Abdul Mganyizi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2019
- 1,042
- 2,005
Habari wanajamvi, mimi nipo Tanga lakini maeneo ya kijijini. Kwa muda niliokaa huku mambo ya kilimo yamegoma hasa kwa sababu ya hali ya hewa. Sasa nikafikiri kufungua biashara tofauti hata mbili au tatu zenye mtaji mdogo huko Dar ili niweze kuingiza hamsini kwa siku.
Kwanini nimechagua Dar ni kwa sababu Dar kuna ndugu zangu ambao wakati mwingne naweza kuwatumia kuangalia mambo yanavyoenda, lakini la pili kutoka hapa kwenda Dar nauli ni kama sh 15,000/=, lakini lingine Dar kuna mzunguko wa pesa tofauti na huku kijijni tulipo.
Naomba wazoefu waniongoze na kutoa ushauri naweza fungua vitu gani na kwa mtaji wa kiasi gani ili nikianza kupata kafaida angalau kuanzia 50,000/= kwa siku. Nitashukuru kwa hilo wanajamvi.