Biashara tofauti za kuniingizia 50,000/= kwa siku

Kuna siku nilikuwa natoka Dodoma naenda Iringa, ilikuwa jioni, ikanilzimu ningoje gari kutoka Arusha, KIMOTCO, ikiwa imehitimu saa 11 Jioni, gari ilikuwa imeshawasili pale, tukaanza safari, pembeni yangu alikuwa amekaa mdada wa makamo, umri ni kati ya miaka 27-33.

Kwa kawaida mimi sio mtu wa stori, ila wakati nimefika Migori kwa ajili ya kupata hiki na kile wakati huo giza likiwa tayari limeshatanda, ilinibidi nikoleze stori na yule dada na hapa tulikuwa tayari kwa kiasi fulani tumeanza kuzoeana, na hata hivyo nilikuwa nimekaa nae meza moja.

Alichoniambia kilinifungua sana, akasema, "kama unataka pesa, ukimaliza masomo yako, karibu mpakani, Tunduma, TZ na ZAMBIA" maelezo yake tukaendeleza kwenye gari. Anasema biashara hunoga sana kwenye mipaka, watu wanapiga hela vibaya mnooo, kwa mfano yeye, awali alianza kununua nguo Kenya, tena kwa bei rahisi sana, good enough ni kwamba, quality ya nguo za Kenya ni kubwa sana, anakuja kuuza Dodoma, baadae akaanza kupeleka mzigo Zambia, kumbe hata siku ile alikuwa na mabalo anayasafirisha, ilikuwa jumatano, akaniambia hapo akikaa sana ni mpaka Jumapili, mzigo umeisha, baadae anatoka Dar na Vifaa vya Elekroniki anapeleka Arusha kwa sababu vina gharama kubwa mno', akisema hata nae hajui ni kwanini.

Kwa maelezo yake, alinambia mpaka siku ile niliyokutana nae, hakuwa hata na mwaka kwenye ile biashara, ila kuna uwekezaji mkubwa sana ameanza kuufanya Dodoma, nilikuwa na mawasiliano nae, akaniambia wiki mbili baadae angekuwa Dodoma kununua eneo ili baadae aje kukata vipande na kuliuza kwa ajili ya makazi.

Ni hayo kwa leo
 
Mkuu, kwanza na wewe ungesema una pesa ngapi watu waweke mipango mezani kulingana na pesa yako.

Anaweza akaja raia na ishu ya mtaji wa 850M tukakimbia uzi
Kwa mtaji huo wa 850M unaotaja na nia na lengo la mleta hoja wa kuzalisha 50,000/= kwa mwezi haviendani!
 
Ndo ukiskia Prof. Jay anachangiwa Matibabu sijui Serikali inamtibu ndo ujue Mtaji wa 200m sio kitu sembuse 4m
Dah mnakatisha tamaa vijana ambao ndio wanataka kuanza biashara ya chips yani mtaji uwe 4mil hapo labda inafanyika Kariakoo ila sisi wengine tumeifanya na tunaijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…