Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Kwa hio hela nafikiri kama ungeiweka kwenye bonds ungeondokana na hizo headaches kabisa. Fanya 12%×300,000,000, hio ni uTT ila BoT wanatoaga hadi 15% at times.
Faida nzuri ya uhakika ni kununua bond au hisa kwenye nchi zenye stable economy ambazo uchumi wake hauathiriki na siasa, mfano Canada, USA,nchi za emirates, scandinavian countries, uswiss. Pesa yako inakua salama we unakula gawio tu KILA BAADA ya miezi 3.
 
Nina pharmacy nilifungua kwa mil 20 kwa mwezi napata faida 3.5m hapo nimetoa kila kitu Kodi mishaara ya wafanyakazi nk,wewe mil 300+ unapata mil 5 na bado haujatoa running cost!!!
Biashara yako kuna watu wanakupiga

Nimeshangaa kwa kweli
 
Mwekezaji utasemaje umewekeza mil 300 alafu faida mil 5 kwa mwezi alafu hapohapo unasema hujalipa wafanyakazi na gharama za kuendesha ofisi....FAIDA NI NINI?? Nadhani tatizo limeanzia hapo.
Huyu haelewi vitu vitatu
Envestmnt,matumizi na faida.
 
Z
Hiyo return ni ya juu sana sielewi kwa nini unalalamika. Ume invest 300M returns kwa mwaka ni 60M ambayo ni karibia 20%. hamna biashara nyingine yenye such high returns. Hata treasury bills/bonds annual returns ni around 10%.
Zipo nyingi tu,sio zile za darasani.
Yaani uinvest kwa mwaka 300m upate faida ya m60 hela ndogo sana hii
 
Aisee mi kuna biashara nimeweka milioni 8 napata laki kwa mwezi faida sold ukiondoa mambo yote.... nimejisikia kinda kabisa kwako... hongera mkuu usikate tamaaa utapata returns nzuri be patient
Bajaj
 
Hahah nakubali mkuu,Cha msingi watu wakubali tu biashara sio kila mtu anaiweza.Zile Hi/Lo,Stress,timing,dynamics za bizness hua sio za mchezo mchezo mkuu.

Na Ni vzr Sana kumheshimu mtu ambae anategemea biashara tu kuendesha Maisha yake ya kila siku na Maisha yanaenda fresh kabisa huyo Ni mwanaume/mwanamke wa Shoka haswaa maana anayoyapitia anayajua mwenyewe.

Wale Ndg zangu wa Nina mshahara lkn Nina side business hao wawe wapole tu,bado hawajaelewa vzr wakisemacho na sitashangaa mshahara/madili ya ofisini ndio yanasukuma hio biashara,na ndio maana wengi tu wamegoma kuachia ofisi waende kwny biashara moja kwa moja au siku wakitoka ofisini tu then biashara nazo huyumba au kufa kabisa.
 
Hakuna biashara rahisi kama pharmacy aisee ikikushinda hii zingine hutoweza hata kidogo.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Wakistaafu na biashara ustaafu, unakuta mstaafu ana magari ya biashara uwani mwake nayo yapo juu ya mawe yamestaafu
 
Milioni 300 ukiamua kuitunza na kutumia kila mwezi 2M maana yake utakula maisha bila stress kwa miaka 20 ijayo. Sijui umri wako ila kama umri pia umeenda, kwa next 20 years maana yake utakuwa umekaribia kumaliza siku zako za kuishi. Kuja pesa ikakata, na wewe siku zako zinakuwa zinaelekea kukata. Yaani hapo ni kula 2M kwa mwezi bila stress za hii dunia. Maisha ya hapa Duniani ni kuchagua tu, maana utajiri hauingii nao kaburini. Kwanini kujipa stress ufe mapema?
 
Wee acha tu. Cement jumla unanunua tshs 15000 halafu wewe unaenda kuuza 15500 hapohapo mteja anaomba discount. Biashara ngumu nyie!!!
 
Hahaha wewe jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…