Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Hakuna biashara rahisi kama pharmacy aisee ikikushinda hii zingine hutoweza hata kidogo.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
Sindo hapo sasa, yani biashara ya dawa za binadamu ata uwe na kiduka tu cha dawa baridi we unatoboa

Ukiwa na pharmacy ndio kabisaaa, maana unaweza wekeza 10M na ndani ya miezi 6 Una 25M

Na tangu watu wajue utamu wa biashara za pharmacy ndio wanazidi kujaa tu mjini, kariakoo siku hizi kila ukiona jengo linakarabatiwa ujue inakuja pharmacy hapo

Ni biashara ambayo kwanza haina stress ata kidogo maana haina uteja/mazoea,haina ushindani maana kila mtu atauza tu ata mjaze pharmacy mtaa mzima na kitu kikubwa haina RISK au kama ipo basi ni ndogo sana

Yani mtu unafanya biashara Bei unajipangia we mwenyewe kulingana na vile ulivonunua mzigo wako, wahitaji wa dawa ni wengi kulingana na population ya eneo husika na pamoja na hayo yote faida ni KUBWA sana

Kuna watu wana viduka vya dawa baridi tu vya mtaji wa 1.5 M na Kwa mwezi mtu anafunga 400k, huyu mchangiaji mwenyewe kama kawekeza 20M kwenye pharmacy na anapata 3.5M per month basi hajui biashara
 
Naona iko sawa tu....baada ya miaka mitano au sita, pesa yako itakuwa imerudi..
Kwani wewe plan yako ilikuwa urudishe baada ya muda gani?
 
Nanusa harufu mbaya hapa. Pole kwa kuyasema haya. Hata hivyo la kheri katika biashara yako, labda hii ya sasa italipa zaidi mkuu
Kuna mda unaweza kuwa kichaa kwenye haya mambo ya biashara. Nimewekeza tsh. million mia tatu(300m+) nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi. Hapo sijatoa mishahara ya wafanyakazi na gharama za kuendeshea ofisi.

Wafanyabiashara mna roho ngumu sana, presha nje nje!
 
Wee acha tu. Cement jumla unanunua tshs 15000 halafu wewe unaenda kuuza 15500 hapohapo mteja anaomba discount. Biashara ngumu nyie!!!
Acha tu mkuu, ndo nimetoka kumnyima mteja mzigo hapa sasa hivi, kanunua mahitaji yake na akasema hana 2500Ths tu hivo nimwachie, wao wanaona kama wauzaji waga wanapata faida kubwa sana

Na hapo kanunua mahitaji ya 122500/= Ila yeye kaona kama vile me nimepata sana kwenye hiyo hela yake kumbe me ndo naambulia 4000 tu sasa nikimuachia 2500 eti kisa mteja si nakuwa nimejitia dore na kunusa

Nimemwambia aende tu akiipata hiyo 2500 aje kuchukua mzigo wake maana haziozi atazikuta tu

Alafu kanatokea kamtu huko kanafanya biashara ya pharmacy ikiwa yeye anajipangia mwenyewe aweke rate ipi ya profit kwenye kila dawa, fyoko fyoko fyoko pumbavu kabisa
 
113 nzuri kwa kuanzia maisha, ukiwa serious utatoka. Kuna jamaa alinitumia video za Scania 124 420 trailer Excell RRR complete kwa 35M.View attachment 2333571
Kuna idea uliisemaga humu ya kununua Fuso kwa mtu kwa Bei nafuu then unaipeleka Moshi wanaifanyia makeke ikirudi road iko Kama mpya,nilijaribu kuifanyia kazi aisee wahuni walitaka kunishikisha Gari za hovyo.Karibu watu 7 walitaka kuniingiza Chaka bht nzuri na Mimi nina abc kidogo kwny hizo mambo nikasitisha huo Mpango pesa nikaenda kuifanyia mambo mengine.Ila nitaifanyia kazi Jambo Hilo.

Nilichojifunza inabidi ujue unachokifanya wkt wkt unainunua hio machine kwa mtu,la sivyo utashikishwa kitu Cha ajabu.
 
Kuna idea uliisemaga humu ya kununua Fuso kwa mtu kwa Bei nafuu then unaipeleka Moshi wanaifanyia makeke ikirudi road iko Kama mpya,nilijaribu kuifanyia kazi aisee wahuni walitaka kunishikisha Gari za hovyo.Karibu watu 7 walitaka kuniingiza Chaka bht nzuri na Mimi nina abc kidogo kwny hizo mambo nikasitisha huo Mpango pesa nikaenda kuifanyia mambo mengine.Ila nitaifanyia kazi Jambo Hilo.

Nilichojifunza inabidi ujue unachokifanya wkt wkt unainunua hio machine kwa mtu,la sivyo utashikishwa kitu Cha ajabu.
Bora ulishtuka mapema mkuu, lazima uwe na uzoefu kununua magari ya mikononi mwa watu.
 
Nanusa harufu mbaya hapa. Pole kwa kuyasema haya. Hata hivyo la kheri katika biashara yako, labda hii ya sasa italipa zaidi mkuu
Harufu ipi kaka?
Kwamba Kuna wajanja watataka kuniingiza kingi?
 
Pole sana mkuu!!!Nadhani choice ya aina ya biashara, Mimi ninewekeza sh M7 kwenye kisteshenari changu napata faida ya laki 900,000 kwa mwezi,nawaza kununua mashine kubwa ya kuchapa mabango Mungu akinijaria uzima ndani ya miaka mitano ijayo, ambapo nimeulizia nikaambiwa mashine hiyo Ni zaidi ya 10M.

Hakika mtu akiniuliza biashara ipi inalipa Mimi nitamwambia steshenanari, hasara Ni ndogo Sana, na tena naweza sema Ni zero
Hyo area Ni inategemea umeweka wapi hyo business yako mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kuna motivational speaker atakuja hapa atakwambia 'mimi nipe mil 10 tu nakupa faida ya mil 3.5 kila mwezi"
hii inawezekana kutegemea na aina ya biashara!

mfano anatefuga kuroiler akawalisha inavyotakiwa na akauza rejareja kila mwezi anaweza fikisha hata 4M

hata anayeweka layers mayai yanalipa kama atachanganya chakula yeye mwenyewe!
 
Inategemea ni biashara ipi na nimekwambia naendelea kujifunza. At least ungeniuliza maswali ya msingi ya kunijenga na sio kubeza hapa na kucheka cheka tuu.
Ah sorry mrembo sio kwamba nakucheka bwana wala kukubeza ni mshangao tuu kwamba biashara inakuwa ngumu mpaka mtaji wa 8m unaleta laki moja
 
Back
Top Bottom