Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Ndugu zangu mna akili sana mmewezaje kujua aina ya biashara na kuja na majibu kuwa biashara kweli hazilipi kwa uwekezaji wa 300m...
 
Huyu atakuwa mchawi[emoji1438]‍♀️[emoji23][emoji23]
Madam huyu tajiri naweza kusema ni gwiji wa mikopo yan haogopi mikopo kabisaa kuna kipind overdraft zilitusumbua sana na vile alikua ana bank 4 kachukua mikopo..yan kuna kipindi muhasibu ashawahi nitamkia kampuni inafilisika ndan ya miez miwili ila aka sustain ilikua watu wa bank wanapishana tu kazini! Alaf alikua kaingiza gari 30 kwa mpigo kipindi hicho! Unakuta robo 3 ya magari ni mikopo na yakimaliza anayaombea tena mkopo kama dhamana anakabidhi kadi. Ukiwa na longterm contract thats easy peasy.

Alaf hz kaz ukishatengeneza reliability kwanzia mzigo, mafuta, spare..kila kitu unachukua kwa mali kauli so ni rahisi ku mantain! Also kulikua na skendo kuna kigogo aliweka mzigo pale ana gari kadhaa ila hatujawah ku prove hayo yao wenyewe.
 
T Bills na T Bonds, hazipo muda wote.

Hizi zapatikana muda serikali inahitaji hela, hivyo kupitia BOT inatangaza tender ya kiasi kadhaa kwa return ya kiasi kadhaa mwa muda kadhaa.
Hapo sasa watu wanashindana, serikali inachukua mwenye rate nzuri zaidi

NB hii ni uelewa wangu, masahihisho yatasaidia wengine
 
Kwamba hukufanya mchanganuo wa biashara yako kabla hujafanya uwekezani?
 
Kuna motivational speaker atakuja hapa atakwambia 'mimi nipe mil 10 tu nakupa faida ya mil 3.5 kila mwezi"
Mtaji wa 10m ushindwe pata 100k per month utakua na masihara Mkuu,walahi nakuambia utakua kuna mahali ukoo wenu watu wamepeleka jina lako likapikwe.
 
Sisemi kwa ubaya au kudhihaki au kwa namna yoyote ile ila siku mimi nashika hizo 300Mil

Hakuna Mtu ataweza nikamata kwa pesa tena maisha yake yote,tupo Humu JF tuombeni

uzima ila biashara ya 300mil kukupa return ya 5m kwa mwezi ni Kulogwa huko nakwambia

watu wenye pesa biashara zenu ni za kibosi bosi,hamuangalii Muda mtaopoteza wala hamuangalii faida mtakazopata.

Hamna uchawi wala tunguli mil 300 sio za kurudisha 5m na nina uhakika mkuu hiyo biashara yawezekana hata ofisini haukai,upo zako hukoo unapga tu simu na kuuliza maendeleo ya biashara.

Endelea hivyo hivyo,ongeza tena 300 mil upate 10m , Hebu nikauze zangu kacholi mimi.....
 
Wameshusha kutokana na janga la vita sio matajiri kuamishia mzigo huko maana vita ilipoanza tu nao wakapunguza interest zao, mbali na hivyo BOT &UTT wenyewe wanatamani elimu hii iwafikie wanachi wengi sema hata ikiwafikia bado ni kikwazo kwamaana bonds utazifurahia, ukiwa na mzigo mrefu hata ukiwa na mzigo mrefu pia kimbembe kipo kwenye kupata coupons hasa za BOT sio kitu rahisi kihivyo, mnada ukitangazwa watu wengi wanabid hii imepelekea washiriki wengi wanakosa, let's say serikali inataka kupata bl 20 tu lakini utakuta washiriki wanajitokeza kuikopesha serikali wanafikisha mtaji wa bl 100 wachache wanapata tena hao wachache utakuta wamebid kiasi kikubwa yaani wamenunua coupons kwa bei ya juu, all in all hata ukikosa mnada mwingine ukitangazwa unashiriki mpk unapata, ni muda mrefu bonds za BOT plus za UTT zimekuwa ni bonge moja la mchongo kwa waliosanukia mapema na ambao wanaoendelea kusanuka kwa maana sio kila mtu anamisuli ya kufanya biashara, faida yake ukiwekeza huko unapata faida bila misukosuko huku ukilinda mtaji wako, na kizuri zaidi serikali zote zinakopeshwa na wanachi wake sio Tanzania tu bali worldwide kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo bonds zitaendelea kuwepo tu.
Duh!!! Nilikuwa nimeshaanza kutaka kulitafutia mikakati kumbe siyo kitu straight forward!!!!
 
