gspain
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,920
- 6,081
Ni kweli mkuu, kwa case yako nimeona huko umesema ni mwezi wa kwanza huu kwenye biashara yako, sijajua tatizo liko wapi na ndio maana in the first place sikuweza kutoa maoni kutokana na maelezo ulivotoa kwa ufupi.Ni kweli nadhani hizi changamoto zisikukatishe tamaa, Bado Kuna watu wema humu.
SI unaona huyu bwana HIMARS yeye kaona Mimi nimekuja kutafuta umaarufu humu
1. Inawezekana upo kwenye uwekezaji sahihi lkn labda bado business haija-mature kukupa full potential.
2. Inawezekana projections zilikuwa too high kuliko uhalisia ama zimekuwa affected na variables zingine kwa kuwa business assumptions huwa zinafanyika 'under ceteris peribus' (other things assumed constant).
3. Labda haukuwa na taarifa sahihi kuhusu uwekezaji husika ama hukuwa na taarifa kuhusu baadhi ya mambo yanayoweza kuathiri uwekezaji wako hivyo ama hukufanya risk assessment au kama ulifanya basi hukuwa na proper risk control measures.
All in all, jaribu kufanya analysis ujue chanzo ni nini, na ni namna gani utaweza kutatua ili kusonga mbele na uwekezaji wako. Hapa unaweza kupata ushauri wa kitaalam (consultation) ama kujifunza kwa walio kutangulia kama wapo.
Mara nyingi medium to large business (300m+ inclusive) huwa zinafikia full potential somewhere in the medium to long term. Ni aina ya uwekezaji ambao unahitaji 'stance na si speed' ili uweze kufikia mafanikio.
Kwa kuanzia kama unapata normal profit (the profit necessary to cover running cost) na bado unaona kuna expectations nzuri baadae, unaweza kuendelea maana ku-quit investment pia kuna gharama utaziingia.