Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Kuna muda unaweza kuwa kichaa kwenye haya mambo ya biashara. Nimewekeza tsh. million mia tatu(300m+) nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi. Hapo sijatoa mishahara ya wafanyakazi na gharama za kuendeshea ofisi.

Wafanyabiashara mna roho ngumu sana, presha nje nje!
We naye ! ,hapo ungekuwa na brothels /danguro zako 3 Matata kabisa Kwa hiyo pesa na pesa inabaki , unaajiri enforcers /pimps kabisa ,huduma unatoa Kwa high class clients 50k Kwa kichwa hiyo minimum , hiyo pesa ndani ya mwaka inarudi unaanza kuchezea faida .mjini akili [emoji16][emoji16][emoji16]
Huwezi firisika hata siku moja Kwa hii biashara , labda ujifirisi wewe mwenyewe .
Hii ndio biashara kongwe kuliko zote na ndio IPO miongoni mwa biashara zenye faida toka dunia kuumbwa .
 
Naona mwanzo tu. Kingine naona biashara yako ni risk free ungeingia kweny risk kubwa ungepata kikubwa mfano hyo pesa kweny madini unaweza kushika mara 3 kwa mwaka sema ni risk sana kuuziwa makapi ya madini au madini yaliyoungua na wajanja ,majambazi hata kuuliwa .
mzee wa marudio
 
Kiuharisia biashara inahitaji roho ngumu aina. Ila kwa hiyo hela yako hupaswi kupata faida hiyo kwa mwezi. Kama ni hivyo ikusanye hiyo M.300 yote wekeza kwenye hisa za mabank. Kwa pesa hiyo utakuwa unapata return ya si chini ya Milioni 25 kila mwezi. Na hapo hakuna wa kumlipa,wala hakuna pressure hata kidogo. Unakula hiyo ukiwa umetulia tu nyumbani.

Naitamani sana hii biashara,siku nikipata tu mkwanja mrefu lazima nijitupie huko
25m/300m×100%×12months=100%

Yaani return ya 25mil kila mwezi maana yake kwa mwaka utapata riba ya 100%,yaani ukiweka mil.300 mwanzo wa mwaka then mwisho wa mwaka utakua umetengeneza mil 300 nyingine,jumla uwe na mil 600?

Wazungu tunasema Yaya geteeeeeeeeee.
 
We naye ! ,hapo ungekuwa na brothels /danguro zako 3 Matata kabisa Kwa hiyo pesa na pesa inabaki , unaajiri enforcers /pimps kabisa ,huduma unatoa Kwa high class clients 50k Kwa kichwa hiyo minimum , hiyo pesa ndani ya mwaka inarudi unaanza kuchezea faida .mjini akili [emoji16][emoji16][emoji16]
Huwezi firisika hata siku moja Kwa hii biashara , labda ujifirisi wewe mwenyewe .
Hii ndio biashara kongwe kuliko zote na ndio IPO miongoni mwa biashara zenye faida toka dunia kuumbwa .
Danguro? Sijakuelewa boss
 
Pole sana mkuu!!!Nadhani choice ya aina ya biashara, Mimi ninewekeza sh M7 kwenye kisteshenari changu napata faida ya laki 900,000 kwa mwezi,nawaza kununua mashine kubwa ya kuchapa mabango Mungu akinijaria uzima ndani ya miaka mitano ijayo, ambapo nimeulizia nikaambiwa mashine hiyo Ni zaidi ya 10M.

Hakika mtu akiniuliza biashara ipi inalipa Mimi nitamwambia steshenanari, hasara Ni ndogo Sana, na tena naweza sema Ni zero
Embu tuelezee inalipa kivipi?
 
Check biashara hizi chache kwa mfano
1.Real estate.kununua na kuuza viwanja.mfano unanunua heka 10 kwa m300 then KILA hekta unatoa viwanja 6,kila kiwanja unauza milioni 20
o kwa heka uliyonunua m30 unapata revenue ya m120 so eka kumi unapata total revenue 1.2 bilioni. Toa gharama zote mfano tax, operation cost, nk haizidi milioni 300 per year.
😂😂😂

Aiseee...

Nimeishia apo tu kusoma kwenye hii aina ya kwanza ya biashara nikaweka na kituo! Jomba Hizo ndoto za namna hiyo usizipendelee sana nyakati za mchana. 😂

Unaweza ishi maisha yako yote in illusion.

Kama current market value ya kiwanja husika umeinunua Acre 1 kwa Mil 30. How long will it take kwa Acre hiyo hiyo moja ku'quadruple value yake to Mil 120? Au wafikiri thamani ya viwanja inapanda kama ule msitari mwekundu kwenye thermometer?

Oh yes tufanye kweli usemavyo, so unataka kutushawishi hizi real eastate company za kibongo ni multibillionares entity au sio?