karibu jf ukutane na maprofesa wabobezi masuala ya uchumi afrika maahariki na kati. ukweli ni kwamba kwa ground vitu havipo rahisi kihivyo.
 
Sisemi kwa ubaya au kudhihaki au kwa namna yoyote ile ila siku mimi nashika hizo 300Mil

Hakuna Mtu ataweza nikamata kwa pesa tena maisha yake yote,tupo Humu JF tuombeni

uzima ila biashara ya 300mil kukupa return ya 5m kwa mwezi ni Kulogwa huko nakwambia

watu wenye pesa biashara zenu ni za kibosi bosi,hamuangalii Muda mtaopoteza wala hamuangalii faida mtakazopata.

Hamna uchawi wala tunguli mil 300 sio za kurudisha 5m na nina uhakika mkuu hiyo biashara yawezekana hata ofisini haukai,upo zako hukoo unapga tu simu na kuuliza maendeleo ya biashara.

Endelea hivyo hivyo,ongeza tena 300 mil upate 10m , Hebu nikauze zangu kacholi mimi.....
Naona umekuna na gia Kali San toa mchanganuo Kama wa extrovert jinsi ya kufanya ROI iwe ata 89% ya faida

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Yaani natesekaaa jamani..
Mmmh
Nilivyokua nakula mshahara nilikua na enjoy kuliko now
Hivi unatengenezaje formula ya kujilipa mshahara?

Unajua nimecheka

Kula mshahara raha jamani

Kwenye biashara kuna hela ni unajikopesha na irudi Kama ilivyo

Saa nyingine Bora kuajiriwa tu
 
Mbona wewe unasema umewahi kushika na unalialia humu jamii forum.

Elon musk Tajiri namba moja duniani tunakesha nae Twitter analialia sembuse wewe choka mbaya
Siku ukimiliki hata mill 10 za kwako utaita watu mbwa
 
Acha Ujinga wako wewe Nenda kwenye account za Elon Musk Tajiri namba moja duniani anashinda Mitandaoni na anapost kila siku.

Ina maana hao ndugu zako matajiri wasioshinda Mitandaoni Wana hela zaidi ya Elon ?

Kushinda Mitandaoni sio baseline ya kujua MTU ni Tajiri au sio Tajiri njoo n sababu zingine.
Shida sio kushinda ana post shida anapost nini? Au na yeye akifungua mradi mpya anasema nimefungua mradi wa kiasi kadhaa? Huo ni ushamba. Hata wakina Mo Wana post Sana social media zao ila hawezi leta habari kama hizi. Afu hiyo sio inshu Sana inshu ni kuwa huwezi kumiliki more than 300m afu uingize 5m per month usijue shida it means we bado mgeni kwenye biashara na hiyo pesa huna paka ww
 
nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi.
Niseme tu kwamba kwa hilo neno nililoweka RED hapo imebidi nimezee yote niliyotaka yaandika.

Kwa sababu hiyo pambana na usiache hiyo biashara,ipe muda Matokeo yake utayaona wala hutohitaji nguvu kuona matunda ya investment yako.

Kuwa na mtaji mkubwa haimaanishi utaanza kuona faida kubwa mwanzoni,biashara zinahitaji Muda kama ilivyo ukuaji wa mtoto, kutambaa,kusimama na hatmae kutembea.

