Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Milioni 300 ukiamua kuitunza na kutumia kila mwezi 2M maana yake utakula maisha bila stress kwa miaka 20 ijayo. Sijui umri wako ila kama umri pia umeenda, kwa next 20 years maana yake utakuwa umekaribia kumaliza siku zako za kuishi. Kuja pesa ikakata, na wewe siku zako zinakuwa zinaelekea kukata. Yaani hapo ni kula 2M kwa mwezi bila stress za hii dunia. Maisha ya hapa Duniani ni kuchagua tu, maana utajiri hauingii nao kaburini. Kwanini kujipa stress ufe mapema?
Bonge la advise.
 
Hahaha wewe jamaa
Maisha ni fursa ya muda mfupi mkuu. Masuala ya kurithisha utajiri kwa watoto achana nayo, watajihangaikia wenyewe. Muhimu hakikisha wanapata elimu bora basi. Wakikua na wao watahangaika. Sasa una 300M bado unahangaika kuziongeza zifike bilioni ngapi Mkuu? Angalia usije ukaiacha dunia mapema kwa kuhangaikia ubilionea. Kaa ukijua kuwa biashara si lelemama. Katika watu 100 kuna chance ya kama watu wawili tu kutoboa. Wengine ni kuhangaika kila siku mara hiki mara kile, kulalamika biashara haiendi mpaka kufa.
 
Maisha ni fursa ya muda mfupi mkuu. Masuala ya kurithisha utajiri kwa watoto achana nayo, watajihangaikia wenyewe. Muhimu hakikisha wanapata elimun bora basi. Wakikua na wao watahangaika. Sasa uan 300M bado unahangaika kuziongeza zifike bilioni ngapi Mkuu? Angalai usije ukaiacha dunia mapema kwa kuhangaikia ubilionea.
Daaah aisee
 
Aisee mi kuna biashara nimeweka milioni 8 napata laki kwa mwezi faida sold ukiondoa mambo yote.... nimejisikia kinda kabisa kwako... hongera mkuu usikate tamaaa utapata returns nzuri be patient
Sii bora hiyo million nane uwekeze kwenye betting tuu.
Michi moja ya yanga tayari una million mbili🤣🤣🤣🤣🤣
 
Bajaji ndo milion 8 mtaji?
Kulikua na mayor wa Tabora alikua anaitwa Ghulam Dewji alikua anamiliki Bodaboda 422(Mia nne ishirini na mbili) na zinaleta hesabu fresh,yaani hapo ndipo unajua kila mtu ana hesabu zake kichwani kwny mambo ya biashara.

Kuna mtu anamiliki pikipiki 1 tu lkn Kijana anamsumbua kuleta hesabu mpk anataka kuumwa pressure.
 
Naona mwanzo tu. Kingine naona biashara yako ni risk free ungeingia kweny risk kubwa ungepata kikubwa mfano hyo pesa kweny madini unaweza kushika mara 3 kwa mwaka sema ni risk sana kuuziwa makapi ya madini au madini yaliyoungua na wajanja ,majambazi hata kuuliwa .
Mwenzako anaweza kuuziwa chupa 😀😀.... Biashara ya madini buanaa
 
Milioni 300 ukiamua kuitunza na kutumia kila mwezi 2M maana yake utakula maisha bila stress kwa miaka 20 ijayo. Sijui umri wako ila kama umri pia umeenda, kwa next 20 years maana yake utakuwa umekaribia kumaliza siku zako za kuishi. Kuja pesa ikakata, na wewe siku zako zinakuwa zinaelekea kukata. Yaani hapo ni kula 2M kwa mwezi bila stress za hii dunia. Maisha ya hapa Duniani ni kuchagua tu, maana utajiri hauingii nao kaburini. Kwanini kujipa stress ufe mapema?
kwa Sababu ya mfumuko wa Bei(Inflation) Miaka20 ijayo unajua hio 2mil itakua na thamani kiasi gani?
 
Umenena vyema jomba, ni kweli ngumu kushauri uwiano wa faida husika kwenye biashara usiyoijua. Ila hapo mwisho nigeuze karatasi kidogo.

Hiyo amount inaweza ikawa kubwa kwako kuitake risk lakini ikawa ndogo kwake that's why kathubutu.

Naamini maisha hayafanani, kuna wengine wanawaza mitaji ya billions kadhaa kuna wengine wanawaza walau 200k tu, Yani kichupa kimoko cha Hennessey wakifanyie mtaji kuendesha familia zao.

Tujaribu kujikita zaidi kwenye ROI ratio kutokana na biashara husika bila kuumulika sana ukubwa wa mtaji.

Kidogo nijuacho, hizi term zina implication tofauti kabisa kulingana na aina ya biashara.
☆Revenue
☆Gross profit
☆Net profit

Mfano biashara hasa retails business, zina higher revenue ila net profit kiduchu. Unaweza fanya mauzo ya Mil 100 faida gross profit ikadinda kwenye 10 tu. Ukilimwa kodi hapo unajikuta unabaki na net profit kama 7 tu.

At the same time aina nyingine ya biashara yenye revenue lel say 50Mil ikawa na gross profit ya hata 15 Mil with net profit of around 12 to 11 million.

Hapa mchawi nahisi ni aina ya biashara ndio inaweza kutoa mtizamo sahihi wa kile kinachoingia kama kinawiana na uwekezaji uliofanywa.

Hizo Mil 300 huenda zimejenga mathalan appartment kuna watu wanapangishwa na hizo M5 ni kodi wanazolipa. Kwa mfano kama huo tunaanzaje kusema kua ni ndogo ama kubwa?

Kitu kingine si kila biashara mtu yoyote anaweza kuifanya. Biashara ina involve uncertainty, ranging from low to high risk. Uwezo wa kuhandle stress za biashara ndio zinazoamua ufanye biashara ipi na utaingiza kiasi gani.

As a principle of thumb, the higher the risk the higher the reward. Na kinyume chake ni kweli. Unaweza muelekeza mtu biashara, ikawa ni faida kubwa ila ina risk kubwa zaidi. Kumbe mhusika akipoteza jero tu halali week 3 mfululizo anaiwaza 😂

Later akila loss huyu si ana panic na kuharibu kila kitu? Kiukweli biashara ina mengi. Kuiendea kichwa kichwa inampiga mtu K.O asubuhi mapeeema mno unless awe na misukule yake kando kama wafanya biashara wengi tuliowazoea mtaani.

Binafsi mleta mada akiifafanua zaidi ntachangia zaidi.
Umeeleza vizuri lakini hapo kwenye misukule ndio umeharibu..... misukule ni udhanifu tu hauna imapct yoyote kwenye biashara yoyote...
 
Kweli bila shaka mkuu japokuwa gharama za magari zimeongezeka kiasi.

Hiyo ya wiki hii na imesimamia 110 Milion. View attachment 2333556
255752638242_status_a1e01bf3d0334c818eff8c815befee00.jpg
 
kwa Sababu ya mfumuko wa Bei(Inflation) Miaka20 ijayo unajua hio 2mil itakua na thamani kiasi gani?
Kwa nini unadhani kuelekea miaka 20 ijayo thamani ya shilingi itaendelea kushuka zaidi na si kuimarika? Unamanisha hii nchi itaendelea kuwa economically stagnant kwa hata hiyo miaka 20 ijayo? Kwamba mtu wa maisha ya kawaida hawezi kumudu gharama za maisha kwa hiyo 2M ya sasa? Kumbuka huyu hatunzi pesa kununua gari ama kiwanja, anatunza kwa ajili ya kununua mahitaji tu ya kila siku..
 
Back
Top Bottom