Biashara Tanzania ni pasua kichwa. Ukiondolewa kwenye reli, kurudi na kukaa sawa si rahisi

Biashara Tanzania ni pasua kichwa. Ukiondolewa kwenye reli, kurudi na kukaa sawa si rahisi

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Jamani wafanya biashara wenzangu nilicho gundua hapa nchini kila siku mambo hubadilika katika biashara na soko.

Kuna marafiki zangu wawili walipata setback kwenye biashara zao moja alikua na mtaji kati ya 70-80m masuala ya ndoa ya kugawana mali na mke akamuondoa kwenye leri ya biashara mgine alikua ana capital base150-200m aliondolewa kwenye leri ya biashara kwa sera mbovu za uchumi za jpm 2016 Ni lidhani baada ya mda mfupi mwaka au miaka miwili watarudi lerini lakini wapi.

Leo ni meenda kuwajulia hali zao kumbe mambo bado wana jikongoja hawajarudi full kwenye biashara moja gari hana anatumia daladala mgine anatumia gari number 'A' kaipata kwa milioni 6 baada yakuuza harrier tako la nyani aongezee kwenye mtaji wake ilio bakia ndo kanunua hiyo no A.

Jamani kama una mtaji wako utunze kwa makini usiigii kwenye biashara usio jua na huna wakika nao mtaji ukikata kurudusha sio rahisi. Mambo ya meshabadilika sio kama zamani.
 
Jamani wafanya biashara wenzangu nilicho gundua hapa nchini kila siku mambo hubadilika katika biashara na soko.

Kuna marafiki zangu wawili walipata setback kwenye biashara zao moja alikua na mtaji kati ya 70-80m masuala ya ndoa ya kugawana mali na mke akamuondoa kwenye leri ya biashara...
Zamani nilikua najiuuliza kwanini wafanya biashara wengi wana punguza mitaji yao na kujenga majumba, kumbe ni security yao biashara hapa kwetu ni unpredictable, kwa sera moja ya TRA mtaji unakatika kwa siku moja
 
Zamani nilikua najiuuliza kwanini wafanya biashara wengi wana punguza mitaji yao na kujenga majumba, kumbe ni security yao biashara hapa kwetu ni unpredictable, kwa sera moja ya TRA mtaji unakatika kwa siku moja
Sure, sera za nchi zinatakiwa kuwa imara.

Sema ndo hivyo mmoja anakuja na sera ya uwekezaji na uzalishaji. Unaenda kuwekeza huko.

Ghafla anakuja mwingine na sera za biashara huria. Unajikuta uwekezaji uliofanya unapotea na kutoka kwenye reli kabisa. Unpredictable.
 
Leri = reli.
Ni kweli boss inahitaji uvumilivu na akili ya ziada kurudi kwenye mstari ukianguka. Muhimu ni kumwomba sana Mungu kukupa utulivu wa akili unapopatwa na majanga kwenye biashara. Yaani hata kama umeanguka kabisa muhimu ni kuhakikisha àkili yako ipo sawa na huendeshwi na mihemko.

Cha kwanza kubali kabisa kwamba tayari maji yamezidi unga inahitaji muda na mbinu kurudi relini. Katika mikakati mipya pambana sana kukwepa kuchukua mkopo. Bora kama una cheti kutafuta ajira ukapiga kwanza huku ukitunza pesa. Kama ajira hakuna anza na ulicho nacho mkononi. Hata kama ni uchinga bora uanzie hapo.

Tatizo wengi wakianguka wanaanza kuwa na presha na kutokukubaliana na hali. Watakurupuka kuuza vitu na kuchukua mikopo na kujikuta kwenye majanga zaidi. KUANGUKA KWENYE BIASHARA ni kawaida ila kurudi tena relini ni wachache wanaoweza.
 
Leri = reli.
Ni kweli boss inahitaji uvumilivu na akili ya ziada kurudi kwenye mstari ukianguka. Muhimu ni kumwomba sana Mungu kukupa utulivu wa akili unapopatwa na majanga kwenye biashara. Yaani hata kama umeanguka kabisa muhimu sio kuhakikisha àkili yako ipo sawa na huendeshwi na mihemko...
Mkuu ulishawahi kupitia hiyo hali au unatoa tu ushauri kwa kutumia uzoefu wako?
 
Palikuwa na madon ila walipigwa na upepo mpaka wakapotea .

Tulikuwa na mzee mmoja wa kisambaa anaitwa "Mswaki " alisumbua sana miaka hyo alikuwa na nyumba kadhaa ..Alipotaka kufanya leverage kweny biashar zake maana alikuwa mtu wa mafuso kubeba bidhaa kama matunda hata dili za ngozi.

Alichukua pesa kibao bank kwa riba ya juu ,duh! mambo yakabuma alipotea kabisa aliuza nyuma zilikuwa kama nne akabakiwa na moja na zile fuso ndo zilimtia hasara maana zilipiga mzinga na mzigo ukapotea uliharibika na dereva wake alikufa .

palitokea series za ajali ya magari yake kama ma3 yakiwa na mzigo mpaka mzee alizirai..

Bahati nzuri ni mkewe alipambana nae ila sasa yupo vizuri zaidi ya miaka 20 nyuma .


Walikuwepo wakina Hussen pambakali sasa kimya ,kuvimba kwa zamu.


Biashara sio rahisi kama watu wanavyofikria tulishalima na mzee tukishirikiana na bibi sehemu moja iniatwa Mbugani- mkomazi ,heka kama 6 zilipigwa na maji yalikuja mafuriko mpaka shangazi yangu alikata moto (alizimia)


Ila ndo hivyo maisha yanasonga.
 
e2b044f2c1f8b0fe439913145482484e.jpg
enterprenuer jay z. 😃
 
Palikuwa na madon ila walipigwa na upepo mpaka wakapotea .

Tulikuwa na mzee mmoja wa kisambaa anaitwa "Mswaki " alisumbua sana miaka hyo alikuwa na nyumba kadhaa ..Alipotaka kufanya leverage kweny biashar zake maana alikuwa mtu wa mafuso kubeba bidhaa kama matunda hata dili za ngozi.
...
Sometime novo ona biashara inavo pelekesha watu na jinsi wanavo filisika najisemea mwoyoni ebu niendelee na hu mtaji wakuuza madafu kwenye basikeli.
 
Sometime novo ona biashara inavo pelekesha watu na jinsi wanavo filisika najisemea mwoyoni ebu niendelee na hu mtaji wakuuza madafu kwenye basikeli.
🤣🤣🤣

Kama ukiona interview yule jamaa wa magaritz alikuwa anakuambia anazungusha mtaji wa billion na kitu kama faidi ila sasa pesa hana na ana deni la million mia kadhaa.

Hapa kuna msitake ndogo ukifanya utaiona dunia chungu baadhi ya mambo hayo ni mikopo ,kuamini watu ,Ukifanya dhuluma karma ikija kukurudia lazima tu uangukie pua.
 
Ndugu yangu mheshimu sana mtu anayeendesha biashara hadi ikasimama kikamilifu, kuendesha biashara Kuna hitaji utulivu wa mwili na akili, sio jambo la muda mfupi! Wape miaka miwili mingine watarudi kundini kama zamani
 
Back
Top Bottom