Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Kila siku tunasema CCM na system uchwara hawawezi kupambana na wakati!
Sasa kila kitu kipo wazi! wanaaibika waziwazi, mipango yao yote inawekwa wazi, wananchi wanayajua yote wafanyayo gizani, mabilioni ya pesa zao walizowekeza kuiua Chadema yanaliwa alafu matokeo sifuriš¤£š¤£š¤£
Baada ya CCM na TISS kuwekeza mabilioni ya fedha kuiua Chadema, jambo moja walilosahau ni kwamba Chadema ya sasa ina watu wajanja sana waliojiandaa vyema na mipango yao hiyo ili kuwaanika wazi na ufedhuli wao. Matokeo yake hela zao zimeliwa project yao imedoda na kufa kifo cha mende, sasa kila mtu anajua na kuelewa kuwa its CCM and State sponsored projectššš
Sasa wananchi wanajua Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndo imeratibu suala la Mchome kuandika barua ili Msajili ajaribu kuifuta Sekretarieti ya Chadema.
Sasa Wananchi wanajua zimetolewa hela kuwahonga watu Chadema ili wajiondoe na wahamie vyama vingine kutengeneza propaganda kwa Wananchi kuwa Chadem inakufa.
Tangu Chama cha Mapinduzi kianzishwe mwaka 1977 hakuna mwaka ambao Chama hiki kimeabika na mipango yao kufumuliwa waziwazi kama mwaka huu.
Huko Kagera Katibu Mwenezi wa CCM maji ya shingo hadi ameanza kuongea na kuropoka mambo ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Chadema. Jambo linalothibitisha wazi maneno yaliyotolewa leo na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani kuwa suala la Barua ya Msajili ni hila zinazofanywa na CCM pamoja na System dhidi ya Chadema.
Poleni sana CCM, Poleni sana TISS.
Kwa TISS najua mwaka huu mtajifunza jambo kubwa sana. Jambo hilo ni kuachana na siasa za CCM na kukilinda chama cha Mapinduzi na kujikita kwenye masuala ya msingi kama usalama wa nchi kwenye mambo ya fedha, uchumi, kijeshi na Biashara.
Dunia imebadilika sana. Mnavyozidi kujihusisha na CCM sio tu mnaonesha kuwa ni Idara ya watu wasio na akili bali hamstahili ya kuitwa Idara ya Usalama wa Taifa katika Karne hii ambayo nchi inatakiwa kujikita kwenye masuala ya msingi kwa ajili ya maendeleo yake na ya wananchi wake.