Biashara Tanzania ni pasua kichwa. Ukiondolewa kwenye reli, kurudi na kukaa sawa si rahisi

Biashara Tanzania ni pasua kichwa. Ukiondolewa kwenye reli, kurudi na kukaa sawa si rahisi

Daaaah Wakuu ,sitaki kukumbuka ila haina jinsi ku share na kunikumbusha mbali japo sio mbali sana,2016 kipindi cha mwenda zake,yupo kwenye high peak ,Mshua bhana alijilupua kwa kuchukua mkopo au hela za watu Bank ,kwa ajili ya kuzungulishia kwenye biashara zake za mafuta,HFO au kwa lugha ya malkia Heavy Fuel oils, ni mafuta ambayo yanatumika viwandani kwenye ma Boiler, alinunua HFO zipato litre 150,000 kwa ajili ya masoko yake nche ya nchi ya Kenya.
Akafanya biashara na mkenya baada ya kuja yard na kuukagua mzigo na kuona mnzurii sana,akalipa advance nyingine mpka mzigo ufike ndio atalipia kwa njia ya bank,..Mshua akatafuta semi tatu za kukodi Tanker,na unzuri Mshua alikuwa na Mende mbili Scania pulling na trailer zake ,vyuma vikapakia mafuta yrd,vikatoka Dar es salaam vinzuri tu mpaka boarder ya Namanga, Changamoto ndio ikaanzia hapo bhana,tumeonyesha documents na vibali vyote vya mzigo,Duh! polen aisee mikopo sio mchezo
 
Biashara inachangamoto sana.....kuna kipindi nilikuwa na biashara maeneo ya chuo flani biashara ya chakura baada ya ile biashara kuwa inalipa sana nikaingia bank nikapatiwa mkopo wazo likaja nifungue sehemu nyingine mpya mbezi mwisho ile road ya kwenda malamba mawili....basi boashara ilikuwa kama hiyo ya kwanza...nikawa nimegawa baadhi ya vyombo vingene nimeacha kwenye office mama nikambeba na kijana wangu mmoja wa kwenda nae kuanza....kweli kufungua biashara siku za mwanzoni mambo yalikuwa mazuri....kilikuwa kipindi corona inachanganya....bhana we ndo ikatokea ile burn ya no michanganyiko mala masharti mengi...nilipotea kwenye ramani ijawahi kuonekana....izi biashara wengi wanafanya ila hawajui kuwa...mtu anaetoka from the ground kabsa bila kushikwa mkono na kufanikiwa ujue ni kazaliwa na hiyo tabia ya biashara
 
Leri = reli.
Ni kweli boss inahitaji uvumilivu na akili ya ziada kurudi kwenye mstari ukianguka. Muhimu ni kumwomba sana Mungu kukupa utulivu wa akili unapopatwa na majanga kwenye biashara. Yaani hata kama umeanguka kabisa muhimu ni kuhakikisha àkili yako ipo sawa na huendeshwi na mihemko.

Cha kwanza kubali kabisa kwamba tayari maji yamezidi unga inahitaji muda na mbinu kurudi relini. Katika mikakati mipya pambana sana kukwepa kuchukua mkopo. Bora kama una cheti kutafuta ajira ukapiga kwanza huku ukitunza pesa. Kama ajira hakuna anza na ulicho nacho mkononi. Hata kama ni uchinga bora uanzie hapo.

Tatizo wengi wakianguka wanaanza kuwa na presha na kutokukubaliana na hali. Watakurupuka kuuza vitu na kuchukua mikopo na kujikuta kwenye majanga zaidi. KUANGUKA KWENYE BIASHARA ni kawaida ila kurudi tena relini ni wachache wanaoweza.
Wabongo wengi mnaogopa mkopo lakini historia haioneshi kwamba unaweza kutoka kwa kudunduliza mshahara, unachotakiwa kukijua ni kwamba mkopo huwa ni wa kuendeleza biashara siyo wa kuanzisha biashara
 
Nimeisikilza hiyo interview ahsante hiyo ndo biashara
Hiyo video imenikumbusha Kuna jama angu pia kauza sheli lake akaingia kwenye madini nikamuonya sasa hivi mwaka umepita nikimpigia simu zangu hapokee sijui kilicho msibu
Wote mnaongea ila hutakaa uone makanjibai na warabu humu wanalia biashara imefilisika..

