Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Ila kuendesha biashara ni kugumu sana cc mzee alikua na kituo cha kuuza mafuta alipaliza kukikarabati t M/Mungu akamchukua ametuachia deni la kama 70m ivi ila daah huu ni mwaka wa 2 huu tumesua sua kulipa deni tumebakiwa na deni la kama 25m ivi ila mtaji umeenda kwa kweli biashar ni changamoto siku zote izo me cjawahi kuona faida ya ata sh 100 mpk mda huu kukiendesha kituo imekua ni changamoto kubwaa san kwetu cc 😭😭😭
Biashara ina mambo mengi Sana mkuu,usione wenye vituo vya Mafuta walikua wanafanya Mpango Mafuta yanaonekana ni ya transit kumbe yanauziwa humu humu nchini,wanapiga hela kichizi unaona tu mtu anafungua vituo vya Mafuta kila siku.

Tafuteni maarifa mkuu.

Nb:Sijasema mkwepe Kodi mkuu.
 
Check biashara hizi chache kwa mfano
1.Real estate.kununua na kuuza viwanja.mfano unanunua heka 10 kwa m300 then KILA hekta unatoa viwanja 6,kila kiwanja unauza milioni 20
o kwa heka uliyonunua m30 unapata revenue ya m120 so eka kumi unapata total revenue 1.2 bilioni. Toa gharama zote mfano tax, operation cost, nk haizidi milioni 300 per year.

2.Kuwa na plant ya kuponda kokoto total investment ni m250.
Lori moja la kokoto 30 tonn wanauza milioni 1.2 hapa profit ni speed yako ya market unacheza na watu wenye plant za concrete mixers,wakandarasi unawapa percentage yao wakupe tenda.
3.Kusuply madini ya matani mfano chokaa,quartz,nk
4.Kuwekeza kwenye recycling taka za plastic, karatasi,
Huwezi kueleweka kirahisi....

Moja kati ya mishe ulizotaja hapo imemtajirisha sana sana ndugu yangu mmoja ambaye hakusoma kabisa kabisa

Mwanzoni tulijua ni mishe za wasiosoma aloo saa hii vyeo vyote ndiye
 
Mtoa mada sijajua lengo lako LA kuleta huu Uzi humu ni nini hasa,kama lengo lako lilikuwa kupata some basic inputs kutoka kwa wadau lazima ungesema aina ya biashara unayoifanya.
Au unadhani kwamba kuna MTU atakuiga hiyo biashara yako-binafsi ninaamini hamna biashara mpya hapa Tanzania ambayo upo peke yako.
 
Milioni 300 ukiamua kuitunza na kutumia kila mwezi 2M maana yake utakula maisha bila stress kwa miaka 20 ijayo. Sijui umri wako ila kama umri pia umeenda, kwa next 20 years maana yake utakuwa umekaribia kumaliza siku zako za kuishi. Kuja pesa ikakata, na wewe siku zako zinakuwa zinaelekea kukata. Yaani hapo ni kula 2M kwa mwezi bila stress za hii dunia. Maisha ya hapa Duniani ni kuchagua tu, maana utajiri hauingii nao kaburini. Kwanini kujipa stress ufe mapema?
Huu ushauri ni sasa na MTU anayenunua government securities au anayeweka pesa yake fixed.maisha ni machaguo kwa kweli.
 
Milioni 300 ukiamua kuitunza na kutumia kila mwezi 2M maana yake utakula maisha bila stress kwa miaka 20 ijayo. Sijui umri wako ila kama umri pia umeenda, kwa next 20 years maana yake utakuwa umekaribia kumaliza siku zako za kuishi. Kuja pesa ikakata, na wewe siku zako zinakuwa zinaelekea kukata. Yaani hapo ni kula 2M kwa mwezi bila stress za hii dunia. Maisha ya hapa Duniani ni kuchagua tu, maana utajiri hauingii nao kaburini. Kwanini kujipa stress ufe mapema?
300/2=150(miezi)
150/12=12.5(miaka)
300m ukitumia 2m kila mwezi utasavaivu 12.5yrs only.
 
Sasa hapo kuna mambo kadhaa yanaweza kuwa na utofauti kutegemeana na hasa eneo unalotaka kufanyia kazi.

