Daaaah Wakuu ,sitaki kukumbuka ila haina jinsi ku share na kunikumbusha mbali japo sio mbali sana,2016 kipindi cha mwenda zake,yupo kwenye high peak ,Mshua bhana alijilupua kwa kuchukua mkopo au hela za watu Bank ,kwa ajili ya kuzungulishia kwenye biashara zake za mafuta,HFO au kwa lugha ya malkia Heavy Fuel oils, ni mafuta ambayo yanatumika viwandani kwenye ma Boiler, alinunua HFO zipato litre 150,000 kwa ajili ya masoko yake nche ya nchi ya Kenya.
Akafanya biashara na mkenya baada ya kuja yard na kuukagua mzigo na kuona mnzurii sana,akalipa advance nyingine mpka mzigo ufike ndio atalipia kwa njia ya bank,..Mshua akatafuta semi tatu za kukodi Tanker,na unzuri Mshua alikuwa na Mende mbili Scania pulling na trailer zake ,vyuma vikapakia mafuta yrd,vikatoka Dar es salaam vinzuri tu mpaka boarder ya Namanga, Changamoto ndio ikaanzia hapo bhana,tumeonyesha documents na vibali vyote vya mzigo,wale majamaa ya wanaohusika kuvusha magari upande wa Kenya ,
wakawa wanakaza ,wakawa wasema mambo ambayo sisi tulijua wanataka chochote kitu lakini wapii ,wanasema mmbo yamebadilika kutokana na mfumo wa Sera za nchi,Tukawa wapole tukaona ngoja tuvumulie pale mpakani Namanga mambo yanawenza kuubadilika lakini wapii,tulikaa kalibia miezi miwili tukaona mambo yamekuwa sio mambo,
fikilia gharama za kupark na ulinzi wa magari,plus madereva ma turn boy ,escorter wa mzigo ,mkenya naye anataka aludishiwe hela yake ,Bank nayo hawaelewi wanataka marejesho yao ilikuwa Mshua anapitia kwenye kipindi kigumu sana mpaka ikafikia sukari kupanda na presure juu, Ila tunamshukuru Mungu alirudi kukaa sawa ,japo sio kama mwanzo ku recover ni ngumu mno,Aliunza baadhi za nyumba,mzigo bei ya hasara na magari pia ili ikawe sawa,