Kuna mengi nimejifunza hapa....mkuu mlikua mna import dawa gani na gani?
Kwenye pharmaceutical industry kipindi unaanza ukiwa na team nzurii...ukiweka miezi mitatu ya kuingia mtaa kufanya marketing na uwe na Bei nzurii pia delivery ya haraka una kick off.
SEMA madawa Yana brand nyingi mfano fluconazole tabs Kuna brand zaidi ya 10 kwa uchache flucan,flucoz, fluderm,zocon,flucazol,flucona denk,fungstop, treflucan, diflu,austfluzole
Dawa moja Ina Brand nyingi Sana Kuna cheap brand pia Kuna brand za Bei juu so you need huge capital
Ushindani sokoni Kuna cutrought competition pia kutafuta customer base/ you can't own customer ndio maana Kuna mtu atakupa oda Kwako na ataenda kununua kwingine pia MUHIMU ""A SATISFIED CUSTOMER IS A FREE AGENT""
Mkuu,
Kumbe hata wewe una madini mengi Sanaa...nikipata utulivu ntakua na donoa donoa..
kwanza dawa ni paracetamol zenye box la kijani kutoka china
Japo alisema kwa badae angeanza ku import na nyinginezo.......
Lakini nilichojifunza kwenye pharm industry cha kwanza uhakika wa mtaji uwepo, hii itakufanya uweze kununua mzigo mkubwa kwa wakati ama kupishanisha muda.....
Mfano contena linaweza toka china Leo mpka lifike dsm.... (Bandarini sio chini ya siku 40 na kuendelea hapo ni pamoja na siku za kukaa anchor rage labda itatumia siku 28 itafika pale zinakopaki anchor rage ili kusubr foleni kama ipo ama issue za documentation na clearing ili meli iingie bandarini ambapo ni siku kumi na mbili ...... Inabidi ucheze na ratiba kama ikiondoka Leo mzgo mwingine uondoke next week au kila week unaagiza kama mtaji upo ama unafanya sales kwa haraka)
Kingine ni Kujua bei sokoni....... Kuna wakati unakuta box ni 300,000 sehemu zingine na 310,000 kwingine 290,000..... Kwahiyo unavyo mchek mteja unamsikilizia kama atakupa news maybe dawa zimepanda ama zimeshuka asiposema chochote ni kuandaa invoice, EFD receipts then mzigo umfikie.......
Akionyesha kulia sana labda achukue box nyingi kwa mia tatu pengine.......
Maake ukikaza na bei kubwa watakimbia, ama ikiwa chini utapata faida ambayo siyo......
Delivery na kuzingatia muda.......
Wateja wengi walikuwa wahindi plus wabongo najua wabongo akiomba oda saa hz km Hana haraka hata kesho atakwambia fresh.... Tunajijua 😂
Njoo kwa muhindi akisema saa hz..... Yaani delivery yake fanya haraka it's better umpe taarifa kwamba Leo hutoweza au utachelewa afu umzingue...... Ataenda kwa wahindi wenzie......
Lakini awe mbongo muhindi mkenya kwenye delivery kuwa smart...... Kama huna gari la kampuni hakikisha una watu unaowatumia at least kwenye gari una watu watatu na bajaji ili ukimkosa huyu mwingine ni rahisi kuja na kukupelekea mzigo
Kwa muhindi invoice na risiti ya EFD ni muhimu huna utarudi na mzigo hapo ndo nilipoona tofaut ya wabongo na wao kwenye business.......
Pia mbali na watu wa sales unaweza kutafuta watu au kutoa offer kwa mtu yeyote mradi ajue ishu za kumpata mteja ........ kwamba akipata mteja anaechukua maybe kuanzia box 50+ na kuendelea utamlipa commission hii ilikuwa inatumika sana unapata wateja wengi tofaut tofaut kwahiyo watu wa sales zaidi ni kupeleka mizigo na kukusanya hela......
Niliobserve zaidi hii ..........