Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Bonge la advise.
 
Hahaha wewe jamaa
Maisha ni fursa ya muda mfupi mkuu. Masuala ya kurithisha utajiri kwa watoto achana nayo, watajihangaikia wenyewe. Muhimu hakikisha wanapata elimu bora basi. Wakikua na wao watahangaika. Sasa una 300M bado unahangaika kuziongeza zifike bilioni ngapi Mkuu? Angalia usije ukaiacha dunia mapema kwa kuhangaikia ubilionea. Kaa ukijua kuwa biashara si lelemama. Katika watu 100 kuna chance ya kama watu wawili tu kutoboa. Wengine ni kuhangaika kila siku mara hiki mara kile, kulalamika biashara haiendi mpaka kufa.
 
Daaah aisee
 
Aisee mi kuna biashara nimeweka milioni 8 napata laki kwa mwezi faida sold ukiondoa mambo yote.... nimejisikia kinda kabisa kwako... hongera mkuu usikate tamaaa utapata returns nzuri be patient
Sii bora hiyo million nane uwekeze kwenye betting tuu.
Michi moja ya yanga tayari una million mbili🤣🤣🤣🤣🤣
 
Bajaji ndo milion 8 mtaji?
Kulikua na mayor wa Tabora alikua anaitwa Ghulam Dewji alikua anamiliki Bodaboda 422(Mia nne ishirini na mbili) na zinaleta hesabu fresh,yaani hapo ndipo unajua kila mtu ana hesabu zake kichwani kwny mambo ya biashara.

Kuna mtu anamiliki pikipiki 1 tu lkn Kijana anamsumbua kuleta hesabu mpk anataka kuumwa pressure.
 
Mwenzako anaweza kuuziwa chupa 😀😀.... Biashara ya madini buanaa
 
kwa Sababu ya mfumuko wa Bei(Inflation) Miaka20 ijayo unajua hio 2mil itakua na thamani kiasi gani?
 
Umeeleza vizuri lakini hapo kwenye misukule ndio umeharibu..... misukule ni udhanifu tu hauna imapct yoyote kwenye biashara yoyote...
 
kwa Sababu ya mfumuko wa Bei(Inflation) Miaka20 ijayo unajua hio 2mil itakua na thamani kiasi gani?
Kwa nini unadhani kuelekea miaka 20 ijayo thamani ya shilingi itaendelea kushuka zaidi na si kuimarika? Unamanisha hii nchi itaendelea kuwa economically stagnant kwa hata hiyo miaka 20 ijayo? Kwamba mtu wa maisha ya kawaida hawezi kumudu gharama za maisha kwa hiyo 2M ya sasa? Kumbuka huyu hatunzi pesa kununua gari ama kiwanja, anatunza kwa ajili ya kununua mahitaji tu ya kila siku..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…