Biashara ndio kitu pekee mbadala wa AJIRA

Mpaka hapa Mtumie milion 20 utampatia wapi na atakuja kujiajiria hii hapahapa bongo.

Unajua kuna watu hapa bongo wakipata kula tu wanazaana wala hawawazi hata kesho tu. Na ukiona inakusumbua kesho ipunguze taswira uliyoijenga kuihusu. Hili ndo jibu la haraka haraka. Haya mambo ya maisha mazuri yaone kama bahati tu
 
🀣🀣🀣 Mimi natoa taarifa silii...kama unavyo sema...hata hivyo biashara nafanya pia ukitaka kuagiza sema...sio lazima unipe pesa naweza nikakutumia mzigo ukipata mzigo wako unanipa mshiko wangu...!

Watanzania Huwa hampendi negative thought mnapenda kusikia mambo mazuri tu ila ya nyuma ya pazia hamtaki kuyasikia ndio maana motivation speaking wanatupiga pesa sana...!​
 
Sema kaka tangia nijiunge JF mwaka 2017 naona wewe unalalamika tu kuhusu MAISHA.

Nadhani hata upewe fursa kubwa kiasi gani sifikirii kama utakuwa positive.

Ebu angalia Mungu alivyokujalia

Una Afya njema.

Una Kazi nayokuwezesha kula ,kuvaa na kulala na kupata matibabu.

Upo nje Dubai wenzako hata ndege hawajawahi kupanda Ila wewe umepanda.

Kabla ya kuondoka Bongo ulikuwa Una kiwanja ,pikipiki ,mke na watoto.


So tabia ya kulilia unbidi kuiacha mkuu kuwa MTU wa kushukuru ndo utaona baraka na utoshelevu wa nafsi.


Nimeona nikwambie hilo mkuu jitahidi uwe positive Sana na uwe MTU wa kutolalamika .

Mafanikio huwa yapo kiroho ukiwa MTU wa kulalamika utabaki chini miaka yote .

Nilikutumia kitabu cha " the magic by Rhoda" ili uanze Ku practice gratitude .

Unaweza kuhama nchi mbalimbali bila mafanikio ikiwa hautakuwa MTU wa gratitude.
 
Shukrani sana nitakisoma vizuri...
 
Jamaa anapenda kutia huruma aisee hadi kero utadhani yeye ni last born wa dunia hii, mbona sisi tunapitia magumu lakini tunakaza. Dunia ya sasa hakuna wa kukuonea huruma zaidi yako.
 
Pongezi kwako na mbu wa dengue kwa kutambua fursa za kibiashara huko dubai. Nashauri pia uige mfano kwa kuwa na whatsapp group au community ili iwe rahisi kushirikishana fursa zilizopo huko hasa biashara ya vitu used.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…