Biashara gani unayoweza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?

Biashara gani unayoweza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?

Kuna hilo tangazo la kijani BOND toka CRDB,ukiwekeza unapata riba ya 10.25%.Kwa mwaka unapata 102.5M Kama faida kwa miaka 5 utapata 512,500,000/= wakati huo ushafikiri mradi upi wa kuwekeza.
Hii ni Risk free,na haihitaji usimamizi, mtaji wako utabaki salama na faida juu
Uwekezaji kwenye bank sip risk free ikifirisika mtapewa laki laki
 
Bilioni 1 ukitulia unaweza zalisha bilioni 2 ...Kwa mwaka ...lakini utulie
Namkubali hili. Ukiwa na hela fursa ni nyingi sana tofauti na ukiwa huna. Kama uko siriaz kwanza fikiria kumiliki kampuni itakayokuwa na uwezo wa kudistribute bidhaa au huduma kwa kampuni nyingine.

Bilioni huwezi kuinvest nje ya operation za kikampuni. Utafeli
 
Kitu cha kwanza unapotaka kufanya biashara yoyote ile ni lazima uijue kwa kufanya utafiti wa masoko bila kusahau wapinzani wako competitors, (market research and competitive analysis)
Ikiwa kampuni hawez feli mana kupambana na competition ni kazi ya marketing officers wake
 
Hiyo pesa inafaa uwekeze Baharini ndani ya mwaka utapata faida kubwa.

Hapo inabidi twende cyprus au ugiriki ununue meli(Land Craft) za kubeba angalau tani 100. Kule zilizotumika unapata kwa 350 mpaka 400million. Zikija moja kwa unafanya biashara ya kubeba mizigo ya Dar Comoro au Dar kwenda Madagascar.

Au jenga boti 2 za uvuvi za 250m, kisha tafuta eneo jenga cold room moja na sehemu ya kukaushia samaki kwa umeme au gesi na jua. Pesa nyingine inayobaki nunua Fuso au Scania 94D yenye body ya refrigerator. Mutukula Uganda, Rwanda na Burundi gari ikifika mzigo unachukuliwa na kugeuza.

Samaki na dagaa wa kukaushwa wakongo watakufata wenyewe uwafungie mzigo
Hii ya kupeleka mizigo Comoro na Madagascar kwa trip moja Meli ya tani 100 unapata faida kiasi gani? vp kuhusu mizigo ya kurudi? au unarudi tupu na kama unarudi tupu si hasara hiyo? namaanisha mafuta unayochoma kurudi bila mzigo
 
Hapo mawe anayosaga ananunua wapi?Ni kiasi gani kinahitajika kupata Tani moja ya kokoto?
Kwenye hiyo gari ya laki 7 faida ni sh ngapi?
Yapo maeneo Yana mawe meusi yaani granite,pwani ya kupakana na morogoro unaenda wizara ya madini kupata vibali na muongozo baada ya kujadiliwa na kijiji,zipo crusher za aina mbili mobile na zisizo mobile Zaid check China Bei uendana na uwezo wa kusaga mawe kwa tani.
Faida unatoa gharama ya kusaga kama ni diesel au umeme, wafanyakazi, mashine za kupakia mawe,ulipuaji,nk.
Gharama za kukodi roli kuleta kokoto dar,nk
 
Mkuu import tire za magari utaapiga hata 500ml.kwa mwaka, import uza wholesale I ASSURE YOU!
Shida ya hii biashara upande wa wholesale imeingiliwa na wachina wenyewe, hawa unaweza kuwachukulia poa ila ni competitors wagumu sana kuwamudu.

Kwahiyo usimpe uhakika 100%, anatakiwa ajue atakumbana na changamoto kubwa tu, apambane nazo ili afike hapo.
 
Unanunua Alizeti,mahindi,mbaazi unaenda kuuza sokoni,mfano Alizeti unaweza kukamua na kuuza mafuta na mashudu pia!Hapo je?
Biashara ya nafaka tena kwa mtaji wa 1B, ukiiparamia kwa kutaka uuze kila kitu hutaambulia chochote.


Hapo uliposema " unaenda kuuza sokoni" , unadhani mzigo wa 1B unaupatia soko kizembe eeeh..?

Hiyo ni biashara inayotaka kwenda nayo kidogokidogo (walau 200M) kwakuanza ili utengeneze soko.
 
Mimi nilikuwa nafahamu kwamba asilimia kubwa ya mafanikio ya biashara yanatokana na uwepo wa wateja
Unaweza ukawa na 1b bila wateja hio biashara itakufa
Ukiiweka vizuri ni sawa na kusema mtu ahakikishe uhakika wa soko kabla ya kutumbukia kwenye biashara fulani, na hata kama hana inabidi awekeze sana kwenye marketing ili kuwavuta hao wateja.
 
Ikiwa kampuni hawez feli mana kupambana na competition ni kazi ya marketing officers wake
Si kweli mimi naongea km mfanya biashara zaidi ya mika 35 baada ya kupata elimu ya ujasiriamali pia ni entrepreneur specialist nimebobea kwenye elimu ya ujasiriamali na ninajua kwanini biashara zinakufa na nina ubunifu wangu wa ninikifanyike, kuna kampuni zinakufa kwasababu ya company policies(ineffective policies) and poor entrepreneurship skills, in entrepreneurship we learn how to do business not about business. Labda niseme kwakifupi unaweza ukawa umebobea kwenye elimu ya ujasiriamali na marketing utakumbana na uncertainty catalyzed by individual factors and the four major environmental factors , (Political, Social demographic variables, National economic and Technological factors). Bahati nzuri namalizia kuandika kitabu changu cha ujasiriamali stay tuned
 
Back
Top Bottom