Biashara tofauti za kuniingizia 50,000/= kwa siku

Mkuu, gharama za kusafirisha si kubwasana?
Hapana wala si kubwa sababu mimi nachukulia mizigo mikoa ya karibu japo changamoto zipo lakini nakabiliana nazo, ni biashara nzuri yenye faida ila unatakiwa ujitoe sababu kuna kipindi cha hasara hasa kama vita imepamba moto
 

Umeweka kitaalamu sana
 
Labda Betting
Mtaji=300,000
Odds=1.5
Kodi=15%

300,000×1.5=450,000

450,000×15÷100=67,500

450,000-67,500=382,500

Faida 82,500

Lakin sio kila siku utabet au utapata kuna kuangukia pua.

Unaleta ujinga kijana
 
4m kwa kuanzia ni nyingi sana kwa mtaji wa chips na supu bro. Na assume kwamba chumba cha biashara/sehemu ya biashara analipa elfu 50 kwa mwezi, akiwa na mtaji hata wa 1m anasogeza vizuri kabisa, provided anapata sehemu ambayo ina mzunguko mzuri na watu wengi
 
Tanga sehemu gani mkuu?
 
Mkuu, kwanza na wewe ungesema una pesa ngapi watu waweke mipango mezani kulingana na pesa yako.

Anaweza akaja raia na ishu ya mtaji wa 850M tukakimbia uzi
Nilivyomuelewa mimi haitaji kuweka kiasi cha mtaji alichonacho. Sisi wadau tumwambie biashara ya kuingiza daily profit ya 50k. Ukisema mtu ataje mtaji wa 850m haitakuwa sawa kwa sabu hiyo italeta profit tofauti.
 
Nilivyomuelewa Mimi haitaji kuweka kiasi cha mtaji alichonacho. Sisi wadau tumwambie biashara ya kuingiza daily profit ya 50k. Ukisema mtu ataje mtaji wa 850m haitakuwa sawa kwa sabu hiyo italeta profit tofauti.
Kweli mkuu umenisoma ,mm lengo langu nijue miradi gani yaenye mitaji kidogo ambayo makusanyo yake fada nikapata 50,000 kwa sikufano hapa nimepata 10,000 ,hapa 20,000, hapa 10,000 na maeneo mengne.Hapo ndoo nimekwama
 
Kuna mtu hapo juu nimemuona anataka kuanzisha biashara yake Dar es salaam kwa kutegemea macho ya ndugu zake, aiseee ni utalia....kama mtoto mchanga. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilivyomuelewa mimi haitaji kuweka kiasi cha mtaji alichonacho. Sisi wadau tumwambie biashara ya kuingiza daily profit ya 50k. Ukisema mtu ataje mtaji wa 850m haitakuwa sawa kwa sabu hiyo italeta profit tofauti.
Mkuu vp hali
 
Kama upo serious mkuu fanya biashara ya mkaa mkuu hautojutia, kama upo karbu na handeni unaweza fanya proces za kuchoma mkaa angalau uanze na gunia 150 ambapo gharama za kuchoma sio chini ya laki5 na gharama za kusafirisha mpaka dar kila gunia ni 6k
kibali cha tfs laki mbil kwa mwaka
gharama za kibanda hapa dsm unaeza pata kuanzia elf 30 mpk 40 kwa mwez kodi ya pango
kila gunia hapa dsm lnauzwa elfu 25 mpka 30 kama ukibahatika kuuza gunia 3 au 4 kwa siku hyo utakuwa na faida ya uhakika
25000*4=100k
faida katika kila gunia ni sh 10k mpk 15k
ukihtaji mchanganuo zaidi nichek 0764064872,,,0786909280
 
Kutokana na maelezo ya mtoa uzi. Na namna anavotaka biashara ifanyike kwa uhalisia inakua ngumu kidogo. Kwa sabab kwanza kabisa biashara yoyote inahitaji usimamizi wa hali ya juu. Japo kuna biashara nyingine haziitaji sana. Ila kwa biashara za mtaji mdogo za kukuingizia kiasi hicho cha pesa zinahitaji usimamizi na huwezi kulikwepa hilo,


ila kwa haraka haraka biashara za kufungua hapo ni biashara ya kuuza juisi ya miwa, juisi ya matunda na bites, hii inakuwa kwenye contena moja ambalo unahakikisha limekaa kwenye sehem yenye mzunguko mkubwa wa watu. Pili unaweza ukafungua banda la uwakala yaani ukatoa huduma za mpesa, airtel money etc japo hela hautaiona kila siku ila mwisho wa mwezi ukiipata utagawanya kwa 30 ili ujue kwa siku ulipata shi ngapi. Sasa sijajua wew una mtaji wa kiasi gani. Nisije nikaandika list kubwa kumbe huwezi kufungua vyote.


Sasa point hapo ni kuwa, biashara za siku hizi sio za utajiri wa haraka kama zamani, naamanisha usitegemee faida kubwa kwa wakati mmoja. Faida unatakiwa kuikusanya kidogo kidog kutoka kwenye sehem mbali mbali, hivyo basi kupitia uo uwakala hizo juisi na kam kuna kuwa na wazo jingine unaweza ukaokoteza 20k kwa 10k mpaka ifikie rengo lako. Na kama rengo halifiki usipate taabu wew tengeneza wazo lingine la biashara uweke pesa au kama pesa zimeisha tumia faida utakazopata kwenye mzunguko wako.


Mawazo yote ya biashara ni mazuri. Swali je wew unaweza ukafanya? Kutokana na mtaji wako, umri wako, kipato chako, dini yako, imani yako, mazingira yako, elimu yako, ustadi wako, usimamizi wako n.k kama ukiamua kufanya biashara jifunze kutokuchagua sana na ujifunze kuthubutu maana ata ukishindwa utakuwa umejifunza.
 

Umeandika vyema sana mkuu
 
Mtaji wa kuanzia ni ngapi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…