Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 17,080
- 33,076
Madam huyu tajiri naweza kusema ni gwiji wa mikopo yan haogopi mikopo kabisaa kuna kipind overdraft zilitusumbua sana na vile alikua ana bank 4 kachukua mikopo..yan kuna kipindi muhasibu ashawahi nitamkia kampuni inafilisika ndan ya miez miwili ila aka sustain ilikua watu wa bank wanapishana tu kazini! Alaf alikua kaingiza gari 30 kwa mpigo kipindi hicho! Unakuta robo 3 ya magari ni mikopo na yakimaliza anayaombea tena mkopo kama dhamana anakabidhi kadi. Ukiwa na longterm contract thats easy peasy.Huyu atakuwa mchawi[emoji1438]ββοΈ[emoji23][emoji23]
Mtaji wa 10m ushindwe pata 100k per month utakua na masihara Mkuu,walahi nakuambia utakua kuna mahali ukoo wenu watu wamepeleka jina lako likapikwe.Kuna motivational speaker atakuja hapa atakwambia 'mimi nipe mil 10 tu nakupa faida ya mil 3.5 kila mwezi"
Duh!!! Nilikuwa nimeshaanza kutaka kulitafutia mikakati kumbe siyo kitu straight forward!!!!Wameshusha kutokana na janga la vita sio matajiri kuamishia mzigo huko maana vita ilipoanza tu nao wakapunguza interest zao, mbali na hivyo BOT &UTT wenyewe wanatamani elimu hii iwafikie wanachi wengi sema hata ikiwafikia bado ni kikwazo kwamaana bonds utazifurahia, ukiwa na mzigo mrefu hata ukiwa na mzigo mrefu pia kimbembe kipo kwenye kupata coupons hasa za BOT sio kitu rahisi kihivyo, mnada ukitangazwa watu wengi wanabid hii imepelekea washiriki wengi wanakosa, let's say serikali inataka kupata bl 20 tu lakini utakuta washiriki wanajitokeza kuikopesha serikali wanafikisha mtaji wa bl 100 wachache wanapata tena hao wachache utakuta wamebid kiasi kikubwa yaani wamenunua coupons kwa bei ya juu, all in all hata ukikosa mnada mwingine ukitangazwa unashiriki mpk unapata, ni muda mrefu bonds za BOT plus za UTT zimekuwa ni bonge moja la mchongo kwa waliosanukia mapema na ambao wanaoendelea kusanuka kwa maana sio kila mtu anamisuli ya kufanya biashara, faida yake ukiwekeza huko unapata faida bila misukosuko huku ukilinda mtaji wako, na kizuri zaidi serikali zote zinakopeshwa na wanachi wake sio Tanzania tu bali worldwide kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo bonds zitaendelea kuwepo tu.
Naona umekuna na gia Kali San toa mchanganuo Kama wa extrovert jinsi ya kufanya ROI iwe ata 89% ya faidaSisemi kwa ubaya au kudhihaki au kwa namna yoyote ile ila siku mimi nashika hizo 300Mil
Hakuna Mtu ataweza nikamata kwa pesa tena maisha yake yote,tupo Humu JF tuombeni
uzima ila biashara ya 300mil kukupa return ya 5m kwa mwezi ni Kulogwa huko nakwambia
watu wenye pesa biashara zenu ni za kibosi bosi,hamuangalii Muda mtaopoteza wala hamuangalii faida mtakazopata.
Hamna uchawi wala tunguli mil 300 sio za kurudisha 5m na nina uhakika mkuu hiyo biashara yawezekana hata ofisini haukai,upo zako hukoo unapga tu simu na kuuliza maendeleo ya biashara.
Endelea hivyo hivyo,ongeza tena 300 mil upate 10m , Hebu nikauze zangu kacholi mimi.....
Kwa
hio unataka kupinga kuwa biashara za mabasi haziendeshwi kwa janja janja?
Yaani natesekaaa jamani..
Mmmh
Nilivyokua nakula mshahara nilikua na enjoy kuliko now
Hivi unatengenezaje formula ya kujilipa mshahara?
Siku ukimiliki hata mill 10 za kwako utaita watu mbwaMbona wewe unasema umewahi kushika na unalialia humu jamii forum.
Elon musk Tajiri namba moja duniani tunakesha nae Twitter analialia sembuse wewe choka mbaya
Shida sio kushinda ana post shida anapost nini? Au na yeye akifungua mradi mpya anasema nimefungua mradi wa kiasi kadhaa? Huo ni ushamba. Hata wakina Mo Wana post Sana social media zao ila hawezi leta habari kama hizi. Afu hiyo sio inshu Sana inshu ni kuwa huwezi kumiliki more than 300m afu uingize 5m per month usijue shida it means we bado mgeni kwenye biashara na hiyo pesa huna paka wwAcha Ujinga wako wewe Nenda kwenye account za Elon Musk Tajiri namba moja duniani anashinda Mitandaoni na anapost kila siku.
Ina maana hao ndugu zako matajiri wasioshinda Mitandaoni Wana hela zaidi ya Elon ?
Kushinda Mitandaoni sio baseline ya kujua MTU ni Tajiri au sio Tajiri njoo n sababu zingine.
Niseme tu kwamba kwa hilo neno nililoweka RED hapo imebidi nimezee yote niliyotaka yaandika.nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi.
Jamaa nimemfatilia mda mrefu na baadhi ya shughuli zake nazijua pale morogoro but ni exaggerater mzuri Sana toka anauza vinywaji. . Shida humu jf coz hatufahamiani basi mtu anaweza post chochote bila kujua akijua hatofahamikaHajadanganya B love ni kweli amefanya huo uwekezaji. It's Genuine bonafide,
πππ Sawa mkuu.Mtaji wa 10m ushindwe pata 100k per month
Daah bado unaendelea mkuu kweli nyumba ya 300m isiwe ya ndoto ya Mtanzania...brother maisha unayoyazungumzia ni Watanzania wachache sana wapo hilo kundi nasisitiza sana...Nadhani utakuwa "ke" kama nimekosea basi naomba uniwie radhi.
300m unaweza kuziona nyingi Kwa vile hauko nazo, ukiwa kwenye chain ya kumiliki pesa utagundua hizo 300m hazitoshi hata kujenga nyumba ya kisasa ya ndoto yako Kwa kipindi hicho
Kwa vile hii ni forum na hatujuani usitoe mawazo ya kijumla kama vile unafahamiana na huyo mtu
Nikuhakikishe tu kwamba hii pesa sio ya mkopo ni sehemu tu ya kiasi nilichoamua kuwekeza kwenye hii biashara mpya ambayo Bado haijatoa return nzuri
πππWew hujui kitu Zaid ya Uzi wa kula tunda kimasiara zaid
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Ukiwa na pesa ni rahisi kuingiza pesa.2.5B kwa rate ya 15% unapata 31,500,000 kwa mwezi. It divides to 4.5M kwa kila mtu