Biashara gani unayoweza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?

Elezea zaidi kuhusu Shelly's, unawajua Regal pharmaceutical wa Kenya?

Kuna faida zipi kuwa wakala na kuna risk zipi kuleta brand mpya sokoni?
Ninaweza kusema Shelys ni moja kati ya makampuni ambayo yamepenyeza na kuuza dawa zao kwa wingi sana sokoni na mara zote hawajawahi kuja na dawa kisha ikawa na mauzo madogo. Kwahiyo unapokuwa wakala wa kampuni kama hii ni wazi kuwa mzunguko wa biashara unakuwa ni mkubwa sana.

Faida zake ni kwamba wakati wanakuletea mzigo kuna kuwa na mzigo mwingine ambao unakuwa ni kama bonus, na mara nyingi utapokea mzigo mkubwa kuliko kile ulichostahili kutoa kama ungekuwa unanunua ilu ukauze, sambamba na hayo kuna incentives mbalimbali ambazo hutolewa pale unapofikia na unapovuka matarajio ya mauzo kwa kipindi kadhaa kama vile Magari (ya maana) nk.

Hapa chini ni orodha ya dawa zilipo sokoni chini ya Shelys:-

COLDRIL, AZUMA, HEMOVIT, ALBENDAZOLE, ERTHROMICINE, PANADOL, SHELADOL, ACTION ,GOODMORNING, DICLOPER, CYPROFLOXACIN, MALAFIN na nyingine nyingi tu.

Hebu angalia hizo dawa kisha uniambie ni dawa gani hapo ambayo haikukimbiza sokoni? Fikiria umekuwa wakala wa kampuni kama hiyo, kisha ujiulize mzunguko wake. Nina mfahamu jamaa mmoja aliyekuwa wakala wa Shelys kanda ya ziwa (Ashif Ladhan) walipiga sana hela enzi hizo.

Kuhusu Regal pharmaceuticals sifahamu mengi zaidi kuwahusu japo ninatambua uwepo wao.
 
Kuna jamaa walionzisha KAMANGA MEDICS pale Mwanza, nadhani kwasasa ni mabilionea (in Tz shillings), kuna jamaa mmoja pia pale Arusha.

Upande wa Afya kunalipa sana sema ni biashara fulani hivi critical inayofuatiliwa sana na mamlaka.
 
Kuna jamaa walionzisha KAMANGA MEDICS pale Mwanza, nadhani kwasasa ni mabilionea (in Tz shillings), kuna jamaa mmoja pia pale Arusha.

Upande wa Afya kunalipa sana sema ni biashara fulani hivi critical inayofuatiliwa sana na mamlaka.
Ishu ni vibali vyote uwe navyo na ufuate kanuni zote kama inavyotakiwa,ukighushi kitu kidogo tu ukashtukiwa unafungiwa kutoa huduma.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Ashif Ladhan, kuna duka lake mitaa ya Liberty Mwanza?
Kumbe alikuwa wakala wa Shelly's?
 
Kumbuka,yeye anataka Milioni 300 kwa mwezi
 
SEMA pesa haitoshi ni ndogo sana ongezea ifike hata 100b ujenge uwanja wa michezo kwenye Moja ya majiji hapa nchini mfano mby! Utanishukuru baadaye
 
Je, ni biashara gani unayo weza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?
Nunua FAW au Shacman 3 za kubeba Mchanga, kokoto na mahitaj mengine ya ujenzi hesabu yake ni 500k mpk 600k ukiwa nazo 3 utapata 1.5 per day...nawasilisha
 
Ashif Ladhan, kuna duka lake mitaa ya Liberty Mwanza?
Kumbe alikuwa wakala wa Shelly's?
Kumbe unamfahamu vizuri kabisa, huyo ni moja kati ya watu waliopiga sana hela kupitia biashara ya madawa maana miaka ile walikuwa ni wachache sana tofauti na wakati huu.

Ndio, alikuwa ni wakala wa Shelys na alikuwa pekeyake akihudumia mikoa minne ya kanda ya ziwa kabla hawajaja kuweka mawakala wa kimkoa.

Juzi nilipita nikakuta kafunga biashara, sijui shida ni nini.
 
Kuna Sunpharm Pharmacy iko Rwagasore Street, ni distributor pekee wa Regal pharmaceuticals toka Kenya, Jamaa katajirikia humo mpaka kujenga hoteli ya Midland hapo katikati ya jiji. Ilifika wakati akazawadiwa gari na Regal ama kweli distributor wanapiga pesa Sana.

Kwa sasa kuweza kuwa distributor sijui utaratibu ukoje?
 
Je, ni biashara gani unayo weza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?

Jenga uza,
Biashara ambayo ukiingia vizuri utapata faida kubwa sana pengine zaidi ya hiyo kwa mtaji ulionao
Lakini inapaswa upate mtu sahihi mwenye huruma maana mafundi tunajijua
Karibu sana kama ukiwa tayari tupeane mpango kazi
[emoji3513] +255 714 122 011
Karibu sana
Hata ukiwa na mtaji chini ya hapo kama milioni 100 hivii utapata faida nzuri sana
 
Yani ukishakuwa distributor wa kampuni inayopeleka dawa vizuri sokoni, utajiri upo nje nje kwasababu ile huwa haina kufeli, wanaotaka dawa fulani zinazozalishwa na kiwanda unachofanyia kazi ni sharti waje kuzchukulia kwako (maana yake ni uhakika wa wateja).

Kupata hizo deals ni kazi sana.
 
Je, ni biashara gani unayo weza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?
Logistics inalipa sana mkuu, nunua brand new truck&trailer za kichina 5, zisajiri kubeba mizigo ya transit kwenda Zambia, Rwanda. Burundi & Malawi utakua na uhakika wa si chini ya USD 50,000 (Approx. 125 Millioni)net kwa mwezi.

Kwa huduma ya Clearing & Forwarding kwa mizigo aina yote, karibu Ruaha Freight Ltd,
Wasiliana nasi;

Ruaha Freight Ltd,
Umati building 3rd Floor, Room No 18 Samora Avenue / zanaki street Dar es Salaam. P.O.Box 62442
Dar es Salaam
.
Email: info@ruahafreight.com
Website: www.ruahafreight.com
Tel: +255222128447

Mob: +255718 866 651 (call or whatsapp).
 
Safi aiseee
 
Ngurue wazuri sana kwbla hujaangalia kwa makini gharama za chakula na matibabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…