Wabongo mkiona mtu amefanya reshuffle ya biashara mnasema kafirisika, Sumry kafirisika lini?
Mfano Mohamed Trans alifirisikaje wakati alikufa mali wakagawana familia sasa mitoto imeleta ubishi kuendesha biashara ikashindwa ikapiga bei mabasi na miundombinu yake na kuhamia mambo mengine. Hapo founder kafirisika?
Kwa mtazamo huu mtasema Siemens walifirisika kisa walikuwa wanatoa simu ila hawatoi siku hizi, wao waliona simu ni vitu kila mwaka unaumiza kichwa utoe products mpya wakaamua wakomae na mitambo ya energy kama gas turbines na mifumo mikubwa ya umeme duniani.
Kuna watu biashara ikileta changamoto wanahamia kwingine, au profitability ikipungua au threats of new intrants au akifika threshold fulani anaona kukua hakupo tena anahamia kwingine au utaalamu ukipungua labda alikuwa ni mhasibu ila uzoefu wa miaka 30 anaona kwa sasa vijana wanakuja na mambo ya computerized accounting yanamchanganya na hawezi kuwa master tena anabadili service kutoka kuwa mhasibu na kuwa agent. Au mtu kuanzia miaka ya 90 alipata hela sana kwenye clearing & forwarding alikuwa giant ila siku hizi anaona imevamiwa anahamia kwenye betting.
Kuna watu hawakazi kichwa kwenye biashara fulani tu, akisoma mchezo anahama. Badala yake kuna wengine wanakomaa anakopa anafanya ili na lile biashara hiyo hiyo.