Biashara tofauti za kuniingizia 50,000/= kwa siku

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2019
Posts
1,042
Reaction score
2,005
Habari wanajamvi, mimi nipo Tanga lakini maeneo ya kijijini. Kwa muda niliokaa huku mambo ya kilimo yamegoma hasa kwa sababu ya hali ya hewa. Sasa nikafikiri kufungua biashara tofauti hata mbili au tatu zenye mtaji mdogo huko Dar ili niweze kuingiza hamsini kwa siku.

Kwanini nimechagua Dar ni kwa sababu Dar kuna ndugu zangu ambao wakati mwingne naweza kuwatumia kuangalia mambo yanavyoenda, lakini la pili kutoka hapa kwenda Dar nauli ni kama sh 15,000/=, lakini lingine Dar kuna mzunguko wa pesa tofauti na huku kijijni tulipo.

Naomba wazoefu waniongoze na kutoa ushauri naweza fungua vitu gani na kwa mtaji wa kiasi gani ili nikianza kupata kafaida angalau kuanzia 50,000/= kwa siku. Nitashukuru kwa hilo wanajamvi.
 
Asilimia kubwa ya biashara nyingi halali huzalisha faida ya kati ya 17% had 20% kwa mauzo. Faida ya 50,000 kwa siku ni mauzo ya kati ya 250,000 hadi 300,000 kwa makadirio. Kwenye hiyo faida tunatoa hapo gharama za uendeshaji ambazo siyo rafiki sana kwa nchi yetu. Unajikuta gharama za uendeshaji ni nusu ya faida unayopata. Hivyo inakulazimu kuuza walau 500,000 hadi 600,000 ili ulaze 50,000.

Tukija kwenye mauzo hayo, ni mtaji kiasi gani? Hapa itategemea na aina ya biashara na location. Mfano: Biashara ya jiko la chips, chomachoma, chapati za kisasa mix supu inakulazimu uwe na mtaji usiopungua 4 milion.
 
Dah mnakatisha tamaa vijana ambao ndio wanataka kuanza biashara ya chips yaani mtaji uwe 4 mil hapo labda inafanyika Kariakoo ila sisi wengine tumeifanya na tunaijua.
 
Toa mchanganuo wako basi tuelimike wengi.
Dah mnakatisha tamaa vijana ambao ndio wanataka kuanza biashala ya chips yani mtaji uwe 4mil hapo labda inafanyika kaliakoo ila sisi wengine tumeifanya na tunaijua
 
Dah mnakatisha tamaa vijana ambao ndio wanataka kuanza biashala ya chips yani mtaji uwe 4mil hapo labda inafanyika kaliakoo ila sisi wengine tumeifanya na tunaijua

Sasa kama umeifanya na unaijua si uweke mchanganuo wako?
Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba.
 
mkuu, kwanza na wewe ungesema una pesa ngapi watu waweke mipango mezani kulingana na pesa yako.

anaweza akaja raia na ishu ya mtaji wa 850M tukakimbia uzi
Wee mwenyewe unaona iyo 850M ni nyingiiiiiii! Si ni kama Dollar 380 hivi. Dah
 
Sasa kama umeifanya na unaijua si uweke mchanganuo wako?
Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba.
Hiyo biashara unaweza kuwa hata na laki tano na ukaifanya inategemea unataka kufanyia kwenye mazingira gani. Mfano mimi nilianza na kuuza kuku tu kipindi hiko Majohe KWA Ngozoma ambao nilikuwa nanunua sh elfu 5 kisha nawatengeneza kuanzia paja kidali na firigisi halafu miguu na kichwa na utumbo kidogo nilikuwa natengeza kitu wanaita kifurushi ambacho nilikuwa nauza shilingi mia tano hapo mtaji wa kuku kujumlisha karai na mafuta na mkaa vilikuwa elfu 80 pamoja na sehemu.

Ndio nilivyoanza kwenye kuku nikawa nalaza elfu 20 mpaka 30 ila nikimaliza kuku nilikuwa nalaza mpaka Eflu 50 na huo ni mtaji wa elfu 80 baadae niliamua kupanda kidogo ndio nikaweka na chips ambao mtaji ukawa umefika huko ila SASA baada ya kuanza kuweka muonekano vyema kama kutumia majiko ya gesi umeme ndio mtaji ulifikia mpaka mil 1.

Hivyo msikate tamaa mnaweza kuanza na kidogo ulichonacho kulingana na biashara. Mimi SASA hivi sifanyi hiyo biashara ni miaka 2 SASA nipo napambana na biashara nyingine ambazo mtaji wake ni mkubwa kidogo lakini nimeupatia kupitia hiyo biashara niliyoanza nayo, kikubwa usione aibu kufanya biashara ambayo utaona inakuingizia kipato.
Sasa kama umeifanya na unaijua si uweke mchanganuo wako?
Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba.
 
Kama unategemea ndugu kwenye hiyo biashara, jipange!
 
Labda Betting
Mtaji=300,000
Odds=1.5
Kodi=15%

300,000×1.5=450,000

450,000×15÷100=67,500

450,000-67,500=382,500

Faida 82,500

Lakin sio kila siku utabet au utapata kuna kuangukia pua.
ila Jamii Forums
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…