Biashara ya boda boda

mimi nilimpa kaka yangu,tukaelewana kwa wiki anipe elf 25000, ila alichonifanyia,Mungu ndo anaona
 
P
mimi nilimpa kaka yangu,tukaelewana kwa wiki anipe elf 25000, ila alichonifanyia,Mungu ndo anaona
Pole ndugu ila biashara hainaga ukaka, umjomba, wala usista! Bora hata mtu baki anaweza kukuogopa kidogo lakini si ndugu yako! Maana anajua hata akiharibu hutamstaki wala kumfunga!
 
Biashara hii wengi walipiga chini, iwe kwa mkataba au bila mkataba changamoto zake ni nyingi na zinaleta stress, kwa upendo kabisa tafuta idea nyingine sio hii, Mara nyingi mfaidika ni dereva
 
Hovyo kama huna cha kuongea kaa kimya dharau ni kitu kibaya sana ....aku
 
[emoji121]
VIZURI SANA MR.OPPORTUNIST.
 
Biashara ya boda boda ni nzuri, ila inategemea na aina ya madereva unaowapata, na aina ya mfumo unaotaka kuutumia. Njia ya mkataba ndio nzuri zaid kwani inakuwa haikupi stress. Madereva wako wengi ila madereva wazuri ni wachache sana. Cha msingi kama unaweza tafuta dereva aliye mzuri ongea naye awe kama msimamizi uwe unamlipa na kazi yake iwe ni kuwatafuta wenzake ambao anaona wanafaa(maana yeye ni mzoefu) na pia awe anahakikisha madereva wanaleta fedha kwa wakati(yaani wasipokutumia ww unaongea na huyo msimamizi awafuatilie kwa sababu ndio kazi yake na unamlipa). Hivyo nadhani utafanikiwa. Mm ninatumia njia hiyo na nina boda boda nyingi tu.
Pia suala la muda wa mkataba linategemea na makubaliano ya wewe pamoja na dereva wako, penda kumpa flexibility dereva ajiangalie uwezo wake wa kufanya marejesho.
Ipo ya miezi 8@15,000 per day, miezi 10@ 12,000 per day, miezi 11@ 11,000 per day na miezi 12 au wengine miezi 13@ 10,000 per day.
 
Pole kwa hiyo uliamua kuachana na hiyo biashara
 
Utaendesha mwenyewe....???
Utanyanganywa.
Utampa dereva..??
Itaibiwa
Achana na hiyo biashara kichaa


Biashara kichaa kwako boss mbona wengine wanapiga pesa kupitia biashara ya bodaboda,acha kukatisha tamaa wengine kwa kuwa wewe umeshindwa.hata kama uliwahi ibiwa pikipiki akukua na ulazima wa kumwambia mtu aasifanye ungetoa maoni yako juu ya changamoto ulizo pitia
 
Boda boda kama hauna shuguli nyingine iendeshe mwenyewe, inalipa sana...la sivyo uifanye kama biashara ya kukusaidia kulipa kodi na hela ya mboga.
Nimekutana na watu wawili watatu baada ya kuona mishahara haikidhi (wasomi) wakaamua kuendesha boda boda...wote hawatafuti tena kazi.
Tatizo ni wale boda boda mapepe, wanafanya hio kazi ionekane ya wendawazimu.
 
Kweli kabisa.
 
Biashara pasua kichwa kwasababu muendeshaji anakuwa na chuki kila akileta hesabu so roho ya gundu ndio tatizo
 
Pole kwa hiyo uliamua kuachana na hiyo biashara
Biashara zote pasua kichwa hakuna biashara rahisi bodaboda mbona wengine wanafanikiwa na magari hivohivo na maduka hivohivo hakuna biashara rahisi muhimu ni kujipanga tu na kukubali changamoto,mfano bodaboda mpaka inakamilika mpya ni kama 2500000,dereva kila wiki hssabu 50000 service inategemea kwa wiki wiki mbili au mwezi inategemea na oil.kwa mwezi unaweza kupata 170000.muhimu hesabu zako uzieke sawa
 
Mkuu hapa umetoa mwanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…