Biashara ya Baa sio ya kuiwekea matumaini sana ikianza kujaza wateja, wateja wana tabia ya kukizoea kiwanja ila ghafla huhama kwa pamoja

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Nimewahi kuziona Baa kadhaa ambazo sikuwahi kudhania kabisa zitakuja kupoteza wateja, Wateja walihama kwa style za kimafia sana, yani vuuup!! ghafla bar inaanza kuwa tupu !! sio kwamba bar imefirisika, sio kwamba warembo wamepungua, sio kwamba hakuna service nzuri, n.k. yaani ndio hivyo, Vuup!

Ni kama vile wateja huwa wapo bluetooth connected, akili zao zimeunganika, wakiamua kuanza kuja utakusanya sana pesa zao, ila wakiamua kuhama ni kwa style hio hio kama walivyokuja.
 
Hiyo biashara mfano ya Bar,mf.Kitambaa cheupe,Element,Makuti.msamvu,Sunrise Mbeya,Fournight Moro,msamvu pub,Frolida Bar,Gloneny 88,Pale zinapokuwa kwenye chat,wekeza kwenye real estate,wekeza kwenye vituo vya mafuta,nunua malori ya mchanga,Jenga apartment n.k
 
Kuna wateja huwa wanafata wateja Fulani,hawafati huduma,mazingira Wala wadada wa bar..akihama huyo mteja kimkoa, au akahamia bar nyingine utaona Kuna baadhi ya wateja wanapungua
Machawa ndio wazinguaji
 
Biashara zina siri nyingi,,,, kuna mtu nAmnjua yuko kwenye hii industry 10+years ila hajawahi kuchuja,,,alafu chimbo la kawaida tu
 
Nimewahi kuziona Baa kadhaa ambazo sikuwahi kudhania kabisa zitakuja kupoteza wateja, Wateja walihama kwa style za kimafia sana, yani vuuup!! ghafla bar inaanza kuwa tupu !! sio kwamba bar imefirisika, sio kwamba warembo wamepungua, sio kwamba hakuna service nzuri, n.k. yaani ndio hivyo, Vuup!

Ni kama vile wateja huwa wapo bluetooth connected, akili zao zimeunganika, wakiamua kuanza kuja utakusanya sana pesa zao, ila wakiamua kuhama ni kwa style hio hio kama walivyokuja.
Ukifika Ifakara usikose kwenda kiwanja kipya Twins Pub maeneo ya posta, jamaa Hana mzuka wa mademu Wahudumu wabovu sana, aendelee kujipanga, uwekezaji mzuri ila Wahudumu zero bar haina pisi kali hapo kawekeza matope , TV nyingi ila hana mtu wa maana wa kutoa furaha kwa mechi za siku hio hovyo
 
Ukiona imeanza kupoteza wateja ihamishie sehemu nyingine wataifuata huko!
 
hakuna kitu kinaitwa vuup mkuu .hamna na hakuna huo muujiza wa kutoweka wateja kama Mizuka. It's a process . kuloose wateja ni jambo linaweza tokea katika biashara yoyote isipokua unazisemea bar kwasababu unawaona wateja wakiwa wamerundikana kwahyo inakuwa rahisi ww kufanya judgment, tofauti na biashara nyingine ambapo ili kuona wateja wamepungua lazima ushike daftari la mauzo uangalie.
 
Walevi hufatana, na bar nyingi hazijijui ni za namna gani.
Leo bar tulivu, kesho mziki mkubwa, mara visingeli nk.

Ila sisi mapro huwa tunatulia tu kwenye vigrocery karibu na majumbani mwetu, tunafata pombe tu sio malaya na mpira ni gambe tuu.
 
Back
Top Bottom