Umenena vyema jomba, ni kweli ngumu kushauri uwiano wa faida husika kwenye biashara usiyoijua. Ila hapo mwisho nigeuze karatasi kidogo.
Hiyo amount inaweza ikawa kubwa kwako kuitake risk lakini ikawa ndogo kwake that's why kathubutu.
Naamini maisha hayafanani, kuna wengine wanawaza mitaji ya billions kadhaa kuna wengine wanawaza walau 200k tu, Yani kichupa kimoko cha Hennessey wakifanyie mtaji kuendesha familia zao.
Tujaribu kujikita zaidi kwenye ROI ratio kutokana na biashara husika bila kuumulika sana ukubwa wa mtaji.
Kidogo nijuacho, hizi term zina implication tofauti kabisa kulingana na aina ya biashara.
☆Revenue
☆Gross profit
☆Net profit
Mfano biashara hasa retails business, zina higher revenue ila net profit kiduchu. Unaweza fanya mauzo ya Mil 100 faida gross profit ikadinda kwenye 10 tu. Ukilimwa kodi hapo unajikuta unabaki na net profit kama 7 tu.
At the same time aina nyingine ya biashara yenye revenue lel say 50Mil ikawa na gross profit ya hata 15 Mil with net profit of around 12 to 11 million.
Hapa mchawi nahisi ni aina ya biashara ndio inaweza kutoa mtizamo sahihi wa kile kinachoingia kama kinawiana na uwekezaji uliofanywa.
Hizo Mil 300 huenda zimejenga mathalan appartment kuna watu wanapangishwa na hizo M5 ni kodi wanazolipa. Kwa mfano kama huo tunaanzaje kusema kua ni ndogo ama kubwa?
Kitu kingine si kila biashara mtu yoyote anaweza kuifanya. Biashara ina involve uncertainty, ranging from low to high risk. Uwezo wa kuhandle stress za biashara ndio zinazoamua ufanye biashara ipi na utaingiza kiasi gani.
As a principle of thumb, the higher the risk the higher the reward. Na kinyume chake ni kweli. Unaweza muelekeza mtu biashara, ikawa ni faida kubwa ila ina risk kubwa zaidi. Kumbe mhusika akipoteza jero tu halali week 3 mfululizo anaiwaza 😂
Later akila loss huyu si ana panic na kuharibu kila kitu? Kiukweli biashara ina mengi. Kuiendea kichwa kichwa inampiga mtu K.O asubuhi mapeeema mno unless awe na misukule yake kando kama wafanya biashara wengi tuliowazoea mtaani.
Binafsi mleta mada akiifafanua zaidi ntachangia zaidi.