Extra miles
JF-Expert Member
- Apr 18, 2018
- 3,652
- 4,972
wakitumia cheat codes za biashara wanatoboa. Tatizo mabadiliko ya kiuchumi duniani yamefanya tubadili uendeshwaji wa biashara tofauti na miaka ya nyuma.Jamani wafanya biashara wenzangu nilicho gundua hapa nchini kila siku mambo hubadilika katika biashara na soko.
Kuna marafiki zangu wawili walipata setback kwenye biashara zao moja alikua na mtaji kati ya 70-80m masuala ya ndoa ya kugawana mali na mke akamuondoa kwenye leri ya biashara mgine alikua ana capital base150-200m aliondolewa kwenye leri ya biashara kwa sera mbovu za uchumi za jpm 2016 Ni lidhani baada ya mda mfupi mwaka au miaka miwili watarudi lerini lakini wapi.
Leo ni meenda kuwajulia hali zao kumbe mambo bado wana jikongoja hawajarudi full kwenye biashara moja gari hana anatumia daladala mgine anatumia gari number 'A' kaipata kwa milioni 6 baada yakuuza harrier tako la nyani aongezee kwenye mtaji wake ilio bakia ndo kanunua hiyo no A.
Jamani kama una mtaji wako utunze kwa makini usiigii kwenye biashara usio jua na huna wakika nao mtaji ukikata kurudusha sio rahisi. Mambo ya meshabadilika sio kama zamani.