Biashara ndogondogo zinaweza kukutoa mapema ukipeleka mnadani



Safi sana mkuu!hongera sana!atakayetaka kujifunza nadhan kapata pakuanzia
 
manengelo
Uko sahihi kabisa, katika sehemu vijana huichukulia poa mojawapo ni mnadani. Mnadani kuna pesa nzuri tu endapo utatuliza akili yako na kujituma pamoja na nidhamu ya pesa.

Mi nakumbuka mzee wangu hizi kazi za mnadani ndio zilimpa kipato kikubwa. Alikuwa anapiga ishu za minada leo wako hapa kesho pale wiki nzima ni kuzunguka minadani. Enzi hizo tulikuwa tunakaa wilayani Magu kwahiyo ishu zake alikuwa anafanya Kuanzia Nassa, Nyahanga, Dutwa, Karemela, Masanza One nakwingineko bila kusahau Magu mjini penyenye. Alikuwa anadili na ishu za yeboyebo soko lake ilikuwa ni Wasukuma hasa kipi cha mavuno ya Pamba basi pesa ilikuwepo kama yote.

Amepiga hiyo ishu baadae akapata dili akawa anachukua mabondo (hivi ni vile viatu kwa jina maarufu "saa sita utanikoma". ikifika mida hiyo kutokana na jua vinaunguza balaa) alikuwa anatoa Kisii, Kenya analeta pale Magu anapiga kwa bei ya Jumla. Wakati huo watu tunasoma shule za hela kupitia kazi za minadani tu. Saizi ana maduka ya jumla kwa yeboyebo pale Mwanza.

Kwahiyo ishu za minadani kama unamtaji mdogo huko ndio pa kukuzia.
 



Duh..hadi nimesisimka!...
 
Mnadani wanapiga sana hela...watu wengi sana....... Ilikuwa siku ya mnada jua kali zamani kidogo nikapelekaga vinywaji vyangu...... Vikaisha fyuu....kuna siku ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi
Mkuu huo ni mkoa gani?

Love and peace
 
Me nimeuza madera ya msomali sanaa ila nilikuwa sipati Wateja narudi nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Minadani na yenyewe inategemena na sehemu uliyojiweka (location) kwa maana unaweza kupanga biashara sehemu sio.mfano wewe unauza madera ukajiweka kwa wale wanauza mitumba lazima upishane na wateja
Kwahy zingatia location
 
Chakula kizuri sana cha ubongo.
 
Mi nafanya hii biashara sijui nakwama wapi Mana nakula za uso balaa
 
Uko wapi tuchangamkie fursa?
 
Unauza jumla au rejareja ni kitu gani kinakupa shida mkuu funguka
 
Minadani kuna hela sana. Watu wengi wa Bunda, Musoma, Tarime, mikoa ya Simiyu Wametoboa kupitia Minadani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…