Nadhani kuna sehemu tuna kosea wasfrica sie..
Nalo neno
 
Afadhali hao Ndugu zako mitaji yao ilikuwa inapukutika kidogo kidogo, mimi rafiki yangu alienda kuchukua nguruwe 200 mbeya wenyewe thamani ya mil 50,kumbe homa ya nguruwe ilikuwa imeanza kuingia kimya kimya anafika dar anawaswaga zizini kesho yake asubuhi anakuta nguruwe zote zimekufa.
Napewa taarifa rafiki yako amepoteza fahamu yupo rabinisia baada kupata fahamu akasema mapambano yanaendelea😄
Daah nimecheka japo sio kitu cha kucheka😂
 
Mimi mshahara wangu unanitosha... Napata pesa najenga nyumba zangu mdogo mdogo... Nikikaribia kustafu nyumba zangu mbili tatu na fremu zitanilisha...
Biashara ni kipaji sio kila mtu anacho... Na sio kila mtu anaweza kufanya biashara... WaTz wengi mnafilisika kwasabab ya kuiga kufanya biashara kama fulani... WaTz wengi wakiona biashara fulani ina trend basi wote wanaitaka... WaTz wengi sana wanafanya biashara ili waonekana tu wakat ukweli hakuna faida wanayoingiza... WaTz wengi biashara zao ndogo wanataka ziwalipie kodi zisomeshe watoto wale bata na kuhudumia ndug, jambo ambalo haliwezekani kiuchumi ktk biashara...
Bongo hii mtu akiwa na kazi akipata pesa kidogo anataka afanye biashara
Mwingine anakuambia kabisa amefungua sehemu ili asiwahi nyumbani anapotoka kazini aiseee
 
Palikuwa na madon ila walipigwa na upepo mpaka wakapotea .

Tulikuwa na mzee mmoja wa kisambaa anaitwa "Mswaki " alisumbua sana miaka hyo alikuwa na nyumba kadhaa ..Alipotaka kufanya leverage kweny biashar zake maana alikuwa mtu wa mafuso kubeba bidhaa kama matunda hata dili za ngozi.

Alichukua pesa kibao bank kwa riba ya juu ,duh! mambo yakabuma alipotea kabisa aliuza nyuma zilikuwa kama nne akabakiwa na moja na zile fuso ndo zilimtia hasara maana zilipiga mzinga na mzigo ukapotea uliharibika na dereva wake alikufa .

palitokea series za ajali ya magari yake kama ma3 yakiwa na mzigo mpaka mzee alizirai..

Bahati nzuri ni mkewe alipambana nae ila sasa yupo vizuri zaidi ya miaka 20 nyuma .


Walikuwepo wakina Hussen pambakali sasa kimya ,kuvimba kwa zamu.


Biashara sio rahisi kama watu wanavyofikria tulishalima na mzee tukishirikiana na bibi sehemu moja iniatwa Mbugani- mkomazi ,heka kama 6 zilipigwa na maji yalikuja mafuriko mpaka shangazi yangu alikata moto (alizimia)


Ila ndo hivyo maisha yanasonga.
Poleni sana
😀Imenibid nicheke tu ila inahuzunisha
 
Dawa zitaendelea uzika ila faida ndo itashuka
Bro hata huko pia watu wataongezeka na ushindani utakuwa mkali sana. Kule India watu wana viwanda vya vifaa tiba kiasi kwamba huo ushindani sio poa.... huku kwetu bado watu wa madawa na vifaa tiba sio wengi kiasi kwamba kuna baadhi ya vitu vinakua shida kuvipata. Inachagiwa pia na hiyo aina ya biashara pia kutaka shule kichwani. Wanapoendelea kuongezeka vijana wasomi kwenye game huko nako kutachafuka.
 
Back
Top Bottom