Leloo June
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 1,001
- 933
Biashara hujaanza ushapiga hesabu kupata elfu 50 Kwa siku utasubiri sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, gharama za kusafirisha si kubwa sana?Sasa hivi nafanya biashala ya Nafaka napeleka burundi na kongo
Hapana wala si kubwa sababu mimi nachukulia mizigo mikoa ya karibu japo changamoto zipo lakini nakabiliana nazo, ni biashara nzuri yenye faida ila unatakiwa ujitoe sababu kuna kipindi cha hasara hasa kama vita imepamba motoMkuu, gharama za kusafirisha si kubwasana?
Asilimia kubwa ya biashara nyingi halali huzalisha faida ya kati ya 17% had 20% kwa mauzo. Faida ya 50,000 kwa siku ni mauzo ya kati ya 250,000 hadi 300,000 kwa makadirio. Kwenye hiyo faida tunatoa hapo gharama za uendeshaji ambazo siyo rafiki sana kwa nchi yetu. Unajikuta gharama za uendeshaji ni nusu ya faida unayopata. Hivyo inakulazimu kuuza walau 500,000 hadi 600,000 ili ulaze 50,000.
Tukija kwenye mauzo hayo, ni mtaji kiasi gani? Hapa itategemea na aina ya biashara na location. Mfano: Biashara ya jiko la chips, chomachoma, chapati za kisasa mix supu inakulazimu uwe na mtaji usiopungua 4 milion.
Labda Betting
Mtaji=300,000
Odds=1.5
Kodi=15%
300,000×1.5=450,000
450,000×15÷100=67,500
450,000-67,500=382,500
Faida 82,500
Lakin sio kila siku utabet au utapata kuna kuangukia pua.
Za Mtumba au dukaniTAFUTA MILIONI MOJA UZA NGUO
4m kwa kuanzia ni nyingi sana kwa mtaji wa chips na supu bro. Na assume kwamba chumba cha biashara/sehemu ya biashara analipa elfu 50 kwa mwezi, akiwa na mtaji hata wa 1m anasogeza vizuri kabisa, provided anapata sehemu ambayo ina mzunguko mzuri na watu wengiAsilimia kubwa ya biashara nyingi halali huzalisha faida ya kati ya 17% had 20% kwa mauzo. Faida ya 50,000 kwa siku ni mauzo ya kati ya 250,000 hadi 300,000 kwa makadirio. Kwenye hiyo faida tunatoa hapo gharama za uendeshaji ambazo siyo rafiki sana kwa nchi yetu. Unajikuta gharama za uendeshaji ni nusu ya faida unayopata. Hivyo inakulazimu kuuza walau 500,000 hadi 600,000 ili ulaze 50,000.
Tukija kwenye mauzo hayo, ni mtaji kiasi gani? Hapa itategemea na aina ya biashara na location. Mfano: Biashara ya jiko la chips, chomachoma, chapati za kisasa mix supu inakulazimu uwe na mtaji usiopungua 4 milion.
Sio wewe ndio mjinga?Unaleta ujinga kijana
Tanga sehemu gani mkuu?Habari wanajamvi, mimi nipo Tanga lakini maeneo ya kijijini. Kwa muda niliokaa huku mambo ya kilimo yamegoma hasa kwa sababu ya hali ya hewa. Sasa nikafikiri kufungua biashara tofauti hata mbili au tatu zenye mtaji mdogo huko Dar ili niweze kuingiza hamsini kwa siku.
Kwanini nimechagua Dar ni kwa sababu Dar kuna ndugu zangu ambao wakati mwingne naweza kuwatumia kuangalia mambo yanavyoenda, lakini la pili kutoka hapa kwenda Dar nauli ni kama sh 15,000/=, lakini lingine Dar kuna mzunguko wa pesa tofauti na huku kijijni tulipo.
Naomba wazoefu waniongoze na kutoa ushauri naweza fungua vitu gani na kwa mtaji wa kiasi gani ili nikianza kupata kafaida angalau kuanzia 50,000/= kwa siku.Nitashukuru kwa hilo wanajamvi.
Nilivyomuelewa mimi haitaji kuweka kiasi cha mtaji alichonacho. Sisi wadau tumwambie biashara ya kuingiza daily profit ya 50k. Ukisema mtu ataje mtaji wa 850m haitakuwa sawa kwa sabu hiyo italeta profit tofauti.Mkuu, kwanza na wewe ungesema una pesa ngapi watu waweke mipango mezani kulingana na pesa yako.