Biashara yako hiyo ikianza kutembea kwa mtaji uliowekeza utakimbia hizo hela utakazokua unapata,kwasasa hivi Uvumilivu ni muhimu sana otherwise utapoteza hata hicho kilichopo (mtaji).
 
Hajadanganya B love ni kweli amefanya huo uwekezaji. It's Genuine bonafide,
Jamaa nimemfatilia mda mrefu na baadhi ya shughuli zake nazijua pale morogoro but ni exaggerater mzuri Sana toka anauza vinywaji. . Shida humu jf coz hatufahamiani basi mtu anaweza post chochote bila kujua akijua hatofahamika
 
Nadhani utakuwa "ke" kama nimekosea basi naomba uniwie radhi.

300m unaweza kuziona nyingi Kwa vile hauko nazo, ukiwa kwenye chain ya kumiliki pesa utagundua hizo 300m hazitoshi hata kujenga nyumba ya kisasa ya ndoto yako Kwa kipindi hicho

Kwa vile hii ni forum na hatujuani usitoe mawazo ya kijumla kama vile unafahamiana na huyo mtu

Nikuhakikishe tu kwamba hii pesa sio ya mkopo ni sehemu tu ya kiasi nilichoamua kuwekeza kwenye hii biashara mpya ambayo Bado haijatoa return nzuri
Daah bado unaendelea mkuu kweli nyumba ya 300m isiwe ya ndoto ya Mtanzania...brother maisha unayoyazungumzia ni Watanzania wachache sana wapo hilo kundi nasisitiza sana...
 
SA ni risk ya kutoibiwa kwa wageni ila zipo biashara unaweza kutoa pale...
1. Pombe hii mtaji usipungue 200m maana kodi yake haipungui 65m haipungui kwa 40 ft conteiner la pombe na tbs wanataka 12m
2.Vifaa vya ujenzi hii hata ukiwa na 60m unajaza gari kodi yake utalipia nusu hapo Tunduma...
3.Apples uwe na gari ya refregerator hapo Johannesburg market kila box ni rand 220 kutegemeana na rangi ya apple na idadi yake ndani kodi yake sio kubwa ni Tunda na pia zinalimwa ndani ya sadc wana punguzo lao..
3.uende na Truck lako ukanunue matrekta uuze Tanzania ila kwenye ubebaji ili ubebe mengi weza kuyavunja ZA trekta wanatumia kwa masaa na bei ni nafuu..
4. Chocolate wapo wanapeba chocolate na pipi tuu hapo Cash and Carry na Jumbo johannesburg
5.Mapazia na mashuka hapo Dragon na pia vyombo vya ndani hapo hapo Dragon au China city..
6.Mabegi,viatu na pochi za wakina dada hapo hapo dragon shopping center..
Note gharama ya kusafirisha bidhaa ipo juu ila ukiweza kuwa hata na fusso lako SA zipo biashara nyingi za kuleta Tanzania uzuri unaweza kwenda kwa kuelekezwa tuu na kuarudi Tanzania bila hata ya kukutana alietoa ushauri..biashara ya Pombe kodi ni 100% usikwepe ukikwepa TRA wanachukua mzigo wote maana hata ukilipa kodi faida unapata vizuri tuu mzigo unanunua hapo Messina boda wala haungii ndani ukienda mara moja ni swala la kutuma hela ukiwa Tanzania baada ya kukutana na huyo mzungu depo yao ingine ipo borgsbug pale..
Ni vizuri ukauliza hapa hapa wengine wakaongeza nyama kuliko inbox boashara zipo msidanganywe matairi pia mapya yapo jamaa anauza mpaka usajiliwe unaweka kiasi cha fedha hata ukiuza tairi Johannesburg unapata faida...mara nyingi nakua road kwa hiyo kuingia humu na kushauri nakosa muda ila wengi walikuja SA wengine hata sijaonana nao naona wanaendelea kuja na maroli ya mizigo wanaongeza hasa hawa wauza Pombe..
 
Back
Top Bottom