Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Ni kweli nadhani hizi changamoto zisikukatishe tamaa, Bado Kuna watu wema humu.

SI unaona huyu bwana HIMARS yeye kaona Mimi nimekuja kutafuta umaarufu humu
Ni kweli mkuu, kwa case yako nimeona huko umesema ni mwezi wa kwanza huu kwenye biashara yako, sijajua tatizo liko wapi na ndio maana in the first place sikuweza kutoa maoni kutokana na maelezo ulivotoa kwa ufupi.

1. Inawezekana upo kwenye uwekezaji sahihi lkn labda bado business haija-mature kukupa full potential.

2. Inawezekana projections zilikuwa too high kuliko uhalisia ama zimekuwa affected na variables zingine kwa kuwa business assumptions huwa zinafanyika 'under ceteris peribus' (other things assumed constant).

3. Labda haukuwa na taarifa sahihi kuhusu uwekezaji husika ama hukuwa na taarifa kuhusu baadhi ya mambo yanayoweza kuathiri uwekezaji wako hivyo ama hukufanya risk assessment au kama ulifanya basi hukuwa na proper risk control measures.

All in all, jaribu kufanya analysis ujue chanzo ni nini, na ni namna gani utaweza kutatua ili kusonga mbele na uwekezaji wako. Hapa unaweza kupata ushauri wa kitaalam (consultation) ama kujifunza kwa walio kutangulia kama wapo.

Mara nyingi medium to large business (300m+ inclusive) huwa zinafikia full potential somewhere in the medium to long term. Ni aina ya uwekezaji ambao unahitaji 'stance na si speed' ili uweze kufikia mafanikio.

Kwa kuanzia kama unapata normal profit (the profit necessary to cover running cost) na bado unaona kuna expectations nzuri baadae, unaweza kuendelea maana ku-quit investment pia kuna gharama utaziingia.
 
Kwa hio hela nafikiri kama ungeiweka kwenye bonds ungeondokana na hizo headaches kabisa. Fanya 12%×300,000,000, hio ni uTT ila BoT wanatoaga hadi 15% at times.
Kiongozi kwa hesabu za kawaida ni kuwa; ukiweka 300,000,000 kwa utt inayo toa 12% utapata faida ya shs milioni tatu (3m) kwa mwezi na ukiweka hiyo inayo toa 15% utapata faida ya 3.75M kwa mwezi; bado ni faida ndogo sana kwa hiyo capital; tofauti yake ni kuwa ni nett profit
 
Ukipata faida zaidi ya Central Bank interest rate, basi una haki ya kufanya hiyo biashara.
That's not the maximum au hata optimum profit, but it's worth doing.
 
Imeanza mambo ya mipasho..tafuta huo mfupa wa 113 umvue mtu then nitafute nikupe tender ya kussuply cements kanda ziwa then uje ulete mrejesho wa taarabu zako umu
 
Logistics ina faida sana ila again , sio kwa kila mtu!
Simu ya dereva kuwa lori limeanguka na copper ya watu imeibiwa inataka ujasiri wa hali ya juu kuipokea na kuifanyia kazi .
BIMA ipo
 
Nilitamani kujua ni bishara ya aina gani ili nipate pa kuanzia kukushauri pengine namna ya kuiboresha kwa kuwa umesha invest (sio kituo cha mafuta kweli?). Ungekuwa bado hujaweka hiyo hela, tungesaidiana mawazo ya nini cha kuanza nacho
 
Imeanza mambo ya mipasho..tafuta huo mfupa wa 113 umvue mtu then nitafute nikupe tender ya kussuply cements kanda ziwa then uje ulete mrejesho wa taarabu zako umu
Bro mpaka nafikia malengo ya kutafuta huo mfupa kweli ntakua sina connection za mizigo kweli?? Niko jikoni me ndo natafuta sub contract nawagawia kazi... kwa sasa tuna kazi ya Rwanda kigali $117 kwa tani., kila trip gari inabakiza 3,100,000 faida na kwa mwez mtu kwenda trip 3 uhakika wengine 4! Siku nikiishiwa kazi ntakuchek mkuu, af usiidharau 113 ndo chombo ya kumtoa maskini mafichoni, mchawi dereva tu mzuri 😁.. pamoja 🤝
 
Pesa inazalisha pesa. Ww wa wapi unataka kuleta hesabu za ajabu!!??
 
Umenena vyema jomba, ni kweli ngumu kushauri uwiano wa faida husika kwenye biashara usiyoijua. Ila hapo mwisho nigeuze karatasi kidogo.

Hiyo amount inaweza ikawa kubwa kwako ku-take risk lakini ikawa ndogo kwake that's why kathubutu.

Naamini maisha hayafanani, kuna wengine wanawaza mitaji ya billions kadhaa kuna wengine wanawaza walau 200k tu, Yani kichupa kimoko cha Hennessey wakifanyie mtaji kuendesha familia zao.

Tujaribu kujikita zaidi kwenye ROI ratio kutokana na biashara husika bila kuumulika sana ukubwa wa mtaji.

Kidogo nijuacho, hizi term zina implication tofauti kabisa kulingana na aina ya biashara.
☆Revenue
☆Gross profit
☆Net profit

Mfano biashara hasa retails business, zina higher revenue ila net profit kiduchu. Unaweza fanya mauzo ya Mil 100 faida gross profit ikadinda kwenye 10 tu. Ukilimwa kodi hapo unajikuta unabaki na net profit kama 7 tu.

At the same time aina nyingine ya biashara yenye revenue lel say 50Mil ikawa na gross profit ya hata 15 Mil with net profit of around 12 to 11 million.

Hapa mchawi nahisi ni aina ya biashara ndio inaweza kutoa mtizamo sahihi wa kile kinachoingia kama kinawiana na uwekezaji uliofanywa.

Hizo Mil 300 huenda zimejenga mathalan appartment kuna watu wanapangishwa na hizo M5 ni kodi wanazolipa. Kwa mfano kama huo tunaanzaje kusema kua ni ndogo ama kubwa?

Kitu kingine si kila biashara mtu yoyote anaweza kuifanya. Biashara ina involve uncertainty, ranging from low to high risk. Uwezo wa kuhandle stress za biashara ndio zinazoamua ufanye biashara ipi na utaingiza kiasi gani.

As a principle of thumb, the higher the risk the higher the reward. Na kinyume chake ni kweli. Unaweza muelekeza mtu biashara, ikawa ni faida kubwa ila ina risk kubwa zaidi. Kumbe mhusika akipoteza jero tu halali week 3 mfululizo anaiwaza 😂

Later akila loss huyu si ana panic na kuharibu kila kitu? Kiukweli biashara ina mengi. Kuiendea kichwa kichwa inampiga mtu K.O asubuhi mapeeema mno unless awe na misukule yake kando kama wafanya biashara wengi tuliowazoea mtaani.

Binafsi mleta mada akiifafanua zaidi ntachangia zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…