Anaweza akaja raia na ishu ya mtaji wa 850M tukakimbia uzi
Kweli mkuu umenisoma ,mm lengo langu nijue miradi gani yaenye mitaji kidogo ambayo makusanyo yake fada nikapata 50,000 kwa sikufano hapa nimepata 10,000 ,hapa 20,000, hapa 10,000 na maeneo mengne.Hapo ndoo nimekwamaNilivyomuelewa Mimi haitaji kuweka kiasi cha mtaji alichonacho. Sisi wadau tumwambie biashara ya kuingiza daily profit ya 50k. Ukisema mtu ataje mtaji wa 850m haitakuwa sawa kwa sabu hiyo italeta profit tofauti.
Dukani bossza Mtumba au dukani
Mkuu vp haliNilivyomuelewa mimi haitaji kuweka kiasi cha mtaji alichonacho. Sisi wadau tumwambie biashara ya kuingiza daily profit ya 50k. Ukisema mtu ataje mtaji wa 850m haitakuwa sawa kwa sabu hiyo italeta profit tofauti.
Akili zake ndizo zimemtuma aandike kama alivyoandika hapo juuUnaleta ujinga kijana
hongeraSasa hivi nafanya biashala ya Nafaka napeleka burundi na kongo
Kutokana na maelezo ya mtoa uzi. Na namna anavotaka biashara ifanyike kwa uhalisia inakua ngumu kidogo. Kwa sabab kwanza kabisa biashara yoyote inahitaji usimamizi wa hali ya juu. Japo kuna biashara nyingine haziitaji sana. Ila kwa biashara za mtaji mdogo za kukuingizia kiasi hicho cha pesa zinahitaji usimamizi na huwezi kulikwepa hilo,
ila kwa haraka haraka biashara za kufungua hapo ni biashara ya kuuza juisi ya miwa, juisi ya matunda na bites, hii inakuwa kwenye contena moja ambalo unahakikisha limekaa kwenye sehem yenye mzunguko mkubwa wa watu. Pili unaweza ukafungua banda la uwakala yaani ukatoa huduma za mpesa, airtel money etc japo hela hautaiona kila siku ila mwisho wa mwezi ukiipata utagawanya kwa 30 ili ujue kwa siku ulipata shi ngapi. Sasa sijajua wew una mtaji wa kiasi gani. Nisije nikaandika list kubwa kumbe huwezi kufungua vyote.
Sasa point hapo ni kuwa, biashara za siku hizi sio za utajiri wa haraka kama zamani, naamanisha usitegemee faida kubwa kwa wakati mmoja. Faida unatakiwa kuikusanya kidogo kidog kutoka kwenye sehem mbali mbali, hivyo basi kupitia uo uwakala hizo juisi na kam kuna kuwa na wazo jingine unaweza ukaokoteza 20k kwa 10k mpaka ifikie rengo lako. Na kama rengo halifiki usipate taabu wew tengeneza wazo lingine la biashara uweke pesa au kama pesa zimeisha tumia faida utakazopata kwenye mzunguko wako.
Mawazo yote ya biashara ni mazuri. Swali je wew unaweza ukafanya? Kutokana na mtaji wako, umri wako, kipato chako, dini yako, imani yako, mazingira yako, elimu yako, ustadi wako, usimamizi wako n.k kama ukiamua kufanya biashara jifunze kutokuchagua sana na ujifunze kuthubutu maana ata ukishindwa utakuwa umejifunza.
Mtaji wa kuanzia ni ngapi??Kama upo serious mkuu fanya biashara ya mkaa mkuu hautojutia, kama upo karbu na handeni unaweza fanya proces za kuchoma mkaa angalau uanze na gunia 150 ambapo gharama za kuchoma sio chini ya laki5 na gharama za kusafirisha mpaka dar kila gunia ni 6k
kibali cha tfs laki mbil kwa mwaka
gharama za kibanda hapa dsm unaeza pata kuanzia elf 30 mpk 40 kwa mwez kodi ya pango
kila gunia hapa dsm lnauzwa elfu 25 mpka 30 kama ukibahatika kuuza gunia 3 au 4 kwa siku hyo utakuwa na faida ya uhakika
25000*4=100k
faida katika kila gunia ni sh 10k mpk 15k
ukihtaji mchanganuo zaidi nichek 0764064872,,,0786909280