Nb:
Sifanyi personally ila nahusiana nayo indirectly na nna jamaa yangu wa karibu sn ambaye tunafanya naye kazi ambaye anamiliki elution machines/plant, hivyo nna experience ya kutosha kukupa ABCs zake.

Nitaongelea kwa uzoefu wa Chunya:

1. Unaweza kujenga ama kupanga jengo ambalo tayari limejengwa ama kununua kabisa the full project ukipata mtu anayeuza au ukimpa mtu ofa atayoridhia maana kwa Chunya zipo nyingi tu.

2. Kama ni kujenga, unanunua eneo (kuna eneo lililotengwa kwa hizo mishe) unafata taratibu zote za vibali nk then utajenga jengo pamoja na miundombinu yote kama godown, ofisi, vyumba vya kulala, jiko, stoo, toilets, mifumo ya taka nk. Sina actual cost za ujenzi ila itategemea na unataka pawe na muonekano gani zaidi ndio itatoa gharama halisi. Hilo ni jengo tu mbali na machine za kuchenjulia.

3. Kwny kukodi mara nyingi ni kati ya 12m-15m per year, yaan hapo unakuta jengo liko na facilities zote then we unafunga mashine zako unaanza kazi.

4. Kuna taratibu za kufata pamoja na gharama za kulipia kuanzia halmashauri, Tra, NEMC na OSHA.

5. Gharama za machine pia hutofautiana kutkana na ufanisi wake. Mfano za huyu mwanangu zilikuwa around 60m kwa machine 2.

Baada ya kukamilisha hapo labda kingine cha kujiuliza unatarget wateja waje kufanyia kazi kwako au unataka kuchenjua mizigo yako mwenyewe?

Kama ni wateja kuna namna ya kuwa-tap ili wafanyie kazi kwako (hili sitaweka maelezo hapa sabab ni siri ya kazi ya jamaa yangu) ila ukiwa serious ntakusaidia namna ya kuenenda.

Pia unaweza kuwa unanunua makapi yaliyokwisha kuchenjuliwa kwny machine zingine na ukayapima ukaona bado unaweza kupata chochote pia ni fursa, ila hii inategemea na ufanisi wa machine zako maana zinatofautiana kiasi kwamba output ya machine moja inaweza kuwa input kwny nyingine.

Atleast utakuwa umepata mwanga mkuu.
Look at this so selfless fellow! Thank you for your selflessness. Priceless kabisa. Nashukuru sana. In your great education, Manpower hujaizungumizia apo kaka... You shall need engineers?
 
Ungewekeza kwenye basi, Arusha/Dar
Mmiliki wa ma-bus ya Princess Muro yeye alikamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta Kule bandarini(TPA),Mmiliki mwingine wa ma-bus ya Arusha-Dar alikamatwa akiiba tairi za mabus kwny stoo ya watu huko na kumbuka huyo mtuana mabus zaidi ya 20 na kila siku yanaingiza pesa.

Sumri alisema sababu mojawapo ya sababu ya biashara ya mabus kumshinda ni wkt wewe unanunua Mafuta kwa Bei ya soko kumbe wenzako wanajua wanayoyapatia.

Au wewe unaenda kununua tairi za mabus yako kumbe wenzako wanaiba tu stoo.

So point ya msingi Ni biashara yoyoye ile Ni tamu kuisikia tu,Ila siri ya urembo Ni ukiingia Field ndipo utajua.
 
Dah, kumbe dawa Zina faida Kama biashara haramu!!

Hivi mtu ambae hana taaluma ya Mambo ya madawa ya binadamu, akitaka kufungua duka la dawa inawezekana kweli mkuu? Nataka nifungue kaduka mtaani hata ka-milion nne au sita , nipatepo pa senti ya beer
Inawezekana mkuu, Kwa kutumia watu wenye taaluma nawewe ukaishia kuwa boss wao
 
Nina pharmacy nilifungua kwa mil 20 kwa mwezi napata faida 3.5m hapo nimetoa kila kitu Kodi mishaara ya wafanyakazi nk,wewe mil 300+ unapata mil 5 na bado haujatoa running cost!!!
Biashara yako kuna watu wanakupiga
Huyu hio mil 300 angeingixa kwenye Dawa angekuwa anaongea mengine muda huuu...!!
 
Back
Top Bottom