Angalia biashara ambayo ni mahitaji ya muhimu kwa watu kama vile maji ya jumla, msosi, n.k, service km kinyozi, unakodisha sehemu laki 3 kwa mwezi au chini ya hapo, unanunua vioo, viti na vitu vyote muhimu vya kuzania, unaweka viti vi 4 unaajiri vinyozi, unamwambia kila mmoja akupe elfu 7 kwa siku, wa 4 unapiga elfu 28, usiwaache wakupe hela ya mauzo hlf uwalipe mshahara utaumizwa kichwa.

Biashara ingne, agiza hiace kutoka japan, kununua mpaka kuileta na kuitoa bandarini itakusimamia milion 10, mpe dereva muaminifu akuletee elfu 50 kwa siku, au endesha mwenyewe upige laki na 20 kwa siku faida.

Biashara ingine nunua mifuko kwa katoni ile midogo meusi hlf uza lakini tafuta wateja kabisa wa kuwapelekea na sio ujaze stoo hlf ukose wanunuzi. lkn inalipa fresh.

Kwenye duka la maji unaweza ukaweka m-pesa, unaweza ukanunua mashine ya juice ya miwa ukapia bao, unaweza ukamuweka na fundi simu akawa anakupa buku 5 kwa siku, zingne anazopiga we usijali, kila mtu na rizki yake.

Dah mzee zipo nyingi, kikubwa location, usitake mjini sana maana kodi nazo kubwa, hizo business juu kokote wapiga, hata kitaa nje ya town, ila isiwe nje sana noma nayo. lol

Pamoja.
 
nunua mi2mba ya warembo wa vyuo vikuu. Uwe unawapelekea mavyuoni hasa dsm. Peleka udsm,tia,duce,cbe,magogoni,bandari college,ifm,mwalimu nyerere kivukoni hasa siku za wekend. Tafta mtaji wa lak5tu. Alaf lengesha time table za boom zao wanazopata loan board. Nakuhakikishia huo mtaji wa laki5 utazalisha milioni20 kwa miezi8tu.
 
Mkuu inaonyesha mtaji wako ni kati ya 200000-500000...ningekushauri ukafanya uchuuzi wa samaki kama uko karibu na bahari au ziwa....samaki wana faida sanna....
 
Back
Top Bottom