Biashara gani Kati hizi zitamlipa huyu kijana anayeanza maisha.

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Kuna kijana amemaliza kidato cha nne hana familia inayomtegemea kwa sasa, amepata sehemu milioni 2 anataka kufanya biashara.

Zipi Kati hizi biashara zinaweza kumtoa kwa kipindi hiki.

1. Kilimo
Kwa mtaji huo atafute eneo alime mazao ya muda mfupi kama nyanya, mahindi na maharage, changamoto kubwa hapa ni kupata eneo na mtaji unaweza kuwa kidogo.

2. Kuuza nguo au viatu vya mitumba kwenye minada, awe ananunua mabalo ya mitumba anazunguka kwenye minada na kuuza.

3. Afungue duka la mpesa, tigo na Airtel money.

4. Afungue mgahawa wa chakula

5. Afungue grocery atafute wahudumu wazuri.

6. Atafute eneo afungue carwash

7. Awe anazunguka kwenye minada ananunua ng'ombe anauza.

8.Atafute eneo anunue ng'ombe na mbuzi awanenepeshe na baadae auze.

9. Afungue duka la reja reja.

10. Anunue pikipiki used afanye bodaboda

11. Anunue pikipiki awe anasambaza bidhaa kwenye maduka.

12. Aende porini awe ananunua mazao ya nafaka anauza mjini.

Unaweza ongezea lingine ambalo litamfaa, karibuni.
 
Ipi hapo anayoimudu?
Biashara zote hapo zinhitaji kujitoa, mtaji mkubwa afya na uwepo wake hasa kwa huo mtaji.

Ni vyema akaangalia kile ambacho anauwezo wa kukimudu zaidi na walau ana taarifa nacho.
 
ukiwa na mtaji kuanzia sh milioni 1-5 unaweza fanya biasha hizi.
hasa ukiwa kwenye miji iliochangamka,

tafuta jokofu used kwa bei rafiki benda, tengeneza juic unatafuta eneo zuuli unauza,

miaka fulani nilikuwa na mtaji wa sh laki 5 nilikuwa ninakwenda kiwandani ninanunua vitenge riject na kwenda kuuza mnadani hakika ilikuwa inalipa sana,

kama yupo sehemu anazoweza kulima ninamshauli alime hoho, bamia,

Nyanyachungu, mchicha, spinachi, sukuma wiki, ,

Asilime nyanya wala vitunguu wala tikiti,

Anaweza kutafuta piki piki used kwa milion moja kisha akanengeneza sanduku kuubwa la mbao ,akenda mjini kununua mifuko hii ya kuuza 200-300-500, akanunua mifuko lain na ile laini ya kuingia kilo 2 akanunua dawa za mbu anunua hiriki, abdala sini , karafuu akafunga za mia mia , akanunua betri , na bidhaa nyiiingi anapakia kwenye sanguku ndani ya piki pikianaingia kitaa kuuza, hii iko poa sana,
 
Afanye biashara ambazo hazina probability au probability yake ni ndogo sana na kwa hizo options zako ulizotoa hapo aingie namba 3 na namba 6 ni uhakika hasa akipata location zinazoeleweka.

Kilimo asiguse kabisa hadi ahakikishe pesa zake sio za mawazo, Kilimo ukikifanya kwa stress ni ngumu kukutoa.

Mitumba huwa inatabia mbili, unaweza ukabahatisha ukapata balo zuri na likakutoa mazima pia unaweza ukapata ronya likakuumiza.

Pikipiki used sio idea mbaya sana ila shida ni kiwango cha uzima wa hiyo Pikipiki yenyewe so probability yake ya kukutoa ni ndogo kuliko kukuumiza.
 
Kwa nini asilime nyanya wala tikiti?
ukiwa na mtaji kuanzia sh milioni 1-5 unaweza fanya biasha hizi.
hasa ukiwa kwenye miji iliochangamka,

tafuta jokofu used kwa bei rafiki benda, tengeneza juic unatafuta eneo zuuli unauza,

miaka fulani nilikuwa na mtaji wa sh laki 5 nilikuwa ninakwenda kiwandani ninanunua vitenge riject na kwenda kuuza mnadani hakika ilikuwa inalipa sana,

kama yupo sehemu anazoweza kulima ninamshauli alime hoho, bamia,

Nyanyachungu, mchicha, spinachi, sukuma wiki, ,

Asilime nyanya wala vitunguu wala tikiti,

Anaweza kutafuta piki piki used kwa milion moja kisha akanengeneza sanduku kuubwa la mbao ,akenda mjini kununua mifuko hii ya kuuza 200-300-500, akanunua mifuko lain na ile laini ya kuingia kilo 2 akanunua dawa za mbu anunua hiriki, abdala sini , karafuu akafunga za mia mia , akanunua betri , na bidhaa nyiiingi anapakia kwenye sanguku ndani ya piki pikianaingia kitaa kuuza, hii iko poa sana,
 
Kuna kijana amemaliza kidato cha nne hana familia inayomtegemea kwa sasa, amepata sehemu milioni 2 anataka kufanya biashara.

Zipi Kati hizi biashara zinaweza kumtoa kwa kipindi hiki.

1. Kilimo
Kwa mtaji huo atafute eneo alime mazao ya muda mfupi kama nyanya, mahindi na maharage, changamoto kubwa hapa ni kupata eneo na mtaji unaweza kuwa kidogo.

2. Kuuza nguo au viatu vya mitumba kwenye minada, awe ananunua mabalo ya mitumba anazunguka kwenye minada na kuuza.

3. Afungue duka la mpesa, tigo na Airtel money.

4. Afungue mgahawa wa chakula

5. Afungue grocery atafute wahudumu wazuri.

6. Atafute eneo afungue carwash

7. Awe anazunguka kwenye minada ananunua ng'ombe anauza.

8.Atafute eneo anunue ng'ombe na mbuzi awanenepeshe na baadae auze.

9. Afungue duka la reja reja.

10. Anunue pikipiki used afanye bodaboda

11. Anunue pikipiki awe anasambaza bidhaa kwenye maduka.

12. Aende porini awe ananunua mazao ya nafaka anauza mjini.

Unaweza ongezea lingine ambalo litamfaa, karibuni.
Namba 4 au namba 9
 
Back
Top Bottom