Biashara inayomfaa mwanachuo anayesoma Doctor of Medicine(MD) ni ipi?

Barajuka

New Member
Joined
Sep 4, 2026
Posts
1
Reaction score
5
WAKUU!,mm n mwanafunzi ninayesoma udaktari wa tiba(MD),nipo mwaka wa kwanza sasa nafikiria ninaweza kufanya biashara gani kwa mtaji wa Tshs.500,000 nikiwa chuoni ili niweze kujikimu kimaisha huku nikiendelea kusoma kozi yang ya udaktari.Naombeni ushauri wenu
 
Naheshimu sana daktari alisoma na mpaka kuwa daktari miaka ya zamani
MD kwa maana Doctor of Medicine, ni moto ambao ukisoma taaluma nyingine ni mpaka kuwa Doctor of Philosphy ni lazima usome miaka kadhaa.
Mpaka uwe Doctor of Medicine ni miaka mpaka 6 ndio umalize uitwe MD, na hapo bado miaka kadhaa tena uwe Registrar doctor, halafu miaka mingine ya kutosha mpaka uitwe Consultant(daktari bingwa)
Zamani ilikuwa ni vipanga tu ndio wanafika huku, ila siku hizi majanga mpaka mtu anatoka na diploma anataka kuwa daktari
 
Zamani ilikuwa vipanga wakati zamani hata CBA walikuwa wanasoma MD??. Sasahivi ndo vipanga maana lazima uwe PCB one ya 3 au ya 4 ya 5 unaweza ukakosa,ukitokea diploma lazima uwe na GPA ya 4.5 na kuendelea. Zamani sasa hadi division 2 walikuwa wanaenda kusoma MD, fanya vyote ila usiseme wanaoenda kusoma udaktari sasahivi hawana akili ilihali madaktari wa zamani hadi CBG walikuwa wanabebwa.
 
Hongera kuwa na nia ya kuanza ujasiriamali ukiwa shuleni.

Mimi pia niliwahi kufanya biashara nikiwa chuo, japo kwa mara ya kwanza nilianza nikiwa shule ya msingi

Kwa mtaji wa 500,000 unaweza kufanya japo sio kwa machaguo mengi

✓Fungua kibanda uuze chipsi
Trey 5 za mayai, vifaa vya kukaangia chipsi, viazi, mafuta lita 10, vifungo (chumvi, tomato sauce n.k), nyama kilo moja stake, meza, kabati la vioo n.k

Kwa mazingira ya chuo, unaweza kuanza kupokea oda za wenzio pia ukawa unafanya delivery na wateja wapita njia

Hii ukiifanya kwa ustadi, utakuwa unalaza sio chini ya 20,000 kwa siku

✓Fungua biashara ya matunda, kama upo Muhimbili utakuwa unawauzia wanafunzi na wagonjwa humo humo ndani

Kwa biashara hii, utahitaji sio zaidi ya shilingi 200,000 kuanza biashara

Ni bidii zako kuwahi kwenye masoko ya stereo na buguruni kuweza kupata bidhaa zako kwa bei nafuu

Hapa utaweza kulaza sio chini ya 10,000 Kila siku kama faida
 
Naheshimu sana daktari alisoma na mpaka kuwa daktari miaka ya zamani
MD kwa maana Doctor of Medicine, ni moto ambao ukisoma taaluma nyingine ni mpaka kuwa Doctor of Philosphy ni lazima usome miaka kadhaa.
Mpaka uwe Doctor of Medicine ni miaka mpaka 6 ndio umalize uitwe MD, na hapo bado miaka kadhaa tena uwe Registrar doctor, halafu miaka mingine ya kutosha mpaka uitwe Consultant(daktari bingwa)
Zamani ilikuwa ni vipanga tu ndio wanafika huku, ila siku hizi majanga mpaka mtu anatoka na diploma anataka kuwa daktari
Haujawahi kuwa na akili na hautokuja kuwa na akili
 
Back
Top Bottom