Biashara gani unayoweza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?

Biashara gani unayoweza fanya yenye uwezo wa kuingiza milion 300 kwa mwaka kwa kutumia mtaji wa bilion 1?

Mkuu, nilimaanisha ulichokisema hapo.

Kuna jamaa wapo pale dodoma ndio wanafanya hivyo;
*Wana-import wenyewe
*Wana wholesale pharmacies, ambazo zinatumika ku-supply kwenye maduka madogo ya dawa.
*Wana 1. Kituo cha afya
2. Specialist clinic,
vyote dodoma, ambapo wana jiuzia dawa
*Wanamiliki chuo cha kati, wanafunzi wakiumwa wanapelekwa kwenye kituo chao cha afya au specialist clinic, ambapo mwisho wa siku wanapewa dawa kutoka hapo juu, jamaa wana-make super profit.

Wamejitengenezea ka mduara fulani hivi kwenye biashara yao.

Kutengeneza brand yako ya dawa ni shughuli pevu [emoji1544]
Naona hakuwa anaelewa alipozungumzia swala la kutengeneza brand yake ya dawa.

Hiyo ni shughuli pevu, kiasi kwamba 1B itageuka kuwa si chochote tena.
 
Mmmmmhhhhhhh

Uko serious or you're just making funny of people??

Hiyo billion moja umeipataje halafu ukashindwa kujua biashara ya kuiwekeza hiyo billion moja kupata 300m kwa mwezi???

Biashara inaathiriwa na vitu vingi sana,
1. Management
2. Cost za kuzalisha au kununua bidhaa zako
3. Marketing, Customer care and network
4. Legal issues; kama adherence na legal framework governing your business


Kwa ufupi siyo just wazo BALI kuna vingi ndani yake...
3 na 4 ndio huathiri kwa ukubwa sana kwenye biashara.
 
Kwa sera za biashara za nchi yetu zilivyo fragile nakuomba wekeza tu kwenye real estate.


Jenga nyumba za kupangisha kwenye semi prime areas Arusha , Dar , mwanza.


Nchi yetu sera za kiuwekezaji ni ngumu sana.


Imagine Leo unafungua kiwanda kesho wanabadiri gharama A unit za luku bila taarifa yoyote. Ndio utaongeza bei Kwa mteja ila wateja hutafuta alternative.
 
Biashara ya nafaka tena kwa mtaji wa 1B, ukiiparamia kwa kutaka uuze kila kitu hutaambulia chochote.


Hapo uliposema " unaenda kuuza sokoni" , unadhani mzigo wa 1B unaupatia soko kizembe eeeh..?

Hiyo ni biashara inayotaka kwenda nayo kidogokidogo (walau 200M) kwakuanza ili utengeneze soko.
Chakula mkuu hakimtupi mfanyabiashara b1sio kitu mkuu!
 
Acha utapeli ndugu swali limewekwa public wewe unataka faragha ya nini? tupo wengi tunaofwatilia haya mawazo...kama una wazo weka hapa... mbona waungwana mawazo yao yako wazi? kama angetaka PM na yy asingetaka mawazo kwa JF members public
Nilitaka kujua mtoa mada anauhitaji au kaja kutuzoa akili.Toka aweke bandiko ukimchunguza Kuna sehemu kachangia?.

Au Ndo tumsubirie atoke bar kudanga
 
Si kweli mimi naongea km mfanya biashara zaidi ya mika 35 baada ya kupata elimu ya ujasiriamali pia ni entrepreneur specialist nimebobea kwenye elimu ya ujasiriamali na ninajua kwanini biashara zinakufa na nina ubunifu wangu wa ninikifanyike, kuna kampuni zinakufa kwasababu ya company policies(ineffective policies) and poor entrepreneurship skills, in entrepreneurship we learn how to do business not about business. Labda niseme kwakifupi unaweza ukawa umebobea kwenye elimu ya ujasiriamali na marketing utakumbana na uncertainty catalyzed by individual factors and the four major environmental factors , (Political, Social demographic variables, National economic and Technological factors). Bahati nzuri namalizia kuandika kitabu changu cha ujasiriamali stay tuned
Bado una hoja za kinadharia mkuu. Au mm ndo sijaelewa hapo?. Unamiliki kampuni yenye wafanyakazi wangap
 
Naona hakuwa anaelewa alipozungumzia swala la kutengeneza brand yake ya dawa.

Hiyo ni shughuli pevu, kiasi kwamba 1B itageuka kuwa si chochote tena.
.kwa mtaji wa 1B kisha ukafungua wholesale pharmacy ambayo mwenye 100M nae anaenda fungua m naona sio sawa, na ndo mana nikasema it is better ajikite kwenye importation ya drugs, awe anawasambazia wholesalers, ikiwezekana achukue uagent wa kiwanda fulani cha china/Vietnam au India awe analeta drugs zao hapa,

Kama tu kina GSM na Haier au Mo na LG sema wew unakuwa upande wa drugs
 
Mkuu import tire za magari utaapiga hata 500ml.kwa mwaka, import uza wholesale I ASSURE YOU!
Au afungue hardware kubwa! Auze mashine kubwa na ndogo... vifaa imara vya ujenzi na awe agent wa majina makubwa kama CAT, KOHLER, HYUNDAI, EDON n.k

Mpunga unarudi na ni uhakika ila aunge urafiki wa kibiashara na maguberi wa kihindi, kiarabu na kisomali
 
Bado una hoja za kinadharia mkuu. Au mm ndo sijaelewa hapo?. Unamiliki kampuni yenye wafanyakazi wangap
Kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi siyo kisababisha cha mafaniko kwenye biashara, ninachopingana pia nawewe kuhusu wazo lako kwamba ukiwa na marketing manager ndiyo mafaniko yatapatikana, hapo ndiyo nimetoa angalizo kwamba biashara nyingi zinakufa kutokana na usiyo yatarajia, (uncertainty) ambayo husababishwa na mambo yanayo mzunguka mfanyabisahara ama biasha kuathiriwa na athari za mtu mmojammoja, (individual factors) na mambo makuu manne, (the four major environmental factors) 1. maamuzi ya kisiasa, 2.Jinsi serikali iliyoko madarakani ilivyojipanga kuinua kipato cha mtu mmojammoja, 3. Aina ya jamii inayo izunguka biashara hii nipamoja na elimu ya mtu mmojammjo kwenye jamii husika, (social demographic variables), 4.Mabadiliko ya teknolojia. Haya mambo manne tunayaongelea kwasababu yanaonekana na tunaweza kabiriana nayo endapo jamii itamua kwa dhati
 
Ukinunua hisa za Crdb au NMB
Utapata zaidi ya milioni 150 gawio Kwa mwaka lakini faida yake ni kuwa hutahangaika kununua chochote kingine wala kuajiri yeyote Yule mwingine.....risks ni ndogo sana...
Unaweza hata kuamua kusafiri na kutembea duniani huku unasuburi hela zako ... mwisho WA mwaka ...
Kama hupendi kubahatisha hiyo inaweza faa sana
Wazo sahihi kabisa, maana iyo B uitumbikize mtaani Tra wamekuangalia, manispaa wapo hapo mala fire mala wafanyakazi wanataka kutokea hapo yani kwa mwaka utakuta imebaki 500M na faida amna, mazingira ya biashara Tz sio rafiki hata kidogo
 
Back
Top Bottom