Kwa uchumi mshumaa huu ulioenea tz unafikiri viwanja vinanunuliwa kama unavyonunua pipi madukani eeh?

Anyway nisjichoshe wala nisikuchoshe. Huo ni mtizamo wako pia unafaa kuheshimiwa dah 😎
 
Sahihi mkuu ndo mana gari zina bima comprehensive na mzigo unakatiwa bima pia.. ndo mana nikasema inamtoa mtu makini yan ni kufatilia kwa karibu sana usi relax..anyway hakuna biashara isiyo na risk! the higher the risk...

Boss wangu wa kwanza nilianza nae kazi 2016 deceber ana gari 23..nimeachana nae 2019 ana gari 159! Naongea kwa experience sijahadithiwa.
Ndan ya miaka3 hizo gari zaidi ya 130 zilizoongezeka umejuaje kama zote ni za kwake na zimetokana na faida hiyo tu ya usafirishaji
 
Yani wewe unataka kufananisha biashara ya pharmacy na biashara zingine,Kwenye pharmacy nyie mnapata faida hadi mara Tatu ya bei uliyonunulia bidhaa

Mnanunua powercef jumla Kwa 600-700Tsh nyie mnauza reja reja 2000-2500Tsh, dawa za Minyoo mnanunua 200 mnauza 1000, paracetamol mnanunua 20 mnauza 100 sasa Kwa mtindo huu mnategemea faida yenu na wengine zitakuwa sawa?

Kutana na biashara ambayo bidhaa unanunua 5000 na unauza 6000 ili upate faida ya 1000 na hapo utoe Kodi,chakula na mishahara ya wafanyakazi

Kwa hizo 20M zako ambazo wewe zinakupa faida ya 3.5 per month, me kuna mtu namjua kawekeza kwenye biashara ingine na zinampa 800k Kwa mwezi na bahati yake ni kwamba yeye ndio msimamizi halipi salary

kwahiyo issues sio return bali issue ni return kwenye biashara ipi, ila usikariri kila biashara inafanana na hiyo yako ya pharmacy,
Dah, kumbe dawa Zina faida Kama biashara haramu!!

Hivi mtu ambae hana taaluma ya Mambo ya madawa ya binadamu, akitaka kufungua duka la dawa inawezekana kweli mkuu? Nataka nifungue kaduka mtaani hata ka-milion nne au sita , nipatepo pa senti ya beer
 
Hiyo return ni ya juu sana sielewi kwa nini unalalamika. Ume invest 300M returns kwa mwaka ni 60M ambayo ni karibia 20%. hamna biashara nyingine yenye such high returns. Hata treasury bills/bonds annual returns ni around 10%.
Wasomi chakarikeni kuna biashara mitaji midogo sana faida yakutosha tafuteni maarifa yalipojificha msipeane moyo vinginevyo hawa wasiosoma kila siku watawaacha mbali kwenye swala zima la kujiajiri.
 
Wengi humu watoa michango wengi sio wafanyabiashara yani wanatoa mawazo kutoka Sehemu A waliposikia wanaleta humu na anticipation zao za juuu.

Msidanganyikee wanaofanya biashara wanajua wanachopata. Na wengine wanataja faida za juu wakati wanakula loss kila siku ili uingie na ww ukale loss kama yao hyo inaitwa kifo cha wengi.

So kama unataka bness fanya ile unaipenda ww na usitake mafanikio kwa haraka tengeneza jina na loyal customers wako ipanue na ipo siku utaona mafanikio. Is what am doing now
 
Ila jamii forum bna..eti mtu anasema tu chukua tender fanya logistics utatoka,tender gani unaipata kirahisi kam ulivyoandika ushajua payment yake inachukua muda gani,mara chukua scania itakupa usd 3500,apo hujaondoa bima services wala posho ya dereva
Mwingne anakwambia nimeweka phamarcy 20M nachuku 3M,wakati huo mtu unaemshauri hajui ata panadol zinauzwa wapi kwa jumla na vibali vyake..mwingne anakwambia weka plant ya kusafisha madini wakati huo hujamueleza ushuru wa halmashauri,NEMC na kuna OSHA,kuna WANASHERIA,gharama za hyo plant na kuisafisha...

USHAURI:tafuta biashara unayoipenda saana ifanyie research kwa muda mrefu (ikiwezekana tafuta mtu aliyefanya ingia kwake ata bla malipo,jaribu kuwa mfanyakazi kwa muda flani)utajua ufanye nin?
Sema wewe kiazi, mimi mhogo nitaambiwa nina mizizi! Nikiwaambia huu ukweli huwa wanasema nawakatisha tamaa. Hakuna short-cut kwenye mafanikio. Ukiwa na akili ndogo na ukafuata ushauri unaoandikwa hapa utaishia sehemu mabaya sana. Hapa watu wanarahisisha lakini kwenye ''site'' mbambo ni tofauti mno.
 
Back
Top Bottom